Nyota zenye bahati zaidi?

Rakims
0

 Katika mlolongo wa nyota 12 basi kuna nyota tatu ambazo hizi ni nyota zenye bahati zaidi kuliko zingine na zenye mafanikio zaidi katika bahati nasibu;


YA KWANZA:

Ya kwanza ni nyota ambayo ukitizama kwenye mfumo mzima wa nyota 12 basi utakuta inatawaliwa na sayari ya bahati. 

Ambayo ni sayari tegemezi kwa wengi kuangalia bahati zao zipo wapi na safari zao za maisha ziko vipi na hata aspects za matarajio ya mtu yaani aspects za future yake huangaliwa hapo. 

Msikufuru aspect inayozungumziwa hapa ni viewing ya mafanikio ya mtu. Hivyo nyota ya kwanza kabisa katika nyota 3 zenye bahati tutaipa nyota ya Kausa yaani Saggitarius ama kwa kiswahili ni Mshale 

ambapo mshale ni nyota ya 9 katika mlolongo wa nyota 12 nayo ni nyota yenye bahati zaidi kuliko nyota zote.

Kila nyota ina sifa zake lakini kwa bahati ni nyota hii inayo milikiwa na Sayari ya mapato na iliyoko chini ya usimamizi wa malaika Israfiil ama Rafael kwa wakristo. 

Nae ni malaika mwenye kupuliza baragumu siku ya Qiyama yaani Judgement Day au Siku ya hukumu.

Ukikuta una nyota hii na huna bahati. Basi rekebisha bahati yako 

Kwa maana bahati yako hukwamishwa na mahusiano (Mwanamke/mwanaume) achana nae. Maana utajikuta kwa uchumi kila unalofanya hufanikiwi 

na hata ukiwa kwenye mahusiano ni mkosi mtupu heri yako wewe ni ndoa maana ukiwa kwenye mahusiano pesa hazikai mkononi na unakuwa ni mwenye kusingiziwa maneno. na ukiwa mzinzi basi mizimu itakusumbua sana hivyo utatakiwa uchague kati ya Mwenyezi Mungu au Mizimu. 

Na ukichagua mwenyezi Mungu umeshukuru Ukichagua mizimu umekufuru za kuambiwa changanya  na zako. 


YA PILI:

Yapili ni nyota ambayo ukitizama kwenye mfumo mzima wa makundi nyota 12 ni nyota inayo tawaliwa na sayari ambayo hutizamwa na wanajimu wote kama sayari ya Mapenzi na mahusiano zaidi 

Na hii ni nyota yenye kutawala mlango wa saba yaani mlango wa Mahaba na mahusiano ya mtu hivyo, katika bahati zaidi tutaipa nyota ya Saba ambayo ni nyota ya Miizaan ama Libya ambayo kiswahili ni Mizani

Hii ni nyota ambayo inatawaliwa na Sayari ya Zuhura amba Venus ambayo inakuwa chini ya usimamizi wa malaika An'yail ama Hananel, jina lingine ni Anael ama Aniel 

Ambaye ni malaika anaetawala na kusimamia doria mbinguni inaamika kwa imani za wengine kuwa ni malaika anaesimamia hisia za watu katika mahusiano ya  ndoa na mapenzi.

Hivyo kwa bahati tunaipa nafasi ya pili nyota ya Mizani.

Ikiwa una nyota hii na huna bahati basi Punguza Ukatili, Hamaki na Umalaya na ujitahidi kudumu katika mahusiano maana ukiendekeza hayo bahati yako huja uzeeni unapokata tamaa. Jitahidi kushika ibada

YA TATU:

Ya tatu ni nyota ambayo ukitizama kwenye mfumo wa makundi nyota 12 ni nyota inayotawala NYOTA ama kwa maneno ya kinajimu huitwa sayari pia. 

Yaani the Sun (Jua) ambayo ni msimamizi wa nishati bora ya asilia ya uhai.

Ambapo kinajimu ni sayari inayohusishwa na Utajiri tofauti yake na Sayari za nyota mbili zilizopita.

  • Jupiter ni sayari ya Mapato
  • Venus   ni  sayari ya pesa
  • Sun       ni Sayari ya Utajiri
Hivyo nafasi ya tatu ya nyota zenye bahati zaidi inachukuliwa na nyota ya kitajiri nyota ya Mfalme wa nyika Asad ama Leo kwa kiswahili ni Simba. ambayo ni nyota pia inahusishwa na bahati ya kamari hivyo ukitaka kujua bahati yako ya kamari ipo vipi angalia nyota ya simba imekaa wapi kwenye chart yako ya kuzaliwa.
 
Hii ni nyota ambayo inatawaliwa na Malaika Raukayail yaani Uriel kwa wakristo ambaye ni malaika mwenye kutambulika zaidi kwa kuwa.

Alisaidia katika kumzika Adam na Abel vile vile ndio kiongozi wa malaika aliyekuwa anatizama milango iliyochorwa damu ya Kondoo Egypt.

Kipindi ambapo Mwenyezi Mungu alimwambia Musa awaambie wana waisrael kuchinja kondoo na Kupakaa damu milango kipindi cha Ugonjwa wa Tauni hivyo ule mwanga uliokuwa unamulika kukagua milango. 
kiongozi wake alikuwa ni malaika Uriel ambaye pia ni mwenye kushikiria funguo za shimo siku za mwisho 

nae ndiye aliyemuongoza Ibrahim kuelekea magharibi kipindi hicho,

Nitakuja kuwachambulia malaika mmoja mmoja na historia nguvu na kazi zake na elimu za kuwatumia kwa idhini ya mwenyezi Mungu

.Hivyo kwa nyota ya bahati zaidi nafasi ya TATU tunaipa nyota ya Asad king of the jungle.

Ikiwa una nyota hii na huna bahati pole; 
Kwa maana ni nyota yenye bahati sana na kila mwenye nayo huonekana na watu hivyo, Jitahidi kurekebisha Ukali na pia rekebisha jini wa mali uliye nae hakikisha hauna urafiki na Incubus au Succubus yaani mahaba dume au Jike

Wasiliana nasi

Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia email lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.

Unaweza kutupata kwa kupitia Email, nambari za simu,kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,

Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.

Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na rakimsspiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.

Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa members pekee;

Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia

Wasiliana nasi kupitia:-


Rakimsspiritual@gmail.com

au

mnajimu@unajimu.com


WhatsApp number


+255 783 930 601


Rakims

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !