Jinsi ya kujua Jambo kabla halijatokea?

Rakims
0

 

 Jinsi ya kujua Jambo kabla halijatokea?


Yawezekana ulishawahi kukutana ama kuskia mtu akisema kuwa kawahi kuona jambo linalotokea ama litakalo tokea huenda ikawa ni wewe mwenyewe ama ni rafiki yako kiliwahi kumtokea hiki na ukichunguza baada ya muda jambo hilo likatokea.


Kujua hivyo ni moja kati ya nguvu za miujiza ambazo kila mtu anayo kutegemea na ya kwake ipo katika mtizamo upi, 

Hivyo nifuatilie katika video hii nitakuchambulia mwanzo hadi mwisho kuhusiana na nguvu hii ambayo ni yenye kupendwa na watu wengi na wewe ujue ya kwako imeegemea upande gani?


Kwa kuanza Nguvu hii ni nini ni ipo ya aina ngapi?


Nguvu ya kuona jambo kabla halijatokea imegawanyika katika makundi yafuatayo:


  • Prophecy yaani kipawa cha kinabii
  • Precognition yaani kipawa cha kuotea ndotoni
  • De javu kipawa cha kuhisi kinachofuata katika kutokea
  • Second sight Kipawa cha kuotea kinachotokea
  • Clair Audience kipawa cha kusikia yatakayo tokea
Well, ikiwa umeshatizama video zilizopita kuhusiana na nguvu za miujiza katika channel hii basi kuna maelezo ambayo yatakuwa teyari umeyafahamu. 

Lakini hapa tutaingia ndani zaidi katika kuchimba nguvu hizi na kila mtu anaweza kujua ni ipi kati ya nguvu hizi yeye anayo; 

Kisha baada ya hapo tutakuja kuangalia jinsi ya kufungua kila moja ikiwa tu una dalili zake.


1# Tukianza na Prophecy: Nguvu ya kinabii


Sote tunatambua kwamba Nguvu ya kinabii mwenye nayo ni Nabii. Hivyo isifike sehemu ukachanganya nguvu hizi na ukapata giza la kulaghaiwa na wenye kujinadi kuwa wanazo. 

Nguvu zote hizi huweza kuwa na hali sawa lakini Zingine zina madhaifu tofauti na nguvu hii ya kwanza ambayo ni Prophecy.

Unabii
Ni moja kati ya nguvu za Miujiza ambazo mwenye nazo huaminika katika Imani zote kuwa anakuwa kapenda na Mwenyezi Mungu.

Ambapo unabii inakuwa ni nguvu inayomuwezesha mtu kufikisha neno na kutoa kwa mifano.
Na kuweza kuzungumzia yajayo kwa uzani ambao ni mzito na hauna shaka ndani yake.

Hivyo kuhusu unabii hatuta zungumzia sana katika video hii kwa maana Mlango wa manabii ulishaisha na ni Imani ya dini zote Mbili ambao ni wafuatiliaji wangu wakubwa katika Channel hii...

Hapa hapa mtu anaweza kuuliza? 
Kwa hivyo hawa manabii wa sasa baada ya Yesu mwana wa Maria na Mtume Muhammad Swalah Allahu Aleyhi wasalaam.

Ni manabii wa nani?
Well kwa Imani ya Waislamu hao ni manabii wa nafsi zao wenyewe.

Lakini kwa Imani ya Wakristo pia hao ni Manabii waliotajwa na Yesu kwamba patakuwapo manabii wa Uongo.

Mkazo wa Imani ya kila mmoja kuhusu Unabii utajadiriwa kwenye Comment. 

Lakini hapa tuangalie Nguvu ya kinabii na kuhusishwa kujua litakalo tokea.
Mifano yake mingi ipo katika Mitume waliopitwa na baadhi ya watu walipopewa maarifa wakajuzwa yajayo 

mfano;
  • Adam baba wa wote kuomba msamaha. 
  • Al-Khidir moja kati ya marafiki wa Mungu aliyeua mtoto mdogo (mbele ya Nabii Musa)
  • Nabii Suleiman ( Song of Solomon)
  • Yesu katika safari za mafunzo yake mfano kujua mbinu za waizrael
  • Muhammad S.A.W katika safari za mafunzo yake mfano end of days
Wote hawa walijuzwa kupitia Mwenyezi Mungu.

Hivyo tunapowaita wengi wao ni manabii wa Uongo sio kwa ubaya isipokuwa kwa hekima ya Imani na Maarifa katika dini zote.

Al Khidir na wengineo tutakuja kuwaona kwenye playlist ya Wajue

Ingawa tunapokuja kwenye nguvu zingine za Miujiza ambazo Mtu yoyote anaweza kuwa nazo na hii ni kutegemea na yeye kuzifungua baada ya kuzijua basi tutaanza na Precognition

2# Precognition

Tunapozungumzia nguvu hii moja kwa moja tunakuwa tunazungumzia nguvu ya miujiza inayomfanya mtu kuona jambo lijalo katika ndoto zake.
Wengine hutambua kama future dreams yaani ndoto za yajayo baadae kwa kupitia ndoto au kwa kupitia mgando wa akili yake kama ukiwa umezubaa mithili ya mtu aliye sinzia au kupata ganzi ya ubongo.

Uwezo huu na nguvu hii ya miujiza huwa nayo watu wengi hasa wengine huwatokea katika kutambua mambo yasiyoonekana kwa macho ya kawaida katika ndoto zao.

DALILI ZAKE:
Wengi hujikuta ni wenye kuota mawasiliano hasa yanayohusu roho ambayo mara nyingi huota mtu kukumbwa na jini kabla jini hajamkumba, Mtu kuota mtu anakufa na kweli ikawa hivyo, mtu kuota ndoa na kweli ikawa hivyo, mtu kuota anafanya tendo la ndoa na kweli ikawa hivyo, mtu kuota anarogwa na kweli ikawa hivyo...

Hivyo unapokuja kwenye precognition asilimia kubwa ni kuota mambo ya kiroho yanayokuja kutokea mbele na sio mambo ambayo ni ya Mwili wa nyama hii ni kwa upande wa Pricognition 

Nikiwa na maana ya kwamba mtu napoota ndoto yenye kuhusiana na tendo la karibu na roho ama tendo la karibu na kiroho na likatokea kweli basi huyo ana precognition

Mtu kuota tukio mwanzo hadi mwisho wake na ukakuta tukio hilo halina faida yoyote katika ulimwengu wa kimwili;

Mfano: 
Umeota upo sehemu umekaa kisha watu wanapita na watakusalimia kisha baada ya hapo mtoto anajikwaa kisha mama yake anaanguka na wewe unashtuka kisha kutoa pole halafu mama yake anakuangalia kwa jicho kali.

Ama anakuwa kajawa na hasira.

Kisha unasahau ndoto hiyo hadi wakati mwingine tukio hilo linatokea na katikati ya tukio unaanza kukumbuka kila hatua linavyokwenda na ukiangalia faida yake huoni basi hii moja kwa moja ni 
Precognition

Japo watu wengi hujaribu kuipamba mtandaoni na kujaribu kuwaambia watu waifungue na kuendelea kuexperience matokeo yake.

Ukweli ni kwamba unatakiwa ufahamu nguvu hii itakufaa sana katika maisha ya kiroho kuliko kimwili kwa maana hadi ikionyeshe lijalo lazima roho yako katika hilo linalokuja iwe katika state ya kuumizwa sana, au kufurahi sana, au kushtushwa sana.. 

Ndio utaona watu hawa wakiota ndoto hizi moyo unakuwa kama unatumbukia nyongo na kuona hazina maana ndoto hizo wala msaada wowote lakini trust me zina maana na msaada mkubwa sana, Subscrribe Channel hii mchanganuo wa kuifungua na faida zake na jinsi ya kutumia utakuja.

3# Dejavu


Dejavu ni aina nyingine ya maono ya jambo kabla halijatokea na hii maono  na kumbukumbu yake huanzia hapo hapo jambo hilo linapokuwa linaendelea kutokea.

Yaani umekaa huna hili wala lile unaona mmekutana na mtu anaanza kuongea unaanza kukumbuka hayo mazingira na hujawahi kuota wala kufika hapo kabla.

Unakuwa na hali ya kuhisi kujua kila kitu kinachoendelea kwa muda huo hahahaha wengi wao huwa wanashtuka na kujiinua wenyewe katika hali hiyo kutokana na mawazo Mengi ya kuanza kujiuliza hili eneo na haya matukio mbona kama nimewahi kufika na kufanya hicho kabla?

Hapo hapo anakuwa kashakata mawasiliano na mtiririko wa yanayoendelea baada ya hapo kwa maana yeye teyari anakuwa kashaanza kuelekeza subconscious mind yake upande mwingine wa kulala hii ni sawa na;-

Umeamka kutoka usingizini kisha unalazimisha kurudi kulala Inashauriwa the moment unapata dejavu basi jitahidi kuichukulia kawaida kama ulikuwa unaongea endelea kuongea na kama ulikuwa unafanya kitu kifuate vile vile utapiga hatua ya pili ya Dejavu..

Japo niwatahadharishe hatua hii ya pili inatisha na kuogopesha maana utakuwa ni sawa na mtu aliyeingia state ya meditation bila matarajio . Unahisi kila kitu unaskia kila kitu unapata Bilocation hapo hapo,

Unatapa Clair Seeing hapo hapo na unapata clair Audience ambayo wengi hapo hapo huanguka chini.  kwa maana ni sawa na mtu aliyeingia state ya meditation 10 times than a normal person.

A human brain for example 

2.5 million gigabytes

Wana sayansi wa kimarekani wanathibitisha kuwa ubongo wa mwanadamu una uwezo wa kubeba mafaili hayo katika kumbukumbu yake na hii ni 1 side of a brain ambayo ni Conscious mind vipi kuhusu subconscious mind?

Hawajua kwa maana still bado hawajajua kwa wale ambao hawana idea kuhusu Conscious mind and Subconscious hii ni sawa na kusema matendo ya hiari na matendo yasiyokuwa ya hiari mathani kusaga chakula tumboni ni matendo yasio ya hiari na vinginevyo....


Tusitoke nje ya mada hiyo ni kwa videos zijazo. hivyo unapozungumzia kujua jambo kabla halijatokea na Dejavu pia inahusishwa lakini kujua jambo kabla halijatokea sio De-javu kama wengi wanavyodhani

Kujua jambo kabla halijatokea source yake ndio inajulisha jambo hili.


4: Second sight   

Niliwahi kuzungumzia nyuma kuhusiana na Second sight kwamba ni machale ama Uwezo wa kuona jambo lijalo kwa mfumo wa maono yaani uwezo wa mtu kuona habari, kwa njia ya maono, juu ya hafla za baadaye kabla ya kutokea(utambuzi) au kuhisi uwepo wa mtu au tukio dakika chache kabla halijatokea.

Hii wengi huwatokea kama bahati nasibu lakini ni aina moja kati ya nguvu za miujiza ambayo inaweza kufanya mtu akaona jambo lijalo. 

Wacheza kamari wakubwa sana huwa na nguvu hii hata katika video ya jicho la tatu nimeielezea.

5. Clair Audience

Hii nimekwisha elezea katika video zilizopita kwenye playlist ya nguvu za Miujiza lakini kuhusishwa kwake na kumfanya mtu aweze kujua yajayo ni kupitia kuambiwa na sauti za roho takatifu ama malaika kwa muda huo anaofanya mambo au jambo lake kisha kuanza kulisema au kuamua kuhama eneo hilo hasa kama ni jambo la hatari.

Yaani mtu akikaa anaskia sauti inamwambia ondoka hapo ama fanya hichi either kwa ukali ama kwa upole japo na mashetani huweza kufanya hivyo hivyo kuwa makini

Ikiwa bado hujaijua hii basi unaweza kuangalia katika video hii upande wa kushoto.

Mpaka wakati Mwingine........

Wasiliana nasi

Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia email lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.

Unaweza kutupata kwa kupitia Email, nambari za simu,kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,

Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.

Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na rakimsspiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.

Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa members pekee;

Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia

Wasiliana nasi kupitia:-


Rakimsspiritual@gmail.com

au

mnajimu@unajimu.com


WhatsApp number


+255 783 930 601


Rakims

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !