Jinsi ya kujua kama nyota yako imeng'aa au imefifia?

Rakims
0

Nyota iliyosawa



Jinsi ya kujua nyota yako ipo juu au chini?


Ikiwa nyota  yako ipo juu zaidi au chini zote hizi sio nzuri kwa maana zina madhara na maafa ndio maana hata ukiona mwenzio kapandishwa nyota na kafanikiwa na wewe umepandishwa na hujafanikiwa basi fahamu kabisa kwamba nyota yako huenda toka mwanzo ilikuwa juu ulichofanya ni kuizidishia mzigo tu.

Hivyo kama nyota yako ipo chini unahitaji msaada haraka iwezekanavyo hata ikiwa juu pia ni majanga nyota inatakiwa kuwa balanced na hiyo ndio hekima ya mizani za nyota na watu wengi hawajui hilo isipokuwa wanahangaika tu kuwapandishia na kung'arishia watu nyota.

Rejea katika video zilizopita nilizozungumzia kuhusu nyota kama hufahamu nyota yako.

Ikiwa hufahamu nyota yako basi endelea kufuatilia video hii na utajua nyota yako ni ipi na kama imejaa au ipo chini.

 
Wengine mnachohitaji ni kushusha nyota ili ziweze kuwa balanced kwa maana kama umehangaika kusafisha nyota bila mafanikio basi fahamu ya kwamba nyota yako imezidi kipimo na unahangaika kuizidishia mzigo au ipo chini sana na unazidi kuiangamiza.

Nyota ya mtu haiwezi kuibiwa wala kuchukuliwa na mwingine kinachofanyika ni kuifunga kuichafua na kuiloga tu lakini ipo pale pale haiendi popote watu wengi huweka dhana za nyota kuibiwa na kuchukuliwa nyota ya laiti mtu angejua maana ya kuibiwa au kuchukuliwa nyota hata asingejiwazia huo ujinga.

Ama kuwaaminisha wengine,

Kwa hivyo pia sina maana kuwa nyota yako haiwezi kutumika na mtu mwingine inawezekana lakini bado sio sababu ya kuwa imechukuliwa.

Kuna nyota 12 katika mlolongo wa makundi nyota ambazo ni maarufu kama zodiac signs.
ambazo ni nyota zilizopo katika utawala wa jua ambazo kitaalamu huwa zinakusanywa na kuunganishwa katika kundi moja ambalo ni maada hili ni somo pana isipokuwa nitakurahisishia kwanza:

Maada hizo ni:

  • Moto
  • Upepo 
  • Maji
  • Udongo
lakini pia ambazo zikitawanywa tunapata nyota 12 ambazo ni makundi nyota hivyo zinakuwa 

Aries (fire)
Taurus (earth)
Gemini (air & earth)
Cancer (water)
Leo (fire)
Virgo (earth & fire)
Libra (air)
Scorpion (water & fire)
Sagittarius (Air & fire)
Capricorn (earth)
Aquarius (air)
Pisces (water & fire)


Nyota zote hizi zinaweza kuwa na maada moja au mbili hivyo usishangae kukuta una dalili ya maada mbili katika nyota yako.


TUKIANZA NA MOTO: Nyota ya moto ikiwa imejaa

Nyota za moto zikiwa zimejaa basi utamuona muhusika mara kwa mara hujichoma moto ama kujiumiza, anakuwa na hasira sana na kisirani na hana subira, vile vile anakuwa anakosa amani ambayo inapelekea kujihisi kama ana shinikizo la damu au presha, dalili za matatizo ya moyo, matatizo ya vidonda vya tumbo na kuwaka moto yaani kujihisi joto na kuchemka anakuwa anasikia amani akikaa uchi. 

Jinsi ya kutuliza:

Kama nyota yako ya moto imejaa basi ili kuweza kuibalance na kutuliza utatakiwa utumie vyakula ambavyo ni vya baridi na vyakula vyenye unyevunyevu na vizito, au vinavyoungua polepole ambavyo husaga nishati ama nguvu ya moto katika nyota yako. 

Kula
Nafaka, mboga za mizizi.

Kwepa sana

Spicy food and red meat yaani vyakula vya viungo na nyama nyekundu mfano pilau na mbuzi

Dawa zake
herbs like chamomile, lemon balm, skull cap and valerian. yaani zeri ya limao na miti fulani hivi kama inatoa maua utaipata supermarkets bei rahisi tu


Nyota ya moto ikiwa ipo chini

Ikiwa ipo chini basi kwako kutakuwa na ugumu wa kuchoma maradhi, na utasumbuka na maradhi ya choo kwa maana kama mnavyofahamu tumboni hukaa Solar plexus chakra kwa wale mnao nifuatilia kwenye chakra hii mtakuwa mmeelewa kwa hivyo 

Usagaji na ufyonzaji wa chakula utakuwa hautoshi na kukupelekea kujihisi una maradhi ya hospital ukipima unakuta kavu
Hivyo utatakiwa kula vyakula ambavyo ni vya moto, vyenye mwanga, vikavu na vyenye kunukia yaani ni sawa na kufanya kinyume na vyakula vya nyota hizi zikiwa zipo juu. 

Kula
lemon, yoghurt, bitter greens like kale, mustard (limau, mtindi, mboga chungu kama kale, haradali/Jira)..

Kwepa
dairy products, meat (Maziwa na nyama)

Dawa yake:
Dawa za kulainisha choo, kama cayenne, mustard, Cloves, cinnamon, garlic pia kitunguu swaum na ginge ama tangawizi. 


Nyota za maji zikizidi

Basi watu ambao nyota zao za maji zikizidi wanakuwa na uvivu wa kwenda haja yaani akipata choo kinakuwa kidogo sana, kupata choo anakuwa anapata isipokuwa ni kwa kidogo sana, ambapo anapata choo binafsi anakuwa anajishtukia kwamba sio cha kutosha, anakuwa ni mgumu sana kuelewa ukimwambia ama akijifunza kitu.

Wenye nyota hii ya maji ikiwa imezidi basi utamuona anakuwa na maradhi ya mafua ya mara kwa mara, uvimbe wa ndani au nje, Pamoja na fungus aina ya candida ambazo ni ngumu kupona kila akitibu zinarudi na haikai muda zinakuwa zinaleta umaji maji.

Nyota hii ikizidi pia utaona mtu anakuwa na matatizo ya uzito, na anashindwa kujizuia kupunguza ama kujikadiria chakula katika upande wa diet yeye kama yeye hadi apate msimamizi.

Matokeo mazuri huja pale ambapo atapandisha metaboliki rate, kwa kupunguza wingi wa unywaji wa vinywaji vya maji. kubadiri mfumo wa chakula, kufanya mazoezi na kula vyakula ambavyo ni vya moto, vikavu na vyepesi.


Kula
steamed vegetables, beans, fruits. yaani mboga za kuchemsha, maharage na matunda.

Usile au kwepa:
Vyakula vya mafuta, diary, vitu vitamu, vitu vichachu, mikate na chumvi punguza 

Remedy:
Dawa zake ni sage, mrehani, zaatar, vitunguu swaum, lugaka au lugola au alugula kitu kama hicho supermarket ukienda wanajua inaitwa parsley, uva ursi and juniper (mreteni au al 3ariil na matunda ya berries, Chaparral zote hupatikana super market katika maduka ya viungo


Nyota ya maji ikiwa chini

Nyota ya maji ikiwa chini basi muhanga utamkuta ni mtu asiyeweza kutoa sumu kutoka kwenye mwili na anakosa mafuta ya kulainisha mfumo wa mwili wake.

Anakuwa ana hali ya kupauka mwili na anakuwa na hali ya kuwa na kiu hasa wakati wa usiku unakuta anataka kunywa maji mengi ana lala usingizi wa tabu na mawenge. 

Anakuwa na hali sawa na mtu mwenye nyota ya upepo ikiwa imezidi wengine hudhani wana mapepo. vile vile huwa na nywele kavu na zenye kukatika katika na zinakosa uwezo wa kunyonya virutubisho, ikiwa ni pamoja na ngozi kung'aa.

Na wanakuwa ni wenye gubu na kutokutaka kucheka na watu.
Jisaidie kwa kuoga mara kwa mara, kunywa maji mengi, na uwe na urafiki na matikiti maji, matango, na usifunge kama sio lazima simaanishi mwezi wa ramadhani.

Usikae sana sehemu za joto ama kutembea juani.
na wala usikae sehemu ambapo ni mbali na miti panda mti pia karibu na wewe kwa matokeo mazuri


Kula
Ngano,wali,shairi,magugu maji au kwa maneno mengine (bange ya bahari) na vyakula vya maziwa ikiwa ni pamoja na sukari asilia.  

kwepa na Usile
Maharage, carrots, kabeji, avokado ya majani na figili. 

Dawa yake
Unachukua licorice au susu unachanganya na asali kisha unatia kwenye juicy ya matunda.
licorice hutumika kuweka ladha kwenye pipi au vinywaji na sigara pia.

Nyota za udongo zikizidi

Hizi nyota zikizidi pia huleta uzito zaidi kwenye mwili na kila jambo la mtu linakuwa gumu sana kufanikiwa. 

Nyota hizi zikizidi uwezo au ujazo husababisha manyoya kwenye mwili kurefuka zaidi huongeza uzito kwenye tissue na kufanya ngozi kuwa nyembamba ikiendana na uvimbe, kupungua kwa calcium mwilini na nyama za mwili zinakuwa ngumu au zimekaza.

Kula
fruit- salads, mboga za kuchemsha,sprouts unatia na viungo, juicy, supu na chai upendelee sana,

Kwepa
Vyakula vyote ambavyo ni vizito


Dawa zake

bitter tonics na vitu vichachu vichachu, viungo vikali sana kama tangawizi, pilipili manga na pilipili kichaa.


Nyota za udongo zikiwa chini

Nyota za udongo zikiwa chini zinahitaji unangalizi wa makini kwa maana watu wenye nyota hii ikiwa chini hawana silika na kile anacho kihitaji unaweza kukuta anakwambia mimi nasubiri kufa tu yaani ni watu waliokata tamaa. Wanahitaji waliokaribu nao kuwaliwaza na kuwapa ishara ya kujihisi wamelindwa nao.
Nao hupenda kulala kuliko nyota zingine na wakilala chini kwenye ardhi husikia raha. 


Kula
nyama, viazi ulaya, nafaka zisizosafishwa, mazao ya mizizi, maziwa, mboga zilizokaushwa, jibini, siagi, sukari na mafuta mafuta kama mkiwa wa kondoo na nyama za nundu.

Kwepa
Matunda na vyakula vibichi

Remedy

Susu ambayo nimesema ni licorice na Elm utaipata supermarket kama slippery elm au maduka ya madawa ya kiarabu kama zalak al dirdarah, vile vile magugu ya bahari na seaweed and minerals, Ginseng maarufu kama majani ya chai ya korea hufanana na binzari, astragalus ambayo husaidia mtu mwenye kisukari pia kushusha na ahashwaganda.

Kwa maelezo zaidi na matumizi ya dawa hizi fuatilia channel yetu ya youtube:

Bonyeza hapa


Nyota za upepo zikizidi

Nyota hizi zikizidi wenye nazo utaona wanakuwa na tabia za akili za kupindukia, yaani zisizotulia, nyeti na uchovu wa neva na huleta ishara za alama za upepo kama ngozi kavu, nywele zinabadirika rangi, kuumwa mafua, kukosa usingizi,  kupoteza kumbukumbu. 

Hupendezewa zaidi na madirisha yakiwa wazi popote alipo, na msisimko mdogo ili kuruhusu mfumo wa neva kujichaji wenyewe.


Kula
Mboga nyepesi za kuchemsha, karanga na kokoto yaani vile viandazi vigumu.

Kwepa
Vyakula visivyoiva vema, 
vyakula vichachu na matunda yake, mizizi na miwa.

Dawa yake
Sanamaki na habat sauda.


Nyota hizi zikiwa chini

Nyota hizi zikiwa chini basi utakuta wahusika wanakosa nguvu ya kupokea nuru kwenye miili yao hasa vile vile mwili unashindwa kufua na kutengeneza nguvu na kukusanya madini ya calcium na magnesia hata akila magnesium anakuwa na kiungulia kikali badala ya kupoza anakikoleza ikiwa ni pamoja na shida kwenye mfumo wa upumuaji.

Hii inatokana na wao kula sana vyakula ambavyo haviivi vizuri hasa nyama hivyo ni vitu vya wao kuepuka na pia juices za kuchanganya hasa shairi kwao sio nzuri sana japo utaona hospital hushauriwa kutumia hizo.

Kula

Pilipili, vitunguu swaumu, yoguart, kefir na Ginko

Remedy
dandelion root (mizizi ya dandelion au angostura chachu.

Wasiliana nasi

Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia email lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.

Unaweza kutupata kwa kupitia Email, nambari za simu au kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,

Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.

Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na rakimsspiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.

Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa members pekee; 

Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia


Email: Rakimsspiritual@gmail.com

WhatsApp:         +255 783 930 601

Rakims

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !