Nyota ya Mapacha (Gemini)

Rakims

Nyota ya Mapacha (Gemini)

Hii ni nyota ya tatu katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 May na 20 June (Kwa nyota za magharibi) na 15 June hadi 16 July (Kwa nyota za mashariki) au wenye majina yalioanza na herufi J au C.

ASILI YAKE

Asili au maada yako ni Upepo.

JINSIA

Kiume

WASIMAMIZI WAKE

Malaika anaetawala sayari na nyota hii anaitwa Raphael au Mikyaail. Jini anayetawala sayari na siku ya Jumatano anaitwa Barkaan au Ophiel. Herufi ya Jumatano ni T.

SAYARI YAKE

Mercury: Katika unajimu Mercury inatawala Mawasiliano. Sayari hii inahusika na ujuaji wa haraka na hali ya neva za mwili.

ALAMA YAKE

Ni watu mapacha: huhusishwa na pande mbili, ubinadamu, utofautishaji au mawasiliano.

TALASIMU YAKE

Picha inayowakilisha takwimu mbili za Mapacha. Huonyesha mikono au mapafu ya mwanadamu (sehemu ambayo mapacha hutawala). Mistari miwili wima imefungwa juu na chini, ikiwakilisha hekima, ujifunzaji na nguvu za akili.

NENO TAWALA

"Ninafikiria" – wakifikiria kitu hukamilika/kufanikisha.

NYOTA INAYOIPA NGUVU

Mshale: Mapacha ni nyota ya fikra na mawasiliano ya binafsi. Mshale ni nyota ya falsafa na mpanuko wa akili, inawasaidia Mapacha kuondoa ubinafsi.

HADHI YAKE

Tukufu

SEHEMU YA MWILI

Mikono, viganja, mabega, na mapafu. Mapacha hushambuliwa na matatizo ya ajali za mikono, mkamba na maradhi ya kupumua.

SIKU YA BAHATI

Jumatano

NAMBA ZA BAHATI

5 na 9

KITO CHA MIUJIZA

Agate/Akiki: Humkinga na uongo, hutoa ufasaha hasa katika matamko ya upendo.

RANGI MAALUMU

Njano inayong’aa, Bluu, Njano ya Chungwa. Wanashauriwa kutumia rangi za njano au bluu isiyoiva. Rangi za Mapenzi: Samawati (Sky Blue). Rangi ya Kipato: Kijivu na Fedha.

MIJI NA NCHI

London, San Francisco, Versailles, Melbourne. Nchi: United States, Wales, Belgium.

MAUA

Lily ya bondeni na Lavenda.

MITI

Mti wa Ntobo na miti yote yenye kutoa matunda makavu.

MANUKATO

Mrujuani (Lavender), Lilaki (Lilac), Yungiyungi.

MADINI

Mercury

WANYAMA

Ndege wenye rangi nzuri na vipepeo.

HATARI

Matatizo katika safari hasa za angani. Tabia zao hubadilika na kuwakasirisha wengine, mara nyingi huamua vibaya.

MAMBO MUHIMU

Sifa: Kubadilika badilika. Ubora: Kuwa na fikra za ndani. Maadili: Ujasiri wa mawasiliano, kufikiria haraka, kujua mambo. Epuka: Kusengenya, maneno makali, propaganda.

USHIRIKIANE NA NANI?

Anaelewana na: Mizani, Ndoo. Haelewani na: Mashuke, Mshale, Samaki. Kikazi: Samaki. Kipesa: Kaa. Ubunifu: Mizani. Burudani: Mizani. Kiroho: Ng’ombe, Ndoo.

KIPAJI CHA MAPACHA

Kipaji cha kuwasiliana na watu walio mbali kwa akili au hisia (Telepathic).

TABIA KIMAUMBILE NA KIMAPENZI

Mchangamfu, mwenye nguvu, msomi. Anaishi katika akili badala ya mihemko. Wana hisia kali, wanakasirika haraka, ni wazungumzaji na wenye kushawishi. Wanapenda mabadiliko, kujumuika, na kusafiri. Wana sura mbili, hubadilika haraka. Katika mapenzi hutumia maneno matamu, lakini uaminifu ni mgumu kwao.

Wengi huishi maisha ya sehemu mbili, hivyo bora kupata mwenza mwenye malezi ya dini kuliko kumpenda mwenye nyota hii.

KAZI NA BIASHARA

Kazi za utangazaji, Radio na TV, vitabu, uchapishaji, kufundisha, ushauri nasaha, ukalimani, biashara za safari.

MAVAZI NA MITINDO

Nguo za kisanii, nyepesi na zilizonyooka, rangi Njano na Nyeupe, vitambaa vya hariri, suti na gloves.

MAGONJWA

Tatizo la kutopumzika linawapa matatizo ya neva. Magonjwa yao: Bronchitis, Asthma, kifua, mafua, ajali za mikono na mabega.

VYAKULA

Kuku, rasiberi, karoti na uduvi.

MAFUSHO

Kashuu Muhlib (kachiri). Choma Jumatano saa 12-1 asubuhi au saa 7-8 mchana.

Wasiliana nasi

Email: Rakimsspiritual@gmail.com

WhatsApp: +255 783 930 601

Rakims Spiritual

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !