
Nyota ya Kaa (Cancer)
Hii ni nyota ya nne katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 Juni hadi 22 Julai au wenye majina yalio anza na herufi D au H au P.
Asili yao ni Maji. Asili yake ni Jike. Maada yake ni maji. Ubora wake ni Cardinal.
Kaa ni nyota ya upokezi, kufikiria, huruma, fadhili, hisia, hai, werevu na angavu.
Sayari yao ni Mwezi (Moon). Mwezi ni Satelaiti ya asili ya dunia, inayoonekana (hasa usiku) kwa mwanga unaoakisiwa kutoka kwa jua. Katika mtizamo wa kinajimu Mwezi ni sayari inayotawala hisia na tabia angavu.
Alama yake ni namba 69 iliyo lala. Siku yake nzuri katika wiki ni Jumatatu. Namba ya bahati ni 2 na 7. Malaika wake anaitwa Gabriel au Jibril. Jini anayetawala Jumatatu anaitwa Murratul Abyadh au Abú nuuril abyadh au Phul.
Madini yao ni Fedha (Silver). Kito (Jiwe) ni Moonstone, Lulu (Pearl), Quartz, Diamond, Moonstone, Peacock Ore. Manukato yao ni Yasimini (Jasmine) na Msandali (Sandalwood).
Rangi zao ni Nyeupe, Bluu, Hudhurungi (Puce) na rangi ya Fedha (Silver). Wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi zozote ambazo siyo nzito au zenye uwiano na rangi nyeupe.
Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni Nyeusi (Black) na Bluu iliyoiva (Indigo). Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Machungwa na Dhahabu.
MAMBO MUHIMU
Ubora unaohitajika kusawazisha mambo yao ni kujirekebisha na tabia ya kusikitika na kunung’unika. Ubora wa nyota hii ni Uongozi.
Maadili yao ni Kung’ang’ania, kuwa na uwezo mkubwa wa kihisia na kupenda malezi. Matakwa yao ni Maisha ya kifamilia pamoja na nyumba yenye amani na maelewano.
USHIRIKIANE NA NANI?
Tabia za kujiepusha nazo ni kupunguza hisia kali na kunung’unika pasipo na haja.
Nyota za watu anaelewana nao: Nge na Samaki. Nyota ambazo haelewani nazo: Punda, Mizani na Mbuzi. Nyota inayomsaidia kikazi: Punda. Nyota inayomsaidia kihisia: Mizani. Nyota inayomsaidia kipesa: Simba. Nyota inayomsaidia katika ubunifu: Nge. Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano: Mbuzi. Nyota bora ya kujifurahisha: Nge. Nyota zinazomsadia katika mambo ya kidini na kiroho: Mapacha na Samaki.
KIPAJI CHA KAA
Kaa wana kipaji cha hisia ya kugundua mambo yanayotendeka ikiwa ni pamoja na kubashiri mambo, kumwelewa mtu kwa undani na kujua jambo ambalo mtu anataka kulifanya au jambo litakalotendeka hasa kwenye watu wengi. (Sensitive)
TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI
Kaa ni watu wenye tabia ya hisia nzito, wapole na wenye huruma. Ni wenye dhamira ya ulezi na kuhurumia watu wengine, hiyo inaonekana waziwazi katika nyumba zao na familia zao.
Ni watu wenye “gubu”, wakali, wenye kujishughulisha na wanajiamini. Ni wenye msimamo na wanaweza kuwa wivu sana na kudhibiti wapenzi wao.
Hisia ni muhimu sana katika mapenzi kwa Kaa. Ni watu wanaopenda kujilinda na wanaogopa kuumizwa. Wanapenda kuwa karibu na wapenzi wao na kuonyesha huba kubwa. Kwao hakuna mapenzi ya nusu nusu.
Kaa bila mpenzi hujihisi hawajatimiza lengo lao. Ni waaminifu na wanategemea uaminifu sawa. Ni wagumu kuachana na wapenzi na mara nyingi wako radhi waumie kuliko kuachana na anayempenda.
KAZI NA BIASHARA ZA KAA
Wanatakiwa wafanye kazi za Utabibu kama Madaktari au Wauguzi, kazi za baharini kama mabaharia, kazi za chakula kama hoteli na migahawa, kazi za kuhudumia watoto, kazi za benki, meneja utumishi au kazi za kuandika.
MAVAZI NA MITINDO
Mavazi yao yawe ya kupwaya pwaya. Magauni yawe ya kuning’inia, nguo ziwe za kubadilika. Mavazi yawe ya rangi ya Fedha na ya Bahari. Vitambaa viwe laini na vyenye kutiririka. Nguo za kike ziwe na marinda na blauzi laini.
MAGONJWA YA KAA
Nyota hii inatawala njia kuu ya chakula kuelekea tumboni, mbavu, mfupa wa kidari, tumbo la uzazi, utumbo mdogo na utumbo. Inatawala bandama na matiti.
Maradhi yao makubwa ni gesi, vidonda vya tumbo, kiungulia au matatizo ya mwili kuwa mnene.
VYAKULA, NCHI NA MIJI YA KAA
Wapende kula mapeas, kaa au vyakula vya baharini, kabichi na saladi. Wapende kutembelea au kuishi katika New York (Marekani), Venice (Ugiriki), New Zealand na Scotland.
MADINI, VITO NA MAFUSHO
Madini ya Kaa ni Fedha. Vito vyao ni Moonstone, Lulu, Pearl, n.k. Mafusho ni Ubani wa aina yeyote au maka. Unachoma Jumatatu kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.
FUNGUO
Funguo ya Kaa ni hisia: “nahisi”, basi wakihisi uwepo wa kitu hukipata.
Wasiliana nasi
Email: Rakimsspiritual@gmail.com
Email: mnajimu@unajimu.com
WhatsApp: +255 783 930 601
Rakims Spiritual