Kuhusu sisi

Rakims
0

 Kadiri ninavyoendelea kuwa mnajimu—ambapo kwa wakati huu ndivyo ninavyotambua zaidi kwamba kile sisi sote tunataka kujua ni kuhusu sisi wenyewe kwanza.

“Mimi ni nani?” unaweza kuwa unajiuliza au unataka kujua ni kipi kinakufanya ujiulize hivyo, kwa nini una hisia kali kama hivyo tofauti na watu wengine, na unapenda kufahamu kuhusu wengine pia kama hujiuliza mambo nyeti ama huwaza kama unavyowaza wewe. Watu wengi huniandikia katika email na kunitafuta kupitia njia zangu za mawasiliano asilimia kubwa wananiandikia kuuliza maswali kama vile:

  • "Ninapaswa kutafuta mwanaume/mwanamke wa aina gani?" 
  • "Kwa nini sina furaha na kazi yangu?"  
  • “Je ni nini ninaendana nacho kinyota?
  • "Nani anaweza kunifaa katika mapenzina Je, tutafurahi pamoja?" 



Wengi wao huniulize kama watapata upendo wa kweli na lini watavuka nje ya kipindi cha huzuni au hofu au mzigo mzito wa matatizo. 

Wengi wanauliza juu ya njia yao ya maisha na jinsi gani wanaweza kupata mafanikio ya yale wanayoyahangaikia.
Kwa hiyo naendelea kuona kwamba sababu ya unajimu kuwepo ni kujibu maswali kuhusu wewe. Na yote kuhusu muhusika na yale anayohitaji kuyajua.


Unajimu umefafanuliwa kama ngazi inayoomuongoza mtu ndani yake binafsi na ubinafsi wake zaidi. Unashikilia ahadi ambayo hutafanya jambo isipokuwa lazima upitie maishani ambayo teyari yapo na ambayo ni hali zilizopo ama zitakazo tokea baadae hivyo ukiguswa na uzoefu, ni sawa na vile wote tunafahamu kuwa kiumbe hai huzaliwa hii haita badirika na vile vile huishi nalo hili halitabadirika pia vile vile kufa ni lazima kwa kila kiumbe ikiwa matarajio kama haya yanafahamika na kujulikana teyari kwamba unaweza ndani ya mipaka kuelekeza hatima yako mwenyewe na ndani mchakato kufikia katika mapito unayopitia kama kujua mtu mbaya huishia pabaya na mtu mwema huishia pema ndivyo hivyo hivyo kama akijua elimu ipi itamtambulisha yeye ni mbaya na pema ni wapi basi ana asilimia kubwa sana ya kusalimia uelewa wa kweli zaidi kuhusiana na elimu ya unajimu ulikuwepo kabla kwa watu wachache waliokadiriwa hekima kabla ndivyo hivyo hivyo wapo sasa watu wengi wenye uelewa na elimu pana sana kuhusiana na Elimu au Somo la utabiri hivyo katika website hii mpya panapo majaliwa kila siku nitakuwa nakujulisha ni nini kinaendelea kinyota.

Ikiwa umekuwa umeongozwa kupitia makala hii basi ili kuweza kulifikia somo zima la unajimu unaweza kulipata kupitia link hii chini;

Https://unajimu.com

Hii ni website mpya itakayokuwa inazungumzia mambo mengi yanayohusu unajimu na vile vile matukio ya mipangilio ya nyota na sayari zake na mengi kuhusu unajimu na utabiri binafsi na wengine pia. Jambo moja la kushangaza kuhusu sayansi ya nyota ni upya wake wa mara kwa mara.  Chini ya karne nyingi wanafalsafa, mafumbo, na walimu wa kiroho wamesoma, mambo mengi na kujitahidi kutafsiri na  kusafisha elimu hii na kutafakari umuhimu wa unajimu.

Ni sayansi kongwe zaidi ulimwenguni kwa kizazi chetu wengi wao wamepoteza hifadhi zinazohusi unajimu na asilimia kubwa ya watu wamezuka na kudanganya ulimwengu kuwa ni wasomi wazuri wa unajimu na kudanganya asilimia kubwa ya watu kuhusu somo la unajimu na kuanza kuhusishwa na uchawi ama nguvu za giza hali ya kuwa ni elimu kama zilivyo elimu nyingine jipya zaidi la uchunguzi. Kulingana na Gallup kura ya maoni, asilimia 35 ya watu wazima wa Marekani wanaamini maisha yao husukumwa na nafasi ya magimba yaliyopo mbinguni. Na pia mengi ya magazeti na majarida yanayochapishwa katika nchi ya Marekani hubeba safu nzima ya unajimu huku kwa vipande vichache tu. katika nchi zingine ikiwemo Tanzania kuna uchache wa magazeti yaliwahi kuandika vipengele kuhusuUnajimu kama somo zito.

Lakini tambua ya kwamba unajimu ni somo zito linatolewa katika baadhi ya vyuo vikuu  nchini marekani na nchi zingine jirani ikiwa ni pamoja na China.
Licha ya kuongezeka kwa kasi hii mpya, hata hivyo, kwa ujumla umma una maarifa mengi tu kuhusu somo hili yaani asilimia kubwa hufahamu somo la unajimu.
Mtu wa kawaida anaweza kusema, "Ninavutiwa, na kufuatilia nyota lakini hawajui mengi kuhusu unajimu."
Moja ya shida ambazo watu hukutana nazo wakati wa kujaribu kujifunza zaidi kuhusu unajimu ni kwamba vitabu vingi vya kufundisha kuhusu unajimu hushughulikia awamu moja tu ya somo. Ukitaka kujua kuhusu ishara yako ya Jua, kuna vitabu vingi juu ya mada hii. Watu hufundishwa nyota zinazotawala tu jua. Kama wewe unataka kujua kuhusu nyota yako ya Mwezi, utapata vitabu
juu ya mada hii pia. Ikiwa unataka kujifunza kuhusu kuzaliwa kwako yaani chati yako ya kuzaliwa, itabidi utafute kitabu kingine kinachoeleza chati ya kuzaliwa na hivi ni vigumu kupata.

Sio muda mrefu uliopita, nilipokuwa nikizungumza na watu wa karibu, wakiniuliza hivi hii elimu ulijifunzia wapi? Nikawa nakumbuka jinsi nilivyokuwa nabeba mabegi na mabegi ya vitabu mfano wa mtu anaefuatilia magazeti ishirini ya kila wiki, maktaba nilizopita, walimu niliopitia, viongozi wa kidini katika kuepuka kujifunza elimu za kupotoka na vile vile watu wenye busara na kukusanya historia mbali mbali lakini matokeo yake nilijibu kwa kawaida kwamba achaneni na hilo swali majibu yake nitaliandikia kitabu. 

Mmoja kati yao alikuwa ni mwenye nyota ya Nge akauliza "Ah," alisema, "unaweza kuniambia wapi sayari yangu ipo ikiwa unasema elimu ya unajimu sio nyota peke yake nataka kujua sayari yangu? Hakujua kuwa kila mtu ana sayari kumi* katika chati yake ya kuzaliwa.

Lakini rafiki yangu angejuaje hili sidhani kama angeuliza hili swali? Unajimu mwingi wa kwenye vitabu havihusiani na chati za kuzaliwa. Isipokuwa ukitaka kujua chart yako ya kuzaliwa utakuta inakulazimu umtafute mpiga falaki ili akifanyie uchunguzi na kwa kuwa elimu hii ni elimu inayochagua baadhi ya watu tu ndio maana utakuta hata vitabu vyake vingi huuzwa kwenye maduka special ya watu wenye kutaka kujifunza mambo ya kirohohivyo utakuta elimu hii inapatikana zaidi kwenye sehemu ya maduka yanayouza vitabu vya uganga na uchawi pia maduka ya vitabu au katika maktaba maalum, ungeweza wapi kwenda kupata hizo taarifa? 

Kitabu chochote cha unajimu kitasema wewe kama nyota yako ni Mapacha au Samaki au moja ya
ishara zingine za nyota 12. Hivyo nini lengo la kukuanzishia website hii ni kwa ajili ya kujifunza mengi kuhusu nyota yako na mengi unayopaswa kujua kuhusu muongozo wako mzima wa maisha yako kinyota.

Website hii itakwambia yote unayopaswa kujua kuhusu mada nzima ya unajimu. Utajifunza kuhusu nyota za jua- na pia kuhusu za Mwezi, Nyota iliyochomoza wakati unazaliwa, Sayari, na
Nyumba(milango) ya chati yako kinyota. Utakuja kuelewa jinsi mambo haya yanavyoingiliana
kutengeneza maisha yako. Utagundua maana ya Vipengele katika usomaji wa nyota yako, na jinsi ya kulinganisha kuzaliwa kwako chati yako na ya mtu mwingine ili kufichua maeneo ya utangamano.
Utajifunza jinsi unajimu ulianza na kukuzwa. Na kama unaweza kufikia mtandao wa internet kompyuta, basi nitakuongoza vema pia jinsi ya kuchambua nyota yako kwa undani zaidi inavyoweza kukuvusha kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
ukiwa unafuatilia tovuti hii Https://unajimu.com utakuwezesha kuweka chati ya kuzaliwa ndani sekunde.
Walakini, nataka kusema neno juu ya tovuti hii utajua mengi sana kuhusu elimu ya unajimu na utaweza kufahamu mengi yanayohusu muongozo wa nyota yako siku hadi siku lakini sio tu kwamba ndio utaishia hapa na elimu hii utakuwa umeikamilisha hapana utakuwa umepiga hatua kubwa sana ya elimu hii sawa na kusema shule huanza awali hadi Masters na kuwa professor tuseme hapa utakuwa umesoma unajimu kuanzia 0 hadi chuo kikuu yatakayokuja mbele ni uchaguzi wako kama kufanyia kazi uliyojifunza ana kuyaspecialist hivyo hii wala haijumuishi hekima yote ya unajimu ambayo imegunduliwa wakati miaka 5,000 iliyopita. Hakuna kitabu kimoja au tovuti moja ingeweza
kufanya hivyo hata kama vingekuwa mara ishirini.
Website hii ni rahisi kueleweka, mwongozo wa yote kwa moja unajimu unahusu nini. Ikiwa unataka kujua wapi na kila kitu kuhusu wewe vyote hivi vipo katika sayari zako ziko kwenye chati yako ya kuzaliwa au jinsi zinavyolingana na nyota yako ya Jua iko na nyota gani ya jua ya mpenzi wako au ushawishi gani wa mwenzi uko katika maisha yako na mpenzi au mafaniko yako yapo wapi- lini utatajirika, utakuwa maarufu au la. Wapi ufanye maisha na miongozo yote, hayo yote utapata hapa katika tovuti hii moja.
Ningependa kutoa hoja moja muhimu zaidi. Unajimu hauwezi kubadilisha maisha yako ikiwa wewe hutafuata maelekezo husika na kukaa tu—ni wewe tu unaetakiwa kufuata maelekezo na busara husika za nyota yako. 

Sisi wanajimu mara nyingi huwafafanulia watu muongozo mzima wa maisha yao na matarajio ya kipi wanachofanya kitakuwa vipi. Wengi wa wanajimu ni waongo na kuahidi watu kupita kiasi ili kuwafurahisha lakini kwa mimi ni tofauti hupenda kumuweka mtu wazi ili kujua maamuzi yake na vile vile wengi wa waongo ni watu wasiojua undani kuhusu unajimu hasa ukizingatia moja ya sheria ya unajimu ni kuwa ukitabiri uongo basi utakudhuru wewe mwenyewe au kutia moyo watu kuwa tegemezi kupita kiasi. Unajimu hautabadilika heka heka za maigizo ya maisha yako. Linaloweza kufanya hivi ni

kukupa ufahamu wa jinsi ya kukabiliana na drama zako. 

Unajimu unatoa habari na mwelekeo na ubora zaidi, uhakikisho. Wakati mwingine mtu anachotafuta ni muongozo sahihi ili kuweza kufanya maamuzi sahihi zaidi,
na najua utapata miongozo mingi sana katika hii tovuti.

Nadhani umeshaamua kufuatilia tovuti hii kwa sababu una nia katika unajimu. Na natumai huu ni mwanzo tu wa uchunguzi wako. Mtu anaweza kutumia maisha yake yote kuchunguza
vipengele visivyohesabika vya mada hii inayoendelea kubadilika na kuwa mpya.

Kwa pamoja tunakaribia kuingia kwa undani zaidi katika jambo hili la kuvutia,
uwanja mpana na mgumu wa maarifa. natumai
hii inakuwa ni tovuti pekee ya unajimu utakayowahi kutaka pekee katika mahitaji yako ya nyota—pekee ambayo utawahi kuhitaji.

Wasiliana nasi kupitia:-


AU

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims
Tags

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !