Ijue nyota yako

Rakims
0

NYOTA YAKO

Katika makala hii nitakueleza kuhusu nyota yako na kabla sijaanza nitapenda ufahamu nyota ni nini?

Nyota ni Elimu ya sayansi ambayo inatumika Dunia nzima. 
Kila mtu katika Dunia akitaka asitake, aamini au asiamini atakuwa amezaliwa katika mojawapo ya nyota hizo 12.

Pia elewa ya kwamba nyota yako moja imegawanyika katika makundi mbali mbali lakini kwa makundi ya haraka nikikutajia yapo manne ambayo ni:

1: Nyota Iliyochomoza wakati unazaliwa Ascendant Sign (nyota iliyochomoza)
2: Nyota iliyochomoza tarehe na mwezi uliozaliwa Zodiac Sign yaani nyota ya jua
3: Nyota iliyochomoza wakati unazaliwa Mbalamwezi ilikuwa eneo gani (Moon Sign).
4: Nyota iliyochomoza wakati unapewa jina lako au nyota ya jina (Name Sign).

Hii ndio sababu watu wengi wanapoangalia maswali ya nyota huona ni uzushi na uongo uliopindukia lakini wanashangaa na kuona wengine zinawang'aria na kupata mafanikio kinyota kwa kuifuata vyema, kufuatilia nyota si dhambi zambi huja pale unapoileta wewe.
Na ieleweke kuwa elimu ya nyota sio kwamba ni Imani ya dini fulani hapana isipokuwa ni maarifa kama ilivyo maarifa mengine kama physics au baiolojia

Fahamu ya kwamba madaraja au mgawanyiko wa hizo sehemu nne za nyota yako ndio hutoa maelezo sahihi ya nyota yako wengi wanawalipulia watu maelezo ya nyota vibaya na kuwafanya kupoteza kabisa ladha ya nyota zao na kuona nyota ni usanii fulani wa kubahatisha kipuuzi lakini ukweli sio hivyo.

Humo humo ndani ya nyota yako ndio kuna maelekezo ya wewe ni vipi unaweza kupata kitu fulani au tukio fulani kwa kufuata muongozo upi,
ili uweze kufanikisha jambo fulani rejea hapa kujua milango (Nyumba)  12 za nyota yako.

BONYEZA HAPA KUJUA MAFANIKIO YAKO!

na pia kwenye nyota hiyo utaweza kujua mambo unayotakiwa kuyafanya kila siku au kuyapangilia ili uweze kujua vipi unaweza kufanikiwa kinyota,

Kumbuka soma mara mbili mbili kuweza kujua wengine hukuta mkang'anyiko wa mambo katika nyota zao hasa pale jina lako linaposema nyota yako ni fulani, na tarehe inasema tofauti na matendo yanaenda tofauti hapo ndio wengi huona huu ni usanii wa hali ya juu,

Karibu uweze kujua na kujifunza au kuongeza maarifa ieleweke kuwa nyota hizi sio mazao ya dini fulani hapana utaonekana usiyeelewa ikiwa utaendelea kuoanisha elimu ya unajimu na dini yoyote ile.



Nyota huwa na athari kubwa katika maisha yako hasa ukitenda kinyume na matakwa ya nyota hiyo. Mfano ukifanya biashara ambayo siyo ya nyota yako, biashara hiyo itaathirika, au ukimchukua mpenzi ambaye sio wa nyota yako bila kujua, mtapendana lakini mwisho utakuwa mbaya, au ukifanya mambo ambayo nyota yako haikubaliani nayo mambo yako yatakwama na utajiona una mikosi.

Nimeandika maelezo haya ili kuweza kuwasaidia, kufahamu undani kuhusu nyota zenu, mambo yanayohusu nyota hizo, 
Yakiwemo: 

siku yako ya bahati, 
rangi ya bahati, 
namba ya bahati, 
nani wa kushirikiana nae kimapenzi, 
kikazi, 
kibiashara, 
jiwe gani uvae, 
manukato gani yanakufaa, 
mafusho ya nyota yako, 
mambo muhimu ya kufanya, 
Kipaji chako, 
mambo ya kujiepusha nayo, 
chakula chako, 
magonjwa yako, 
mpaka nchi za kukaa kama una uwezo.

ukifuatilia vizuri na kwa makini utaweza kujiepusha na matatizo mengi sana ya kimaisha, 
Ndoa zitadumu, 
biashara zitashamiri, na Mikosi itakuondokea.

Nyota zinatambulika kutokana na tarehe yako ya kuzaliwa,muda na saa au kama hujui basi inafaa na ndio bora zaidi kupigia hesabu jina lako la kuzaliwa pamoja na mama mzazi 

kwa nini tunatumia mama mzazi? 
kwa sababu yeye ndio ana uhakika zaidi ya kwamba wewe ni mtoto wake.

Tukianza na nyota ya kwanza:

NYOTA YA PUNDA (ARIES)



Hii ni Nyota ya kwanza katika mlolongo wa Nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 Machi na 20 Aprili au wenye majina yalioanza na herufi A au M au Y au L au E.

Namba yao ya bahati ni 1 na 9.
Asili yao ni Moto, nayo ni nyota dume.
(dume ikiwa na maana ya chanya/sio jinsia za wenye nyota)

Usawa wake ni Imara
Ni nyota ya utendaji,yenye nguvu,inafaa na yenye msukumo na nyota yenye matumaini,iliyowazi katika mabadiriko na hali mpya.

Sayari yao ni Mars (Mariikh).
Marikh kwa historia za kale ni kuwa ni sayari ya Kiumbe wa vita,vurugu,uovu na ubaya.
katika elimu ya nyota hii husimama kama sayari ya hamu/shauku na upinzani huleta hisia za ajali na humiliki moto na Hatari.

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI KUHUSU NYOTA YA PUNDA:


NYOTA YA NG'OMBE (TAURUS)




Hii ni nyota ya pili katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya tarehe 20 April hadi May 20 au wenye majina yalioanza na herufi B au V au U jinsia ya nyota hii ni Jike.

Sayari yao ni Venus (Zuhura).
Siku yao ya bahati ni Ijumaa.
Namba yao ya bahati ni 6.
Rangi yao ya bahati ni kijani.
Asili ya nyota yao ni Udongo.

ngombe ni nyota yenye sifa za ukimya,upole,usikivu,usawa,ujeuri na kutokukubali kubadilika.

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI KUHUSU NYOTA YA NG'OMBE

NYOTA YA MAPACHA (GEMINI)




Hii ni nyota ya tatu katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 Mei na 20 Juni au wenye majina yalioanza na herufi C au O au K au G
Asili yao ni Upepo.Sayari yao ni Mercury (Attwarid). Siku yao ya bahati ni Jumatano na namba yao ya bahati ni 6

Malaika wake anaitwa Raphael au Mikyaail na Jini anayetawala siku ya Jumatano anaitwa, Barkaan au Ophiel, Herufi ya Jumatano ni T

Rangi zao ni Bluu, Njano, Njano ya Chungwa Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi za njano au bluu isiyoiva ambayo inapendeza ndani ya nyumba.

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI KUHUSU NYOTA YA MAPACHA

NYOTA YA KAA (CANCER)



Hii ni nyota ya nne katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 Juni hadi 22 Julai au wenye majina yalio anza na herufi D au H au P.Asili yao ni Maji,

Sayari yao ni Mwezi (Moon)
Siku yake nzuri katika wiki ni siku ya Jumatatu.
Namba yao ya bahati ni 2 na 7.
Malaika wake anaitwa Gabriel au Jibril,
Jini anayetawala Jumatatu anaitwa Murratul Abyadh au jina la utani anaitwa Abú nuuril abyadh au Phul
Madini yao ni Fedha (Silver)
Kito (Jiwe) ni Moonstone, Lulu (Pearl). Quartz, Diamond, Moonstone, Peacock Ore Manukato yao ni Yasimini (Jasmine) na Msandali (Sandalwood).

Rangi zao ni Nyeupe, Bluu, Hudhurungi (Puce) na rangi ya Fedha (Silver), Wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi zozote ambazo siyo nzito au zenye uwiano na rangi nyeupe.

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI KUHUSU NYOTA YA KAA

NYOTA YA SIMBA (LEO)



Hii ni nyota ya Tano katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Julai hadi 22 Agosti au wenye majina yalio anza na herufi E au Q au S au T.

Asili yake ni Moto. .
Sayari yake ni Jua(Sun).
Siku yake nzuri ya bahati ni siku ya Jumapili,
Namba ya bahati ni 1 na 4 .
Malaika wake anaitwa Michael au Raukayaeel
Jini anayetawala Jumapili anaitwa Abdulahi Saeed al Madhhab au Och.
Rangi zao ni rangi ya Dhahabu (Gold), Nyekundu (Red) na rangi ya Machungwa (Orange)

Watu wote wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi zilizochangamka na zenye kuonyesha utajiri kama Dhahabu na Njano nzito au iliyoiva.

Rangi zinazowapa uwezo wa Mapenzi, Mahaba na Furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Nyeusi,
ambayo hiyo mara nyingi hufaa zaidi siku ya jumamosi
Bluu iliyoiva (Indigo) na Bluu ya Samawi (Ultramarine).
ambazo pia hufaa zaidi siku ya Alhamisi.

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI KUHUSU NYOTA YA SIMBA

NYOTA YA MASHUKE (VIRGO)



Hii ni nyota ya sita kwenye mlolongo wa nyota 12 na ni ya watu waliozaliwa kati ya Tarehe 22 Agosti hadi 22 Septemba au wenye majina yalio anza na herufi F au P au T au R.

Asili yao ni Udongo.
Siku yake nzuri katika wiki ni Jumatano.
Namba yao ya bahati ni 5.Sayari yao ni Mercury (Attwarid).

Malaika wake anaitwa Raphael au Mikyaail
Jini anayetawala siku ya Jumatano anaitwa, Barkaan au Ophiel,

Rangi zao ni Rangi ya udongo, Njano na Rangi ya machungwa. Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi Nyeupe au rangi ambazo siyo nzito au zenye kuonekana sana.
Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi Bluu.

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI KUHUSU NYOTA YA MASHUKE

NYOTA YA MIZANI (LIBRA)



Hii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12,Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya tarehe 23 september hadi 22 october au wenye majina yanayoanzia na R au T.
nyota hii Usawa wake ni Dume
Hali yake ni: Thabiti
Mizani ni nyota ya utendaji,ulaini wa mambo,yenye amani,kupenda uzuri na sifa njema,kidoplomasia na yenye kung'ara katika jamii.

Sayari yako ni VENUS (ZUHURA).
sayari hii wengine huitambua kama kiumbe wa mapenzi au mtawala mapenzi:
kinyota hujulikana kama sayari inayosimamia maelewano,amani,radhi ya uraia na kukimbilia mambo yakijamii,sanaa na kupamba, lakini pia ni yenye kujishughulisha na mapenzi ya starehe.

alama yake ni mizani: ambayo humaanisha usawa,msawazo,mpangilio na haki.

PICHA YAKE:
Picha yake au muhuri wake ni mizani ambayo huwakilisha kipimo sawa cha nyota hii, hii mizani ni alama ya kale ya ki Egypt ambayo ilikuwa ikiwakilisha kipimo cha Jua, ambayo ilikuwa inawakilisha pia kipimo cha dunia mbili yani katika maana za kialama inasema kuwa mwezi kama vile umelalia mistari miwili iliyopo sawa, mstari wa juu ukiwa na maana ya hisia na wa chini ukiwa na maana ki mwenza

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI KUHUSU NYOTA YA MIZANI

NYOTA YA NGE (SCORPIO)



Hii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Oktoba na 22 Novemba au wenye majina yaliyoanza na herufi H au N au Y au S

Siku yao ya Bahati ni Jumanne, Namba yao ya bahati ni 9.Asili yao ni Maji.
Sayari yao ni Pluto.

Malaika anayetawala nyota hii anaitwa Samael au Israeel na Jini wa siku hii anaitwa Abuu Muhriz al Hammar au Phaleg

Rangi zao ni Urujuani nyekundu. Nge wanashauriwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi nzito yenye kutia shauku na kuvutia kama rangi ya damu ya mzee (Maroon).

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI KUHUSU NYOTA YA NG'E


NYOTA YA MSHALE (SAGGITARIUS)


Hii ni nyota ya tisa katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Novemba na 20 Disemba au wenye majina yalio anza na herufi I au B au D au P au U.

Asili yao ni Moto.Siku yao ya Bahati ni Alkhamisi. Namba yao ya Bahati ni 3
Sayari yao ni Jupiter (Mushtara).

Malaika wake anaitwa Sachiel au Israfeell na Jini anayetawala alkhamisi aanaitwa Shamhuurush Kadhi wa Majini au Bethor

Rangi zao ni Bluu na Bluu iliyokolea. Wenye nyota hii wanatakiwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara rangi zenye kusisimua na uchangamfu na zinazoashiria hali ya kumkaribisha mgeni. Rangi hizo ni Nyekundu iliyochangamka (Warm Red) rangi ya Zambarau (Purple) na rangi ya hudhurungi au kahawia (Brown).

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI KUHUSU NYOTA YA MSHALE

NYOTA YA MBUZI (CAPRICORN)



Hii ni nyota ya kumi katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 Disemba na 19 Januari au wenye majina yalio anza na herufi J au V au K.

Asili yao ni Udongo.Siku yao ya bahati ni Jumamosi. Namba yao ya bahati ni 8
Sayari yao ni Saturn (Zohal).

Malaika wake anaitwa Cassiel au Kafyaeel, na Jini anayetawala Jumamosi anaitwa, Abuu Nuhu au Aratron.

Rangi zao ni Nyeusi na Bluu iliyoiva. Wenye nyota hii wanashauriwa wapake rangi zifuatazo kwenye nyumba zao, rangi ya Kahawia (Brown) Rangi ya Kijivu (Grey) au Nyeusi (Black).

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Hudhurungi (Puce) na Fedha (Silver).
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Rangi ya Samawi (Ultramarine).

Kito (Jiwe) ni Black Onyx. Madini yao ni Risasi (Lead).

Manukato yao ni yale yatokanayo na Msonobari (Pine), Maua yanayofanana na ya Jamii ya Choroko, Njegere au Dengu (Sweet pea) na Magnolia.




Hii ni nyota ya kumi na moja katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 20 Januari na Februari 18 au wenye majina yalio anza na herufi K au W au G au S.

Asili yao ni Upepo.Sayari yao ni Uranus. Siku yao ya bahati ni Jumamosi. Namba yao ya bahati ni 8

Malaika wake anaitwa Cassiel au Kafyaeel, na Jini anayetawala Jumamosi anaitwa, Abuu Nuhu au Aratron.

Rangi zao ni Bluu, Kijivu na Samawi ya Bluu (Ultramarine blue). Wenye nyota ya Ndoo wanatakiwa wapake nyumba zao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi zilizotulia kama Bluu au Kijivu.

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Dhahabu na Machungwa.
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Aqua.
Kito (Jiwe) ni Lulu Nyeusi, Obsidian, Opali (Opal) na Johari (Sapphire).
Madini yao ni Risasi (Lead).
Manukato yao ni yale yatokanayo na Mgadenia (Gardenia) na Azalea.

BONYEZA HAPA KUISOMA ZAIDI KUHUSU NYOTA YA NDOO

NYOTA YA SAMAKI (PISCES)



Hii ni nyota ya 12 katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 19 Februari na Machi 20 au wenye majina yalio anza na herufi L na X au D na C au J.

Asili yao ni Maji.Sayari yao ni Neptune.Siku yao ya Bahati ni Alhamisi, Namba yao ya Bahati ni 8,

Malaika wake anaitwa Sachiel au Israfeell na Jini anayetawala Jumapili aanaitwa Shamhuurush Kadhi wa Majini au Bethor

Rangi zao ni Bluu iliyochanganyika na Kijani na Aqua. Rangi zinazowapa uwezo wa Mapenzi, Mahaba na Furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Udongo, Njano na Njano-machungwa.

BONYEZA HAPA KUISOMA ZAIDI KUHUSU NYOTA YA SAMAKI

Hizo ndizo nyota 12 na maelekezo yake mengi nitaendelea kuongeza maelekezo mengine
ifahamike nyota hizi hazihisiani na dini yoyote na kama mtu anadai Nyota ni tabia ya dini fulani basi kaachwa nyuma kwa maarifa ni vitu haviendani.

kama una swali au swala ambalo ni binafsi:

Wasiliana nasi kupitia:


AU

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims
Tags

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !