Nyota ya Mshale (Sagittarius)
Hii ni nyota ya tisa katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 November hadi 20 December kwa nyota za magharibi au 16 December hadi 14 January kwa nyota za mashariki au wenye majina yalioanza na herufi I au D au P au U.
Asili yao ni Moto. Siku yao ya Bahati ni Alkhamisi. Namba yao ya Bahati ni 5 au 7. Sayari yao ni Jupiter (Mushtara).
Malaika wake anaitwa Sachiel au Israfeel na Jini anayetawala Alhamisi anaitwa Shamhuurush ambaye ni Kadhi wa Majini au kwa jina lingine ni Bethor.
Rangi zao ni Bluu na Bluu iliyokolea. Wenye nyota hii wanatakiwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara rangi zenye kusisimua na uchangamfu na zinazoashiria hali ya kumkaribisha mgeni. Rangi hizo ni Nyekundu iliyochangamka (Warm Red), Zambarau (Purple) na Kahawia (Brown).
Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni Njano na Njano-machungwa. Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Nyeusi na Bluu iliyoiva.
Kito (Jiwe) ni Feruzi (Turquoise) na Kito chekundu (Carbuncle). Madini yao ni Bati. Manukato yao ni Yasmini (Jasmine) na Manemane (Myrrh).
MAMBO MUHIMU
Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye uwezo wa Kuongoza, Kuratibu, Kuandaa, Kupanga na Kusikiliza kwa makini.
Maadili yao: Ukweli, Kuona mbali, Ukarimu na Kusikiliza mawazo ya wengine japokuwa si lazima akubaliane nayo.
Matakwa yao: Kupanuka kimawazo.
Tabia za kujiepusha nazo: Kutegemea mambo kuwa mazuri siku zote, Kutia chumvi mambo na Kuzidisha ukarimu kwa kutegemea hela za watu wengine.
USHIRIKIANE NA NANI
Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Punda na Simba.
- Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Mapacha, Mashuke na Samaki.
- Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mashuke.
- Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Samaki.
- Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mbuzi.
- Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Punda.
- Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Mapacha.
- Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Punda.
- Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Simba na Nge.
KIPAJI CHA MSHALE
Mshale wana kipaji cha kutabiri na kujua mambo ambayo yatatokea mbele au muda utakaokuja, na mara nyingi wanalolisema huwa linatokea hata likiwa la kipuuzi (Prophetic).
TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI
Mshale ni wenye matumaini ya mafanikio kwa lolote wanalolitegemea. Wanapenda kuwa na uhuru wa kupenda na kuchagua na wanapenda watu wengine wawe kama wao. Hawapendi mambo nusunusu.
Ni watu walio wazi, wanaopenda kusoma na wakweli. Ukihitaji kuelewana nao, na wewe uwe mkweli. Ni watulivu, waaminifu na wanapenda uadilifu. Hawaoni taabu kusema jambo la kweli hata kama linaumiza.
Pamoja na kwamba wanapenda kuwa huru na kujiamulia mambo yao, wanapenda starehe na wanahisi furaha wanapokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Wanapenda sana kujihusisha na makundi lakini pia wanapenda kutumia muda na wapenzi wao. Katika mapenzi ni wachangamfu na wenye kupenda, ila tabia yao ya kutojali huwafanya wapenzi wao wajihisi kukosa ulinzi wa kimapenzi.
Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu. Mwanzoni huwa wagumu kujihusisha lakini wakishaingia wanajitoa kwa dhati. Wanaweza kupendelea kuwa na mapenzi ya muda mfupi au mabadiliko ya mara kwa mara kwa sababu wanaogopa mapenzi ya kudumu kuwanyima uhuru.
Ni watu wanaopenda ngono kwa muda mrefu na hisia zao ziko mbali. Inashauriwa wapenzi wao wawe wametulia na kushiba kabla ya tendo la ndoa ili kuepuka shida.
KAZI NA BIASHARA ZA MSHALE
Mshale ni waaminifu na wanaopenda mafanikio. Wako tayari kufanya kazi wakati wowote. Kwa sababu hii mara nyingi wanakutana na nafasi bora katika muda unaofaa. Ni wafanyakazi waaminifu na hawapendi kuwasimamia wengine.
Wakiwa ofisini hujenga mazingira ya urafiki na kuaminiana. Kazi zinazowafaa: usafiri, sheria (wakili au hakimu), uandishi, ualimu, dini (sheikh, padri, mchungaji), michezo, kazi za kijeshi na uuzaji.
MAVAZI NA MITINDO
Mshale wanatakiwa wavae nguo zenye mvuto na ucheshi, kama koti au blauzi zisizo rasmi, au nguo za kitamaduni zenye mapambo na nakshi nyingi. Rangi zinazofaa: Zambarau, Hudhurungi iliyochangamka na Bluu.
Vitambaa viwe vya sufu. Nguo ziambatane na mikanda na viatu vya buti. Wanawake wavae sketi.
MAGONJWA YA MSHALE
Nyota hii inatawala sehemu ya chini ya kiuno. Wenye nyota hii mara nyingi huugua kutokana na kutumia nguvu na akili kupita kiasi bila mapumziko. Wanathamini sana mizunguko kuliko kupumzika.
Tatizo jingine ni kupenda kula na kunywa kupita kiasi, jambo linalosababisha unene usiotakiwa. Ili kuepuka matatizo wanashauriwa kuwa na ratiba ya mapumziko.
Magonjwa yanayowapata: majereha, matatizo ya nyonga na mapaja, magonjwa ya ini, kupooza miguu na matatizo ya mishipa ya nyuma ya paja.
VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA MSHALE
Wenye nyota hii wanashauriwa kula nyama mwitu, kunazi za bluu, maboga na juisi ya mapera.
Ili kupata mafanikio ya kinyota wanashauriwa kuishi au kutembelea nchi na miji ifuatayo: USA na Spain; Budapest (Romania) na Cologne (Ujerumani).
MADINI, VITO NA MAFUSHO
Madini ya Mshale ni Bati. Vito vyao vya kuvaa ni Yakuti ya Njano au Lapis Lazuli.
MAFUSHO
Mafusho ya Mshale ni Udi Kafur. Unachomwa siku ya Alkhamisi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.
FUNGUO
Funguo ya nyota ya Mshale ni "Nalenga" — yeye akilenga kitu basi huwa hakosi hata akikipania.
Wasiliana nasi
Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya wiki kupitia:
Email: Rakimsspiritual@gmail.com
WhatsApp: +255 783 930 601
Rakims Spiritual