Nyota ya Mizani (Libra)

Hii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya tarehe 23 Septemba hadi 22 Oktoba au wenye majina yanayoanzia na R au T.
Usawa wake ni Dume. Hali yake ni Thabiti. Mizani ni nyota ya utendaji, ulaini wa mambo, amani, upendo wa uzuri, diplomasia na kung’ara katika jamii.
Sayari yao ni VENUS (ZUHURA) — sayari ya mapenzi, maelewano, furaha, sanaa na mapambo.
PICHA YAKE
Alama yake ni mizani ambayo humaanisha usawa, msawazo, mpangilio na haki. Mizani hii ni alama ya kale ya Misri ikiwakilisha kipimo cha Jua na dunia mbili.
Siku ya Bahati: Ijumaa. Namba za Bahati: 6 na 9. Malaika: Anyail. Jini: Zawbat. Shetani: Succubi (jini mahaba).
MANUKATO NA RANGI ZA BAHATI
Manukato: marashi yenye mauwaridi yenye harufu laini isiyokera.
Rangi: Kijani isiyoiva, Bluu na Lavender. Rangi hizi huwafaa kwa mapenzi, furaha na urafiki.
Asili ya nyota hii ni UPEPO.
KIPAJI CHA MIZANI
(Extra Sensory Perception) — Wenye nyota hii wana kipaji cha kufumbua siri na kumjua mtu kabla hajajieleza.
TABIA ZA MIZANI
Ni wapenda usuluhishi, amani na upatanishi. Watiifu, wasikivu na wepesi kuongozwa. Wanawake wa Mizani mara nyingi huwa na maumbo mazuri. Ni wakarimu, wenye adabu na wenye kupenda mapenzi na mahaba.
TABIA YA MIZANI KATIKA MAPENZI
Wanapenda kuhusiana kimapenzi na mara nyingi hupumbazwa na mapenzi. Huchukua muda mrefu kufanya maamuzi kuhusu wapenzi na mara nyingine huingia kwenye ndoa mapema bila kuangalia. Wanaamini bora ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.
Ni mabingwa wa Romance na Sex. Wanapenda kutoa maneno matamu, zawadi na kumridhisha mpenzi kitandani.
MAMBO MENGINE
Ni rahisi kupendeka na huvutia kwa tabasamu na maneno yao. Wana nyumba zilizopambwa vizuri na hupenda starehe zinazohusiana na pesa. Hawapendi kutembea peke yao, hupenda kuwa na mwenza kila mahali.
USHIRIKIANE NA NANI
Nyota bora ya ndoa: Punda.
Nyota zinazofaa: Mapacha na Mshale.
Nyota zisizofaa: Ng’ombe, Mashuke na Mbuzi.
Nyota inayosaidia kikazi: Mapacha.
Nyota inayosaidia kipesa: Mshale.
Nyota inayosaidia ubunifu: Mapacha.
Nyota bora ya kujifurahisha: Punda.
Nyota zinazosaidia kiroho: Mshale na Samaki.
MITIZAMO YA WATU
Huonekana kuwa watu muhimu katika familia na jamii, lakini wakati mwingine hukosolewa kwa ujuaji au kung’ang’ania mitizamo yao.
MAGONJWA YA MIZANI
Husumbuliwa na matatizo ya mgongo (hasa karibu na makalio), figo na maungio ya kiuno.
MADINI, WANYAMA, VITO
Madini: Copper. Wanyama: Nyoka na Mijuzi. Kito: Opal — huletea mafanikio ya kifedha, huzuia wivu na tamaa na kuongeza ufahamu.
MAFUSHO
Ubani Mashtaka — una rangi ya kijivu, mgumu na unapukutika unga mweupe.
KAZI NA BIASHARA
Kazi zinazowafaa: Ushauri wa Ndoa, Urembo, Uanasheria, Uhakimu, Biashara ya Sanaa, Pancha na mapambo ya harusi. Ni washiriki wazuri na huchangia kikamilifu kwenye kazi za pamoja.
MAUA
Maua yanayofaa: Uwaridi — huendana na nyota hii ya mapenzi.
UHUSIANO WA KIMAPENZI
(Punda na Mizani) — Punda hupendezwa na diplomasia ya Mizani, wakati Mizani hupendeza kwa kipaji cha mahaba.
HATARI ZA MIZANI
Ni rahisi sana kujirahisisha kimapenzi na huweza kusaliti au kutokua waaminifu, jambo linaloweza kuvunja moyo wa wapenzi wao.
FUNGUO
Funguo ya Mizani ni "Ninalinganisha" — akijilinganisha na kitu au mtu, basi humpata kwa kufikiria hivyo moyoni.
Wasiliana nasi
Email: Rakimsspiritual@gmail.com
Email ya pili: mnajimu@unajimu.com
WhatsApp: +255 783 930 601
Tovuti: unajimu.com | rakimsspiritual.com
Rakims Spiritual