Nyota ya Ng'ombe (Taurus)

Rakims
0

 NYOTA YA NG'OMBE (TAURUS)

Hii ni nyota ya pili katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya tarehe 20 April hadi May 20 au wenye majina yalioanza na herufi B au V au U jinsia ya nyota hii ni Jike.


Nyota hii ya Ng'ombe ni Nyota ya mtu mkimya, mwenye upendo, mvumilivu, mwenye utulivu, mwenye dhamira na vitendo, mkaidi, na anayepinga mabadiliko.

Ng'ombe ni nyota yenye sifa za ukimya, upole, sikivu, usawa, ujeuri na kutokukubali kubadilika.


SAYARI YAO

Venus (Zuhura) kwa historia za kale Nchini Roma ilikuwa ikiaminiwa kama moja kati ya miungu yao ya kike ambaye ni Mungu wa Urembo na Sanaa vile vile raha na mihemko.
Kinyota Sayari hii ni sayari inayoshawishi kupelekea kupenda anasa na uweze wa kipekee wa ubunifu,

UBORA WAKE

Ni nyota isiyohamishika (fixed sign)

ALAMA YAO

Ng'ombe DUME: Ambayo huwakilisha Nguvu, mkaidi, mwenye kujivuta, anayeweza kuwa na tabia mbili kwa pamoja mkali na mpole.

TARASIMU YAO

Ni Picha inawakilisha pembe na kichwa cha Ng'ombe Dume.
 
Nyota ya Ngombe


Pia inayoonesha kidevu na vile vile koo la kiume lenye kuchomoza kwenye shingo nyota hii inapotawala ambayo huwakilisha nguvu ya mali na utajiri unaotokana na nguvu ya mapenzi (duara).
au majaliwa ya mapenzi.

NYOTA INAYOENDANA ZAIDI


NGE

Ng'ombe ni nyota ya mali na pesa. Wenye nyota hii wanajali sana kukusanya mali na wanajulikana na wenye kufanyia uchoyo kwa kile kilicho chao.
 
Nge, ni nyota ya kinyume na Ng'ombe, Nge ni nyota ya urithi na utajiri wa pamoja. Utajiri wa Nge
ni wa watu ambao huwa kiroho badala ya ubinafsi, ambao huwapa wengine kwa njia ya kufundisha, kuandika, na sanaa ya uponyaji.

hivyo ni sawa na kusema nyota ya kunyume chake kwa maneno mengine ni nyota ambayo inaweza kuiweka sawa.

SEHEMU YA MWILI INAYOTAWALA

Shingo ni eneo ambalo nyota hii inatawala pamoja na koo.
watu wengi wengi wenye nyota hii wana sauti nzuri kama sio za kuzungumza basi za kuimba lakini ni watu wenye kuwa wadhaifu sana katika baridi,koo kavu na matatizo ya kidaka tonge ikiwa ni pamoja na mfumo mzima wa sauti.

SIKU YA BAHATI

Ijumaa

NAMBA ZA BAHATI

6 na 4

KITO CHA BAHATI

Emerald: Ambayo humkinga kutokana na ukafiri na udanganyifu, inahakikisha uaminifu, na inaboresha kumbukumbu.

RANGI ZA BAHATI


Blue iliyopauka na rangi ya zambarau nayokwenda kwenye pink yaani mauve:
Rangi laini za uboreshaji na upole.

Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi za kijani au rangi za pinki au rangi ya bluu ambayo haijakoza katika nyumba zao au sehemu zao ya biashara ili kuleta mvuto wa kinyota.

NCHI ZAKE NA MIJI YAKE

Ili kupata mafanikio ya kinyota, kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota yao; 

Nchi hizo ni USSR (Urusi), Ireland, Leipzig, St. Louis Lucerne (Switzerland).
Ireland, Switzerland, Cyprus na Greece

MAUA YAKE

 Violet na Poppy

MITI YAKE: Mvinje na Tufaa

MADINI:
Kopa (Copper)

WANYAMA:
Ng'ombe

HATARI YAKE

watu wenye Nyota hii wana tabia ya kushiriki katika hali za vurugu zinazohusiana na mapenzi au pesa.
Mara nyingi huwachukiza wengine kwa uchochezi wa mapenzi kwa sababu ya ukaidi wao na umiliki wa kutaka kutawala.

KIPAJI CHA NG'OMBE


(BODY-CENTERED)
Wenye nyota hii wana kipaji kikubwa kilicho ndani ya mwili wao ambacho ni pamoja na kuelewa mambo kimbele, hesabu, kuponya kwa kutumia mikono na kwa kumwagia mtu maji.

TABIA YA NG'OMBE

Wenye nyota hii ni watu wanaopenda kujishughulisha katika shughuli nyingi. Ni watu wakarimu na wanaopenda kusaidia watu, na wana tabia ya uvumilivu na subira katika jambo lolote wanalolifanya.

Ni watu wenye malengo na wenye msimamo thabiti, wasiopenda kupindishwa na wana tabia ya ubishi na ukaidi hasa katika jambo lao wanalolitaka.

TABIA YA NG'OMBE KATIKA MAPENZI

Wenye nyota hii ni waaminifu sana katika mapenzi na wanaohitaji ulinzi katika mapenzi na njia au mwenendo unaoeleweka.

Pamoja na kwamba asili yao ni udongo, wanaweza kuwa ni wenye mahaba na mapenzi makubwa kwa wapenzi wao.

Uhakika wa mapenzi ndio jambo kubwa ambalo wenye nyota hii huangalia kwanza na baadae Penzi hilo liwe lenye hisia na mpangilio.

Pamoja na hisia kali walizonazo, wao ni watu imara na wasiobadilika hivyo kuwafanya watu wenye shauku kutovutiwa nao.

 Uaminifu ni jambo la pili ambalo wenye nyota hii wanalo hivyo kuwafanya wao wawe watu wenye kuaminika na hiyo inasababisha wawe wenye wivu kupindukia.

Wanachotakiwa kufanya ni kujitahidi kuwapa nafasi wapenzi wao la sivyo watajikuta wako peke yao. Ndoa kwao ndio uamuzi mzuri kuliko kuishi na wapenzi. Tabia yao ni ya kudumisha jambo fulani wanaloliamini au walilolianzisha na hawapendi kubadilishwa.

MATATIZO YA KIAFYA

Nyota hii inatawala shingo, koo, koromeo, kidevu na sehemu ya chini ya taya.
Kwa asili wenye nyota hii ni watu wabishi na wenye kufanya mambo kwa upole na wagumu kubadilika.

Wanapenda sana vyakula vitamu na vyenye mafuta na huwezi kuwabadilisha katika hilo na wengi wao wanakuwa wanene kupita kiasi na inakuwa ni vigumu sana kuwashawishi kuamka na kufanya mazoezi ya mwili.

Tatizo lingine ni kufanya kazi kupita kiasi ambalo linawafanya wapate matatizo ya mvutano na misuli hasa katika sehemu zilizotajwa. wenye nyota hii wanatakiwa wajihadhari na mpangilio wao wa chakula na wafanye mazoezi kwa wingi.

KAZI ZA WENYE NYOTA YA NG'OMBE


Wenye nyota hii wana falsafa ifuatayo kulingana na kazi; "panda mbegu iote, mti uote halafu ule matunda". Ni watu ambao wanafuata mpangilio wa kikazi na wanaopenda kujituma na kujishughulisha. Wengi wenye nyota hii ni wafanyakazi wazuri na wanapenda wapewe muda kujenga vipaji na utaalamu wao wa kazi.

Kazi zao zinakuwa kazi za muziki, kazi zinazohusiana na chakula, hoteli, migahawa, kazi za ujenzi, kazi za mashamba, kazi za uhasibu, na kazi za sanaa hasa uchoraji au uchongaji vinyago.

FAMILIA ZA NG'OMBE


Wazazi wa familia za Ng'ombe ni watu wenye msimamo, wakutegemewa na wanaothamini familia zao, na wako tayari kugombana na mtu yeyote kwa ajili ya watoto wao. 

Ni wazazi wanaopenda kufuata mambo ya kizamani au ya asili hasa katika masuala ya nidhamu. wanapenda sana kuheshimiwa na watoto wao na huwashawishi au kuwashauri wawe huru.

Ni wazazi wanaotegemea watoto wao wafuate nyayo zao hasa katika biashara au kazi wanazozifanya, hivyo watoto wa wazazi Ng'ombe wanakuwa na muda mdogo wa kufikiria mambo mapya. 

Ni wazazi ambao hufanya kazi kwa bidii kuhakikisha watoto wao hawakosi wanachokitaka na wanapenda watoto wao wawe na elimu nzuri. Hata hivyo ni wazazi ambao wanategemea watoto wao wafuate wanavyotaka wao vinginevyo inakuwa matatizo.

MADINI YA NG'OMBE

Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa EMARALD.
Mawe haya yanawafanya wenye nyota ya ng'ombe wawe katika hali yao ya kike kike (Feminine) vili vile thamani ya mawe haya ni uthibitisho wa nyota hii katika fedha.

UHUSIANO WA KIMAPENZI

Tabia ya uaminifu na ukweli waliokuwa nao wenye nyota ya ng'ombe inakuwa ni faraja kubwa kwa nyota ya Nge ambao wana tabia ya wivu kupita kiasi na kudhania maovu, kutuhumu na kushuku.

VYAKULA VYA NG'OMBE

Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndivyo vinavyotawaliwa na nyota yao; Tofaa (apple), (oysters), viazi mbatata (potatoes), na dover sole.

NENO LAKE TAWALA


Funguo za mafanikio yao ni "NINACHO" kujihisi kuwa teyari kashakimiliki anachokitaka basi hukipata.

MAMBO MUHIMU


Unaonekana kuwa ni mtu ambaye wengine wanamtegemea katika kuongeza msukumo wa mambo yao,
pia unaonekana ni mtu anayevumilia au aliyemvumilivu wakati wa kuvunjika moyo na kutengwa.
 
Kwa sababu uvumilivu ndio jambo bora zaidi kwako linalohitajika kwa mafanikio, na mara nyingi wewe ukiwa mvumilivu basi huwa unafanikiwa.

Pia unaonekana kutokuwa mwenye ushindani wa kugombania kuwa wa kwanza,
lakini ni mtu mwenye kwenda taratibu na kufikia malengo

Nyumba na miji hujengwa kwa udongo. Kama ni mtu mwenye nyota hii basi ni mtu unaonekana kuwa na ukaidi ndani yako

Nguvu yako kubwa inaonekana kuwa ni msisitizo wa mambo na kuwa thabiti, na unaonekana kuwa ni mtu mwenye makusudi zaidi,

Ni mtu mwenye subira sana ambaye huwa na subira hadi kuona mwisho wa jambo unaisha vipi.
unakuwa ni mtu wa kiasilia usiye pindishwa na mwenye nguvu isiyoweza kuzuilika ukilitaka lako.

Nyota hii ya Ng'ombe ni nyota ambayo ni thabiti, maana yake ni kwamba mwenye nyota hii sio wa kubadilika badilika kama nyota zenye nyuso mbili au nyota vigeugeu. Nyota ya Ng'ombe yenyewe huwa thabiti hivyo ni nyota ambayo huwa haikimbilii jambo lolote jipya kwa pupa

Ni mtu mwenye njia tofauti ambazo hutengeneza kutokuwa na wasiwasi ndani yako.
Unakuwa huru zaidi pale tu unapokuwa na watu wa karibu na familia yani watu wa ukoo wako,

ni mtu huwa na mtazamo wa kufupisha mambo kama "Ikiwa kila kitu kinaenda sawa na kipo kawaida kwanini tuhangaikie na jambo jipya"?
“Hakuna mtu anaekuona ukiwa umepandisha hasira ni mara moja sana na kwa muda mfupi tu
Ni mtu ambaye ni mpenda haki na msawa vile vile ni mvumilivu na hata kama ni kutiwa hasira basi itachukua nguvu kubwa sana hadi umtie hasira.

Walakini vile ni mtu ambaye unakuwa na moto unaokuwaka ndani yako japokuwa ni mtulivu lakini ni mtu mwenye uchungu na hasira za ndani za kujificha na ni mtu ambaye huanzishi shari na mtu bali mtu akikuanzishia shari hujuta.
 
Ni isimu ya ng'ombe mnyama jinsi anavyokuwa na upole na ukimchokoza basi anaanza kupandwa na hasira.
Ni mtu mwenye kujali,kutoa na mwenye mapenzi na watu lakini watu wengi wanaomzunguka huwa wana mtumia

Ni mtu mwenye kupenda kila kitu kizuri,
Kutawalia na Sayari ya Zuhura sayari ya mapenzi na urembo au uzuri, ni mtu uliyejaliwa ubunifu na mchoraji mzuri na mwenye kuvutia katika sanaa ya kuchora au muziki.

Ni mtu mwenye ladha ya kifahari sana. mwenye jicho la kupendezewa kwa kile ambacho ni cha thamani na kawaida huwa mwenye kupenda sana kukusanya. 

Kwa hakika, kama ulizaliwa chini ya nyota moja kati ya nyota hizi mbili yaani Ng'ombe na nyingine ni (KAA) basi jua upo kwenye nyota zenye bahati sana maana nyota yaNg'ombe inawakilisha mali,vitu,utajiri, na pesa.

Mara nyingi sana wenye nyota hii utawakuta wanafanikiwa pindi tu watakapo jiingiza katika sanaa ya uchoraji au muziki basi huwa na majina makubwa na vile vile katika chochote kila kinachohusu uzuri basi huwanufaisha.

Na kama watahitaji mafanikio basi wajihusishe na kazi za mapenzi na nyumba na ndoa. au wengi wao hufanikiwa zaidi wanapoingia kwenye ndoa na kuishi makwao katika ndoa zao.

Ni mtu mwenye matumizi makubwa na mwenye kupenda kuzungukwa na vitu vya thamani ikiwa ni pamoja na kuwa na pesa karibu karibu.

Watu kuishi na wewe ni kazi kidogo;
Unaweza kuwa mbabe,
mwenye usiri, ubahili, mvivu maoni na tuhuma kuwashutumu watu, na ni mtu mwenye ushindani wa kisiri siri pamoja na wivu.
ni mtu mgumu kusongwa na mawazo maani ni mtu huwa unajifurahisha mwenyewe.

Vile vile ni mtu ambaye huwa na aibu hasa kwa wageni na pia hujitenga na sehemu inapokuwa na wageni au mkusanyiko wa watu,
lakini anapohitajika huwa ni mhudumu mzuri na kujishughulisha na watu kwa kuchanganyika nao vema,
Ni mtu mwenye kupenda kujitengenezea vema mazingira yake na maisha yake kwa ujumla ni watu wanaojipenda na kutamani kuwa na hali nzuri muda wote.

NDANI YAKO

Unahitaji kuamuru na kupangilia maisha yako —unapata wasiwasi wakati mambo yanapokuwa hayaendi au kuonekana kukuzidi. 

Na chochote kisicho julikana hukufanya ukose kujiamini, ni mtu mwenye kujiengua kujaribu vitu usivyo vijua. Unahitaji kuwa huru zaidi ili kuweza kubadirika.
Kuwa na vitu vizuri ni muhimu zaidi kwako, na machale yako yanakupa kujimwaga katika mahusiano.

Ni mtu wa kuwashikiria haraka wale unaowajali wanapokuhitaji na ni mwenye marafiki wachache wa karibu, Katika mapenzi unafurahia mapenzi na watu wenye kujituma na kujali.

Ni msiri sana - na ukisema neno kwenye mapenzi na likakataliwa kwa ukali basi huwa inakukasirisha sana — na kwa mahusiano mageni, mara nyingi hupendi mtu mwenye kujisikia au kujitambua.

MITIZAMO YA WATU

Unafikiriwa kama mwenye ushawishi wa utulivu, na mtu ambaye hutegemewa na watu, na watu wanavutiwa na akili yako iliyopangwa. Sio watu wengi wenye kujua au kujali maumivu yako au kukujali.

Vile vile ni mtu unaeonkana kwa watu kama mtia chumvi au laghai, kwa sababu unayo silika za sauti kuhusu pesa, ni mtu pia ushauri wako wa kifedha huhitajika.
 
Kwa upande mwingine, watu wanachukia tabia yako ya kuwa mwenye msimamo mkali au itikadi.
Hata ikiwa unasema kweli, wengine wanakuwa hawaelewi na kufikiria wewe ni king'ang'anizi,

Huo ndio mtizamo wa watu kwako.
Fuata na rekebisha yanayohitajika kinyota utaona mabadiriko mengi katika maisha


Nyota ya Ng'ombe

Wasiliana nasi

Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia email lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.

Unaweza kutupata kwa kupitia Email, vile vile kwa namba za simu, kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,

Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.

Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na RakimsSpiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.

Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa Members pekee;

Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia:-

Rakimsspiritual@gmail.com au mnajimu@unajimu.com

WhatsApp number: +255 783 930 601

Rakims
Tags

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !