Nyota ya Nge (Scorpio)

Rakims

Nyota ya Nge (Scorpio)

Hii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Oktoba na 22 Novemba au wenye majina yaliyoanza na herufi H au N au Y au S.

Siku yao ya Bahati ni Jumanne, Namba yao ya bahati ni 9. Asili yao ni Maji. Sayari yao ni Pluto.

Malaika anayetawala nyota hii anaitwa Samael au Israeel na Jini wa siku hii anaitwa Abuu Muhriz al Hammar au Phaleg.

Rangi zao ni Urujuani nyekundu. Nge wanashauriwa wapake nyumba zao, vyumba vyao, magari yao au sehemu zao za biashara rangi nzito zenye kutia shauku kama Maroon.

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni Kijani. Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Bluu.

(SCORPIO)

Nyota ya Nge (Scorpio)

Kito (Jiwe) ni Topaz, Bloodstone, Malachite, Ruby, Rhodochrosite, Kunzite, Moldavite, Opal, Diamond, Selenite, Quartz. Madini yao ni Chuma, Radiamu (Radium) na Chuma cha pua (Steel). Manukato yao ni ya Msandali (Sandalwood), Tikiti maji (Watermelon), Nazi (Coconut), na Mcheri (Cherry Blossom).

MAMBO MUHIMU

Sifa ya Nyota hii ni Kuwa Imara.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni uwezo wa kuangalia na kujua mambo kwa upana zaidi.

Maadili yao: Utiifu, Kuwa Imara, Kuazimia jambo, Ujasiri na Undani.

Matakwa yao: Kuingilia undani wa kitu na kukibadilisha.

Tabia za kujiepusha nazo: Wivu, Kulipiza kisasi, Kutokubali kusamehe, Kubishana na kung’ang’ania mambo.

USHIRIKIANE NA NANI

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Kaa na Samaki.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Ng’ombe, Simba na Ndoo.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Simba.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Ndoo.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mshale.

Nyota inayomsaidia katika Ubunifu ni nyota ya Samaki.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Ng’ombe.

Nyota bora ya Kujifurahisha ni nyota ya Samaki.

Nyota zinazomsadia kiroho ni nyota za Kaa na Mizani.

KIPAJI CHA NGE

Nge wana kipaji na uwezo wa kiroho wa kuwasiliana na watu katika kutekeleza mambo wanayohitaji. (Mystical)

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI

Nge wana uwezo mkubwa wa kuvutia watu, ni jasiri na wepesi kuelewa mambo. Wana tabia ya kutilia mkazo mambo yao na hata kutumia ukali ili kufanikisha malengo yao.

Ni wasiri, wanaopenda kufanya mambo yao kisiri na hawaogopi giza. Wana akili nyingi na kipaji cha asili cha kutimiza malengo.

Wakati mwingine wanaweza kujidhuru wenyewe wanapokutana na changamoto kubwa. Wanapenda kutumia mapenzi na tendo la ndoa kama njia ya kuonyesha ujasiri wao. Kwao mapenzi ni sehemu muhimu ya maisha kwa kuwa nyota ya Nge inatawala sehemu za siri.

Ni wenye ashki kubwa, hasira wanapoumizwa na mara nyingi hasira hizo huisha baada ya tendo la ndoa. Wana tabia ya usiri kwenye mapenzi ili waweze kupata wapenzi wengi na kukidhi kiu yao ya ngono.

KAZI NA BIASHARA ZA NGE

Nge ni watu makini na wenye ushupavu katika kazi. Wanafanya kazi kwa bidii kuhakikisha malengo yao yanatimia. Wana akili na heshima kwa wenzao.

Kazi zinazowafaa: tiba na madawa, upelelezi, utafiti, ufundi bomba, elimu ya kale, ushauri wa mapenzi na biashara zinazohusiana na ngono.

MAVAZI NA MITINDO

Nge wanashauriwa wavae mavazi maridadi yenye rangi ang’avu. Mavazi yao yawe katika hali ya suti, rangi nyekundu, mashati au skafu nyekundu. Vitambaa vinafaa: sufi, fulana au vinavyomeremeta. Wanawake wavae suruali, wanaume wavae mavazi yenye nakshi ya kujiamini.

MAGONJWA YA NGE

Nyota hii inatawala: kifuko cha mkojo, uume, uke, coccyx, mlango wa kizazi na sehemu ya haja kubwa. Pia mfumo wa mkojo na tezi kibofu.

Matatizo makubwa: kansa ya tezi kibofu, kuziba mkojo, magonjwa ya damu ya kike na mabusha. Mara nyingi matatizo haya husababishwa na tabia yao ya kuzoea mambo ya mapenzi kupita kiasi.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA NGE

Vyakula vinavyowafaa: mananasi, vitunguu vibichi na vilivyopikwa, nyama ya kondoo mchanga na vyakula vyenye viungo vikali.

Miji na nchi zinazowafaa: Liverpool (Uingereza), New Orleans (Marekani), Poland na Switzerland.

MADINI, VITO NA MAFUSHO

Madini ya Nge ni Chuma. Vito vyao: Topaz, Ruby, Bloodstone, Malachite n.k. Mafusho ya Nge ni Qist, unachomwa Jumanne kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

FUNGUO

Funguo ya nyota ya Nge ni "Natamani" — wakitamani kitu kwa dhati hukipata.

Wasiliana nasi

Email: Rakimsspiritual@gmail.com

WhatsApp: +255 783 930 601

Rakims Spiritual

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !