
Nyota ya Simba (Leo)
Hii ni nyota ya Tano katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Julai hadi 22 Agosti au wenye majina yanayo anza na herufi E au Q au S au T.
Usawa wake ni Dume. Asili yake ni Moto. Tabia yake ni Thabiti. Sayari yake ni Jua (Sun).
Siku yake nzuri ya bahati ni Jumapili. Namba ya bahati ni 1, 3, 10, 19 na 4.
Malaika wake anaitwa Michael au Raukayaeel. Jini anayetawala Jumapili anaitwa Abdulahi Saeed al Madhhab au Och.
Rangi zao ni Dhahabu (Gold), Nyekundu (Red) na Machungwa (Orange).
NGUVU YA NYOTA HII
Wenye nyota hii huwa na nguvu ya Ubunifu, shauku, ukarimu, moyo safi, furaha, na kupendelea kucheka.
UDHAIFU WA NYOTA HII
Kiburi, ukaidi, kujitegemea, uvivu, asiye na akili.
WANACHOPENDA
Wenye nyota hii hupenda maeneo yenye kujichanganya kwa watu kujionyesha, kuchukua likizo, kupenda mambo makubwa ya gharama, rangi zenye kuwaka, na kujifurahisha na marafiki.
WASICHOPENDA
Kupuuzwa, kukubaliana na hali, na kutokutukuzwa kama mfalme au malkia.
MAMBO MENGINE KUHUSU WAO
Wenye nyota hii ni watu wenye bahati sana hasa kulingana na nyota yao katika maswala ya kiuchumi, japokuwa wanatumia pesa hovyo. Vile vile ni watu wanaoogopwa kwa ukali wao, lakini pia ni wabunifu, wakarimu, na viongozi wa asili.
Simba mara nyingi huwa na marafiki wengi kutokana na ucheshi na uaminifu wao. Wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi zinazochangamka kama Dhahabu na Njano.
Rangi za Mapenzi na Furaha ya kijamii: Nyeusi (Jumamosi), Bluu iliyoiva (Indigo) na Bluu ya Samawi (Alhamisi). Rangi ya Kipato: Njano na Njano-Machungwa.
Kito (Jiwe): Amber, Ruby, Chrysolite, Yellow Diamond, Petrified Wood Garnet, Diamond, Jasper, Quartz na Onyx. Kito kikuu: Ruby.
Madini yao ni Gold (Dhahabu). Manukato yao ni Miski (Musk) na Uvumba.
MAMBO MUHIMU
Sifa ya Nyota hii ni Uimara na Kutokubadilika.
Ubora unaohitajika: Unyenyekevu.
Maadili yao: Uwezo wa Uongozi, Kujiamini, Ukarimu, Ubunifu na Kupenda raha.
Matakwa yao: Starehe, Kung’ara mbele za watu, Kujikweza.
Tabia za kujiepusha nazo: Kujisifu, Kiburi, Kuamrisha.
USHIRIKIANE NA NANI?
Wanaelewana: Punda na Mshale. Hawaelewani: Ng’ombe, Nge na Ndoo.
Nyota ya Kikazi: Ng’ombe. Nyota ya Kihisia: Nge. Nyota ya Kipesa: Mashuke. Nyota ya Ubunifu: Mshale.
Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano: Ndoo. Nyota bora ya Kujifurahisha: Mshale. Nyota za Kiimani/Kiroho: Punda na Kaa.
KIPAJI CHA SIMBA
Simba wana kipaji cha ufunuo wa kiungu, uongozi, na kuponya kwa mikono. Pia wana uwezo wa kuvumbua mambo ya fedha na kipekee.
TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI
Simba hupenda sifa, utajiri na heshima. Ni wakali sana katika mapenzi, mara nyingi hawawezi kudumu kutokana na ghadhabu zao. Ni wakarimu lakini wajeuri, wenye hisia kali, na mara nyingine huficha maumivu ya ndani.
KAZI NA BIASHARA ZA SIMBA
Kazi zinazowafaa: Usimamizi, Michezo, Uongozi wa vijana, Usonara, Mitindo ya mavazi, Uigizaji, Uendeshaji wa sinema, Ualimu.
MAVAZI NA MITINDO
Mitindo yao iwe ya kifalme na Kitajiri. Kitambaa kiwe cha hariri inayong’aa, velvet au kilicho tariziwa. Rangi: Dhahabu. Wanawake: Magauni ya Dhahabu au Machungwa.
MAGONJWA YA SIMBA
Nyota hii inatawala moyo, sehemu ya juu ya mgongo na bandama. Magonjwa: Shinikizo la damu, Maradhi ya moyo, Homa ya uti wa mgongo.
VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA SIMBA
Vyakula: Machungwa, maboga, vitu vichachu (ndimu, malimao), nyama za ng’ombe, mbuzi na kondoo. Nchi: Italia, Morocco. Miji: Bombay (India), Roma (Italia).
MADINI, VITO NA MAFUSHO
Madini: Dhahabu. Vito: Peridot, Ruby. Mafusho: Sandarusi (Jumapili saa 12-1 asubuhi na 7-8 mchana).
FUNGUO
Funguo ya Simba: "Nita" – anaposema atapata au atafanya basi hukipata.