Nyota ya Ndoo - Aquarius

Rakims
0

NYOTA YA NDOO (AQUARIUS)

Nyota ya ndoo

Hii ni nyota ya kumi na moja katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 20 Januari na Februari 18 au wenye majina yalio anza na herufi K au W au G au S.

Asili yao ni Upepo.Sayari yao ni Uranus. Siku yao ya bahati ni Jumamosi. Namba yao ya bahati ni 8

Malaika wake anaitwa Cassiel au Kafyaeel, na Jini anayetawala Jumamosi anaitwa, Abuu Nuhu au Aratron.

Rangi zao ni Bluu, Kijivu na Samawi ya Bluu (Ultramarine blue). Wenye nyota ya Ndoo wanatakiwa wapake nyumba zao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi zilizotulia kama Bluu au Kijivu.

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Dhahabu na Machungwa.
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Aqua.
Kito (Jiwe) ni Lulu Nyeusi, Obsidian, Opali (Opal) na Johari (Sapphire).
Madini yao ni Risasi (Lead).
Manukato yao ni yale yatokanayo na Mgadenia (Gardenia) na Azalea.
MAMBO MUHIMU:-

Sifa ya nyota hii ni Uimara na Kutoyumba.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa Wachangamfu na Wenye hisia.

Maadili yao ni Uwezo mkubwa wa Kiakili, Uwezo wa Kuwasiliana, na Kuelewa mambo ya muhimu, Kupenda mambo Mapya.

Matakwa yao ni Kujua na Kuleta mambo mapya.
Tabia za kujiepusha nazo ni Kutojali, kutoshawishika au kutobadilika, kuwa na mawazo yasiyobadilika.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Mapacha na Mizani.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Ng’ombe, Simba na Nge.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Nge.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Ng’ombe.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Samaki.

Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mapacha.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Simba.

Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mapacha.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Mizani na Mbuzi.

Siku yake nzuri katika wiki ni siku ya Jumamosi.

KIPAJI CHA NDOO:

Ndoo wana kipaji cha kutoa tafsiri sahihi ya jambo lolote linalotokea wakati wowote, Sudden Revelation.

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Ndoo ni watu wachangamfu, wavumbuzi na wenye akili za kubuni jambo au kitu. Ni watu ambao wenye furaha wakati wote lakini inakuwa vigumu wakati mwingine kuwa karibu nao. Ni waaminifu na wakweli na wako tayari wakati wowote kutoa msaada unaohitajika.

Kwa upande mwingine ni watu ambao hawatabiriki hasa wanapokasirika, wanaweza kuwa wakaidi, wenye kushikilia jambo hata likiwa baya, ni wapotovu wa nidhamu na waasi.

Ni watu ambao hawajali Dunia inasema nini au inafikiria nini, wakati mwingine hukataa shughuli za kijamii na kujihusisha katika mambo yasiyo na maana yeyote.
Kwa ujumla ni watu wenye Roho nzuri ya kibinaadamu wanapenda kutoa msaada pamoja na kwamba wakati mwingine wanakuwa siyo dhahiri.

Ndoo ni watu wanaopenda uhuru na hawawezi kabisa kukubali kudhibitwa katika mapenzi, mawazo yao na miono yao inaweza kubadilika mara moja na kuwa wakaidi na wasumbufu. Pamoja na kwamba ni waaminifu na wanatoa msaada mkubwa kwa wapenzi wao.

Wako tayari kutulia katika mapenzi iwapo watahakikishiwa uhuru wao na haki ya kutoingiliwa katika mambo binafsi. Ni watu ambao hawapendi kuonyesha hisia zao halisi na wanachukua muda mrefu kuingia kikamilifu katika uhusiano wa kimapenzi.

Mara nyingi inakuwa vigumu kwao kuwaamini wapenzi wao lakini wakisha waamini wanakuwa waaminifu.
Ni watu ambao husema mambo bila kuficha na mara nyingi hawaeleweki kwa wapenzi wao.

Katika ngono, kwa sababu ya kupenda uhuru huwa wanapenda kufanya mambo wanavyotaka wao na hawakubali kuingiliwa.
Wakati mwingine hushindwa kuelewa hisia za wapenzi wao jambo ambalo linawafanya wapenzi wao washindwe kuwaelewa.

KAZI NA BIASHARA ZA NDOO:
Ndoo ni watu wenye akili nyingi na wenye malengo maalum katika shughuli fulani. Ni wawekezaji asili na wana uwezo wa kuwabadilisha watu tabia zao kutoka mbaya kuwa nzuri.

Kwa uhakika mawazo yao saa zote yanafanya kazi. Ni watu ambao muda wote wanafikiri njia mpya na za uhakika za kutekeleza wajibu wao na kikazi.

Kazi zao wanazifanya kwa upole na uhakika, pamoja na kwamba wanafanya kazi kwa bidii mara nyingi huwa wanaonekana hawajafanya kitu au sifa huenda kwa watu wengine.

Watu wa Ndoo ni wenye mawazo ya ubunifu na wenye kugundua njia mpya na zenye uhakika katika kazi.
Kazi zinazowafaa ni za uhandisi wa umeme, kompyuta, utafiti wa Sayansi, utabiri, huduma za jamii na utafiti wa mambo ya kale.

MAVAZI NA MITINDO:
Ndoo wanatakiwa wavae nguo za mitindo, zilizoshonwa kwa ustadi. Nguo hizo ziwe za rangi ya Kijivu, au Kijani iliyoiva au hudhurungi nzito. Kitambaa kiwe cha kitani (Linen) au cha ngozi. Nguo ziwe ni suti na ziambatane na saa za mikono.

MAGONJWA YA NDOO:
Nyota hii inatawala kifundo na ugoko. Wenye nyota hii wana mawazo mapana ya kufanya mabadiliko ya Dunia na hii inawasababisha wajisahau hasa katika afya zao na mara kwa mara hupata matatizo ya kuugua.

Kutokana na ubishi wao mara nyingi wanakuwa wabishi kupokea ushauri kuhusiana na hali zao za kiafya.
Matatizo yao makubwa yanasababishwa na kuchoka kwa misuli kutokana na kazi nyingi, kwa kawaida ni wagonjwa wabishi wasiopenda ushauri.

Wanapofanya mazoezi wanashaurwa wasiwe na hasira kwani hiyo inawafanya wajiumize au wapate ajali ndogo ndogo hasa sehemu za miguu, ugoko, vifundo na uvimbe katika sehemu hizo.
Vile vile matatizo yao mengine ya kiafya ni mzunguko wa damu na mishipa ya miguu.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA NDOO:
Ndoo wanashauriwa wepende kula vyakula au Matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota zao, vyakula vya nazi na nyama aina zote. Vile vile wapendelee kula Viazi Vitamu na Samaki Gamba.

Ili kupata mafaniko ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota zao. Nchi hizo ni Sweden na Zimbabwe na Miji ni Humburg (Ujerumani) na Leningrad (Urusi).

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Ndoo ni Uranium ikiwa ngumu kupata tumia Lead (risasi). Vito vyao vya kuvaa katika pete ni amethyst au Onyx.
Mafusho ya Ndoo ni Miatun- saila. unachoma siku ya Jumamosi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

FUNGUO:


Funguo ya wenye nyota ya ndoo huwa ni "najua" basi yeye akijifanya mjuaji wa mambo huwa anafanikiwa kwa mengi

Wasiliana nasi

Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia email lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.

Unaweza kutupata kwa kupitia Email, vile vile kwa namba za simu, kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,

Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.

Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na RakimsSpiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.

Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa Members pekee;

Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia:-


Rakimsspiritual@gmail.com


au


mnajimu@unajimu.com


WhatsApp number


+255 783 930 601


Rakims

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !