Nyota ya Punda

Rakims
0

NYOTA YA PUNDA ( Kondoo )

ARIES


Hii ni Nyota ya kwanza katika mlolongo wa Nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 March hadi 20 April au wenye majina yalioanza na herufi A au M na DH mfano Dhul Kifli.

Namba yao ya bahati ni 1,9,13 na 25.

Asili yao ni Moto,

nayo ni nyota dume.

(dume ikiwa na maana ya chanya/sio jinsia za wenye nyota)

Usawa wake ni Imara (UFALME)

Ni nyota ya utendaji,yenye nguvu,inafaa na yenye msukumo na nyota yenye matumaini,iliyowazi katika mabadiriko na hali mpya.

SAYARI YAO

ni Mars (Mariikh) Marikh kwa historia za kale ni kuwa ni sayari ya Kiumbe wa vita,vurugu,uovu na ubaya.
katika elimu ya nyota hii husimama kama sayari ya hamu/shauku na upinzani huleta hisia za ajali na humiliki moto na Hatari.

ALAMA YAKE

Kondoo dume: mkali,mkorofi,kingono,mwenye uwezo wa kupanda chart juu zaidi.

TALASIMU YAKE

Picha inayo wakilisha pembe na pua ndefu ya kondoo dume. na pia inakuwa na muonekano wa nyusi na pua ya uso wa mwanadamu na kichwa ni sehemu kuu ambayo sheria ya Punda inatawala yaani halmashauri ya kichwa).
 
maana nyingine talasimu yake ni mfano wa mwezi uliokatwa katikati na kuwa vipande viwili vilivyo karibiana ambayo inaonyesha ishara yake ya utawala na uongozi wa nyota hii.

NENO LAKE TAWALA

MIMI hili ndilo neno tawala la Punda yaani umimi kwanza Maarifa makuu kabisa ya punda ni ujasiri
Mara nyingi ni mtu mwenye ubinafsi wake haijarishi ataficha na kukataa kiasi gani. Ni mbinafsi.

NYOTA INAYOENDANA ZAIDI

Mizani au Libra
Punda ni nyota ya umimi kwanza watu wenye nyota hii wanatabia ya ubinafsi zaidi na wanaweza kuwa ni watu ambao wenye kuangalia maslahi yao wao tu.

Ambapo Mizani ni kinyume cha Punda. Vile vile ni nyota yenye kuweza kuing'arisha na ushirikiano na wenye nyota ya mizani. 
Wao hujihisi hawajakamilika bila ya mwenza au mpenzi. Nyota hizi mbili zikiungana basi huendana vizuri zaidi. Basi huwa na nguvu maradufu, na hasa wakiungana kimapenzi basi hung'ara zaidi.

SEHEMU YA MWILI UNAYOTAWALIWA NA PUNDA

Kichwa: Watu wa punda hukabiliwa na maumivu ya kichwa, na wanakabiliwa na majeraha madogo kuzunguka kichwa na uso wengi utawakuta na alama usoni

SIKU YAKE NZURI

Siku nzuri katika wiki kwa wenye nyota hii ni Jumanne

MALAIKA

Malaika anayetawala au kuangalia nyota na sayari yake anaitwa Izrael, ambaye ni malaika mtoa roho za viumbe,

JINI WA NYOTA HII

Jini wa nyota na sayari hii anaitwa Abuu Muhriz al Hammar au Mwenye mavazi mekundu.

SHETANI WA NYOTA HII

Phaleg kiswahili wanamtambua kama SUBIYANI pia ni mwenye mavazi mekundu.

MANUKATO

Manukato au Perfume yao ni Marashi ya Asali (Honeysuckle)

KIPAJI CHA PUNDA

Wenye nyota hii wana kipaji cha Hisia, ni rahisi kwao kutafsiri jambo lolote, wanaweza kwa urahisi kutafsiri ndoto, vilevile wana kipaji cha kusikia sauti ndani ya kichwa kuhisi jambo litakalotokea na ikawa kweli.

Ikiwa watafanya Taamuli (Meditation) kwa dakika ishirini wakati wa usiku au kitu cha kwanza wanapoamka asubuhi, akili na miili yao itatulia na watapata ufunuo wa mambo mengi sana.

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI

Punda ni wakali na wachangamfu, wenye hisia na wanaoweza kujieleza wakiwa na hali ya kufanya chochote. “SASA HIVI” hayo ndio mambo wanayotaka kusikia.

Ni watu wasiokuwa na subira, kila kitu kinafanyika kwa msukumo na haraka haraka. Ni viongozi majasiri ambao hawaoni karaha kuchukua majukumu, wakati wote wanajiona kwamba “Wanajua sana”.

Kimapenzi Punda ni watu wenye mapenzi motomoto, tatizo lao kubwa hawapendi kusikiliza ushauri wa kimapenzi, na hawakubaliani na mambo nusu nusu. 

Ni watu wenye kutegemea mazuri wakati wote na hawakubali kushindwa. Hupenda kukimbilia katika mapenzi bila kufikiri, wanapohisi wamepata mpenzi wa kweli. 

Ni wepesi kuvutwa katika mapenzi na wenye miamko ya ghafla au misukumo ya kiwazimu ambayo wakati mwingine inawafanya waonekane wapumbavu.

KAZI NA BIASHARA ZA PUNDA 

Wote wake kwa waume waliozaliwa katika nyota hii wana kipaji cha asili cha uongozi na wasiwasi wa kushindwa katika utekelezaji.

Kazi zinazowafaa ni Jeshi, Kazi za Uokoaji, Michezo, Uuzaji, Upasuaji, Kufundisha (Ualimu), Masuala ya Fedha.

Biashara za kubadili fedha,Biasharaza kuuza vifaa vya michezo, biashara za vifaa vya shule au maduka ya madawa.

MAVAZI NA MITINDO

Mavazi yao yanatakiwa yawe ya mitindo mikali na tofauti, yenye kuchangamsha na Kusisimua ya rangi nyekundu.
Vitambaa vyao viwe vya sufu (wool), Fulana, na vitambaa vilivyo na kishiwa kwa nyuzi za rangi ya chuma. Wasikose kuvaa kofia, wanawake wapendelee sana kuvaa na Suruali

Rangi yao ya Bahati ni Nyekundu na maalumu zaidi kwa maana huwakilisha moto ambao ni asili ya Punda,

Rangi zinazowafaa kwenye Nyumba au Vyumba vyao ni rangi nyekundu (Scarlet).

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za kijani na kijani kibichi. Rangi inayowapa uwezo wa kifedha ni rangi ya Kijani

MAGONJWA YA PUNDA

Nyota hii inatawala kichwa, Ubongo, Macho, Mifupa ya uso na fuvu la kichwa. Magonjwa yanayohusiana na nyota hii ni kuumwa na Kichwa, Kuzimia, Homa ya ubongo, maradhi ya kupata ajali ndogo ndogo za uso na kichwa Maradhi ya chunusi na magonjwa ya mishipa ya kichwa.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA PUNDA

Punda vyakula vyao vikuu ambavyo vitawaletea bahati ni Mananasi,Viungo vya pilipili, Vitunguu na nyama ya mbuzi.

Nchi ambazo wanaweza kupata mafanikio ni England, Germany, Poland na Switzerland na miji yao ni Florence, Marseilles,Verona Liverpool na New Orleans

MAUA

maua ya nyota hii ni Geranium,honeysuckle na sweet pie

MITI YAO

Miti yote ile yenye miba basi inaendana na nyota hii

MADINI

Madini yao ni Chuma,

VITO

Vito au Mawe ya bahati na miujiza ni Almasi
Almasi: Humvutia upendo, mafanikio ya kifedha, na huleta bahati katika miradi mpya. Almasi kwake ni bahati kubwa sana akivaa na ikiandaliwa kwa kufuata masharti maana ukikosea huvuta upande mbaya wa nyota hii unaweza kuwasiliana nasi kwa maelekezo zaidi.

Hii hasa kwa watu wa Punda. Kidole cha kuvaa ni kidole cha pete(ring finger) kushoto.
Hii kwa sababu huvuta mapenzi mafanikio ya kimaisha, bahati za kupitiliza hili jiwe huwapa bahati sana wenye nyota ya punda. 

linapovaliwa upande wa kushoto, mawe mengineyo ni Ruby, Hematite, Aventurine, Bloodstone, Carnelian, Citrine, Diamond, Lapis Lazuli, Mexican Lace Agate na Quartz

WANYAMA

wanyama wa nyota hii ni kondoo hasa madume ikiwa mwenye nyota hii anataka kufuga basi afuge kondoo na wengi wawe madume.

MAFUSHO

Mafusho yao yanaitwa Qist, yako kama vipande vya mizizi na yana rangi ya kahawia. Ili kupata bahati wanatakiwa wachome mafusho haya kila Jumanne asubuhi saa 12 mpaka saa 1 na saa 7 mpaka saa 8 mchana.

FUNGUO

Funguo yao ya mafanikio ni "UMIMI"

HATARI

Hatari ya punda ni kujiweka mbali na vitu vikali pamoja na moto pia hutakiwa kujiweka mbali na kukimbiza hovyo magari. 

Maana wao hupoteza muelekeo kwenye spidi vichwa vyao huvijua wao wenyewe na hupenda kujiweka karibu na vurugu na sehemu za hatari hivyo kama wewe ni Nyota yako hii epuka mambo hayo

MAMBO MUHIMU:-

mara nyingi huwa nyota ya umimi kwanza punda ni watu ambao kama ilivyokuwa ni nyota ya kwanza basi wao huwa mstari wa mbele sana katika kufanikisha mambo kwa haraka. 

Lakini pia ni watu ambao hawaoni shida kuanza moja kwa jambo lolote lile wao huonekana kama watu wa maajabu sana katika maisha.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo yao ni “kuwa waangalifu”

Maadili yao ni “Utumiaji wa nguvu, Ujasiri, Uaminifu, kuwa huru na kujitegemea.

Matakwa yao ni Vitendo

Tabia za kujiepusha nazo:
Kutokuwa na subira, kufanya mambo haraka haraka bila kufikiri, kutumia nguvu bila akili na kuharakisha mambo.

Punda ni nyota ya kwanza ambayo huonesha mwanzo mpya na huonyesha mabadiriko ya haraka.
Maisha kwa mwenye nyota ya punda yanathibitisha yeye kufikia mahala sahihi ambapo yatamletea faida na ni moja kati ya nyota za mali.

Vilevile ni moja kati ya watu ambao wakipigania kitu kwa ajili yao basi hawatulii hadi waweze kufikia mafanikio yake.

Kwa uhakika watu wengine huthibitisha kuwa wenye nyota hii ni viumbe waliojawa na maajabu katika utendaji ushupavu na uhodari wao.

Ni nyota ya watu ambao huwa kupumzika kwao ni muda mfupi tu na ni viumbe shapu zaidi kuliko nyota zingine.

Wenye nyota hii ni watumishi wazuri na wenye kufanya mambo yao kwa uharaka zaidi ni watu ambao wanataka kusikia mambo ya haraka haraka na ni watu wa kupenda matokeo ya sasa hivi kwa maneno mengine ni viumbe wasio na subira au kupoteza muda.

Mara nyingi ni watu wenye hasira za karibu na kauli ya “Kumsikitikia mtu" ndio mara nyingi huwa nayo.

watu wanapokutana na mtu mwenye nyota hii basi humuona ni mwenye kusisimua katika kuongea na umahiri sana.

Wengine huwa na bahati sana ya kutotolewa maneno makali na watu wenye nyota hii.
kama mtu akileta mada kwa mwenye nyota hii basi atafurahika jinsi alivyo mahiri katika mazungumzo,

Mwenye nyota hii ni mtu wa wa vitendo zaidi kuliko maneno ukitaka muendane nae basi uwe ni mtu wa vitendo zaidi kuliko maneno tu.

Ni watu shupavu na wenye nia ya kufanikisha mambo wao binafsi bila msaada wa mtu.
Kwa kuwa asili yao hujielezea kwa nguvu basi hukata mawasiliano na yoyote mwenye kuleta maongezi ambayo humfanya kujihisi kero na kutokuwa na mawasiliano nao tena.
na kama hii ni nyota yako basi unatarajiwa kuwa kiongozi wa asili ambaye ni mwenye kujiamini.

Mara nyingi hili huonekana tangu akiwa na umri mdogo basi wao huhisi unaelekea mafanikio.
mwenye kupenda kufurahi, pia ni mkarimu juu ya kusaidia wengine katika migogoro.

wanakuwa ni marafiki wenye mioyo iliyo wazi ambao hushiriki maoni na ushauri, na wanapenda kuchukua hundi.

huwa na ubora wa ukubwa. Ni watu ambao hawavutiwi na vitu vidogo vidogo. wao hupendelea mambo makubwa na yenye ubora.

Hakuna mambo nusu nusu kwao wakati wengine wakiwa na uoga wa mambo au kupenda mambo nusu nusu basi wenye nyota hii ni wenye kujitoa zaidi na kuwa mstari wa mbele kwa kila kitu

Kufanya mambo bila tahadhari yani kujitupa ni asili yao na ni kitu kinachowafanya wajihisi wapo hai.
kukimbizana na muda ndio jadi ya wenye nyota hii zaidi kuliko hata kufikia mafanikio wao wanachowahi huwa ni muda na ukiwakuta mara nyingi ni watu wenye kupenda kutembea haraka haraka

Vile vile ni watu wenye mtizamo wa kuhitaji zaidi kuliko kupata ni watu wenye kucheza kamari au kubahatisha mambo na kufuata ndoto zao na kuweka malengo yao na kuyafuatilia vema na shauku isiyozuilika

utendaji wao na ubora wa matumaini huvutia wengine. Japokuwa nyuma ya pazia anaweza kuwa hana uhakika na analofanya. 
lakini huwa ni mvuto mkubwa kwa wengine kutokana na energy aliyonayo na hakuna mtu anaweza kutambua hilo kirahisi
Na hii haimaanishi kuwa hawabadiriki au hawakosei hapana ni vile tu wao huwa wapo straight forward

Vile vile majira ya baridi huwapelekea kuwa wenye kukata tamaa lakini hayadumu wiki na wenye nyota hii hurejea katika hali yao ya kukimbizana na Maisha.

ni wenye matumaini yasiyovunjika.
Ni kweli, hata hivyo, ni kwamba watu wa nyota hii wanajulikana kwa kukasirika kwa kupenda
vitisho au mikwala vile vile ni watu hupata majeraha madogo madogo.

Hasira za karibu na utoto mwingi,
na kizingiti chao cha kuchoka ni vikali sana na huwashusha chini katika kufanikisha wanachokitaka.

Ikiwa mafanikio sio ya haraka, basi wao huwa wanapoteza
hamu ya kuendelea na hicho kitu na kuamua kujishughulisha na mambo mengine Matokeo yake, subira, kwenda taratibu kwa mambo na na kuvurugika kichwa ndio kitu huwa kinaingia akilini vijana wa mjini wanaita Jam za kichwani.

Wenye nyota hii wana sifa ya kutokumaliza jambo waliloanza, wengi wao huishia njiani vitu wanavyofanya haijarishi wameanza nini.

Ni watu ambao hupungukiwa na uvumilivu, au subra na ukosefu wa kushikamana na dhamira za wengine ndio kasoro zao na ni kitu wanatakiwa kujirekebisha na ndio moja kati ya udhaifu wao ni watu hutumia nguvu zao kwa njia nyingi tofauti,

Uhuru ndio neno pekee au kitu pekee wao hupenda hugeuka mbogo au kuwa na hasira ukitaka kuwatawala sana na kuwaamrisha ni wenye kupenda ukubwa na kuheshimika na wenye kupenda kila kitu waendeshe au waongoze wao.

Na wakishindwa basi hujilazimisha walau hata kidogo wakafiti sehemu husika mradi tu wawe wenye kuonekana wamefanikisha upinzani wao huwa hawashindwi na yoyote isipokuwa nafsi zao wenyewe kuacha kujiamini.

wao huona ni bora zaidi kuwa mjusi mkubwa zaidi ulimwenguni kuliko kuwa nyoka mdogo zaidi ulimwenguni maana yake hata awe dhaifu vipi hutaka kuwa mkubwa tu.

Wengi wenye kujigamba wao ni maskini jeuri basi huwa na nyota hii kwa maana huthibitisha kiburi cha hali ya juu
Moja ya mbinu zao kimsingi ni kuwa wabinafsi.

Isipokuwa watajitahidi kuweka muonekano mzuri kwa wengine na kuficha hisia zao za ubinafsi,
Ingawa kwa ujumla ni waaminifu na wenye kuaminiwa, uwezo wao kudanganya ni mdogo na wakikudanganya. 

Basi utahisi ni kweli lakini ni mwepesi sana kugundulika kwa maana uongo wao huwa haujifichi vema kama wenye nyota ya mbuzi.

watu wanapo watizama wenye nyota hii basi huwaona ni wenye kukosa busara yani maneno yao hayana busara japokuwa yanakuwa hayajabeba uovu wowote vilevile kukosa huku busara ni sawa na wenye nyota ya mshale maana nao ni moto .

lakini moto wa punda na mshale na simba ni tofauti japo kwa kiasi kidogo nguvu zao hufanana wengine huwaona wasema hovyo au midomo haina break. 

Na wengine huwa na sauti kali kidogo au ya ubabe mara nyingi ni watu wenye kuzungumza bila kufikiria na kusema chochote kinachoingia kinywani mwao. Na kawaida hujuta baadae kwa nini walisema.

Japokuwa dhamira zao hazikuwa mbaya wakati wanasema. Wenye nyota ya mshale vile vile huwa na hii tabia.

Ni nyota yenye bahati sana kipesa lakini inamatatizo sana katika matumizi ya pesa kwa maana ni nyota ambayo wanatumia pesa inayayuka kama moto na pale ambapo pesa ikiisha ndio roho zao hutulia.

Matumizi yao ni makubwa sana na ni watu ambao hawaoni tabu kununua chochote cha bei ghali mradi tu ana pesa mfukoni.

Ni wenye kiburi sana wanapokuwa wanadaiwa na katika urafiki ni watu wenye kutoa sana kwa wale wenye uhitaji lakini ni watu wenye kupenda kupata sifa wanapotenda wema.

Katika bustani kama ni wenye kupanda basi utakuta kuna zambarau kidogo.
Vile vile ni wabunifu, wenye mioyo iliyo wazi, wenye roho nzuri sana, na wenye kupanuka kimawazo, pia wenye kushauri bure, na wenye papara. na vilevile mwenye kujishughulisha

Basi kwa wenye kujihusisha na wewe watakuwa na shida moja kuu:

Je! Watawezaje kwenda na kasi yako?

NDANI YA MOYO/ROHO AU AKILI YAKO

Unapenda kuwa mwenye dhamana au kubeba majukumu na mwenye kupenda kuongoza mambo yako wewe mwenyewe na sio kuwa chini ya kauli ya yoyote.
 
Ni mtu mwenye kupenda kufanikisha mambo unavyotaka na mwenye kupenda kujipa msukumo mwenyewe wa kukamilisha jambo.

Japokuwa ndani yako umejawa hofu na kujichanganya ni jinsi gani unaweza kukabiliana na kila kitu wewe binafsi, ni mtu mwenye kuchukia kuchoshwa na ni mtu mwenye kuangalia mtazamo mwingine ikiwa mmoja unakukera.

watu wapya na mazingira mapya ni vitu ambavyo hukuvutia zaidi na ni mtu ambaye subira au uvumilivu wako ni mdogo unatakiwa kujifunza kuwa na subira na vile vile huna subira na watu ambao hawawezi kukutatulia shida yako. 

Una imani zaidi na vitendo yale uliyonayo ni ukarimu na shauku ingawaje unasumbuliwa na kutokujikubali. Hali ya kuwa unajua kwamba kama unataka kufanya jambo basi unaweza!

MITIZAMO YA WATU KWAKO

Ni mtu mwenye mvuto kwa watu, tabia yako ya sumaku huwavuta watu kukufuata ni mtu ambaye unaweza kuwaletea watu msisimko katika maisha yao.
 
Wanatamani jinsi unavyopambana ukikutana na changamoto. Shida yoyote ile, unaonekana ni mwenye kutoa maoni kana kwamba ni mtu mwenye jibu tayari.
 
Unawavutia pia kwa uaminifu wako; huonekani kuwa mwenye shida.
Kile ambacho watu hawapendi ni tabia yako kuelekea ukiritimba na sifa yako inayostahiki ya
kuwa na ulimi mkali.
 
Wanaogopa kukuvuka katika hoja kwa sababu wanajua unaweza kuzikata kwa haraka.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao “Wanaelewana” nao ni nyota za Simba na Mshale

Nyota za watu ambao “Hawaelewani” nao ni nyota za Kaa, Mizani na Mbuzi.

Nyota inayomsaidia “Kikazi” ni nyota ya Mbuzi

Nyota inayomsaidia “Kipesa” ni nyota ya Ng’ombe

Nyota inayomsaidia katika “Ubunifu” ni nyota ya Simba.

Nyota bora ya “Kujifurahisha” ni nyota ya Simba

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya “Kidini na kiroho” ni Nyota za Mshale na Simba.

WATU MAARUFU WENYE NYOTA YA PUNDA

Ambao unaweza kuwapima kwa maelezo haya ya nyota yako niliyokupa ni:

nyota ya punda

Maya Angelou
Johann Sebastian Bach
Alec Baldwin
Warren Beatty
Marlon Brando
Matthew Broderick
Charles Chaplin
Na wengineo wengi

Wasiliana nasi

Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia email lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.

Unaweza kutupata kwa kupitia Email, vile vile kwa namba za simu, kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,

Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.

Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na RakimsSpiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.

Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa Members pekee;

Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia:-


Rakimsspiritual@gmail.com

au

mnajimu@unajimu.com


WhatsApp number


+255 783 930 601


Rakims

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !