
Nyota ya Mashuke (Virgo)
Hii ni nyota ya sita kwenye mlolongo wa nyota 12 na ni ya watu waliozaliwa kati ya Tarehe 22 Agosti hadi 22 Septemba kwa njia za magharibi na 16 Sept hadi 15 October kwa njia za Mashariki au wenye majina yalio anza na herufi F au P au T au R.
Asili yao ni Udongo. Siku yake nzuri katika wiki ni Jumatano. Namba yao ya bahati ni 5. Sayari yao ni Mercury (Attwarid).
Malaika wake anaitwa Raphael au Mikyaail. Jini anayetawala siku ya Jumatano anaitwa Barkaan au Ophiel.
Rangi zao ni Rangi ya udongo, Njano na Rangi ya machungwa. Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi Nyeupe au rangi ambazo siyo nzito au zenye kuonekana sana.
Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi Bluu. Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Rangi ya Kijani kibichi.
Kito (Jiwe) ni Cuprite, Diamond, Sugilite, Moss Agate, Quartz, Peridot. Madini yao ni Quicksilver (Zebaki). Manukato yao ni ya Mrujuani (Lavender) na Lilaki (Lilac).
MAMBO MUHIMU
Sifa ya Nyota hii ni wanakuwa na uwezo wa kubadilika badilika.
Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye uwezo kuangalia mambo kwa mtizamo mkubwa zaidi.
Maadili yao ni Uchambuzi, Wepesi wa Akili, Uwezo wa kuwa makini na Uwezo wa Kuponya.
Matakwa yao ni kuwa wenye uwezo wa Kutumika.
Tabia za kujiepusha nazo ni ukosoaji usiokuwa na malengo mazuri.
USHIRIKIANE NA NANI?
Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Ng’ombe na Mbuzi.
Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Mapacha, Mshale na Samaki.
Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mapacha.
Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Mshale.
Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mizani.
Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mbuzi.
Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Samaki.
Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mbuzi.
Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Simba.
KIPAJI CHA MASHUKE
Mashuke wana kipaji cha kuhisi, kufikiri, kutambua tatizo au ugonjwa au kupata picha ya wazi akilini ya kutambua jambo lolote. Vilevile wana uwezo wa kuponya na wana uwezo wa kusoma michoro yeyote.
TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI
Mashuke ni watu ambao wanaopenda kusoma. Wana akili nzuri ambayo inatumika zaidi katika kupambanua njia ya asili ya mpangilio wa mambo. Kwa ujumla ni watu ambao wanapenda kufuata kanuni na kufanya mambo kwa usahihi kabisa. Ni waangalifu sana hasa katika mambo madogo madogo na wanapenda kushutumu hasa mambo yanapokwenda vibaya.
Katika Mapenzi ni watu wenye aibu kwa undani lakini wanajiamini, wanapokuwa katika mapenzi hunawiri. Ni watu ambao inawawia vigumu kuonyesha penzi lao. Wanapotafuta mpenzi wanaweza wakakupumbaza na maneno matamu na raha zisizo na kifani.
Mara wakishapata mpenzi wa kweli wanakuwa waaminifu sana na watafanya kila njia kuhakikisha mapenzi yanakuwa hai na yenye kupendeza. Hata hivyo wanaweza kuwa wasumbufu, wenye kulalamika na wenye mtizamo wa makosa ya mpenzi wake.
KAZI NA BIASHARA ZA MASHUKE
Mashuke ni tegemezi, wenye bidii ya kazi na tabia ya kufanya kazi bila ya kuchoka. Wanapenda sana kazi zenye mpangilio na ambazo kila kitu kiko katika mpangilio maalum.
Kazi zao ni zile zinazohusiana na uchapishaji, utangazaji, afya, udaktari, kazi za unesi, kazi za uongozi, elimu na kufundisha, biashara yoyote au kazi za ukatibu muhtasi.
MAVAZI NA MITINDO
Mashuke wanatakiwa kuvaa Nguo zenye Mitindo ya kisanii, nguo ziwe Nyepesi na zilizonyooka. Ziwe za Rangi ya Njano na Nyeupe. Kitambaa kiwe kama hariri, chepesi na chenye kumeremeta. Wake kwa waume wapendelee kuvaa Suti na ikiwezekana wasikose kuvaa Gloves.
MAGONJWA YA MASHUKE
Nyota hii inatawala utumbo, sehemu ya uvunguni mwa utumbo na neva zote zilizo chini ya kitovu. Kutokana na asili hiyo wenye nyota hii huwa wanapata matatizo ya ugonjwa wa tumbo au tumbo la uzazi au matatizo ya kizazi.
VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA MASHUKE
Mashuke wanashauriwa wapende kula kuku, rasiberi, karoti na uduvi. Ili kupata mafanikio ya kinyota wanashauriwa waishi au watembelee nchi/miji: Austria, Norway, Jerusalem na Paris.
MADINI, VITO NA MAFUSHO
Madini ya Mashuke ni Quicksilver (Mercury). Vito vyao vya kuvaa katika pete ni Green Sapphire. Mafusho ya Mashuke ni Kashuu Muhlib (kachiri). Unachoma Jumatano kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.
FUNGUO
Funguo ya Mashuke ni "Nachambua". Akisema anachambua au akilichambua sana akilini basi humfika.
Wasiliana nasi
Email: Rakimsspiritual@gmail.com
Email ya pili: mnajimu@unajimu.com
WhatsApp: +255 783 930 601
Rakims