Nyota ya Samaki (Pisces)

Rakims
0

 NYOTA YA SAMAKI (Pisces)


Hii ni nyota ya 12 katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 19 Februari na Machi 20 au wenye majina yalio anza na herufi L na X au D na C au J.

Asili yao ni Maji.Sayari yao ni Neptune.Siku yao ya Bahati ni Alhamisi, Namba yao ya Bahati ni 8,

Malaika wake anaitwa Sachiel au Israfeell na Jini anayetawala Jumapili aanaitwa Shamhuurush Kadhi wa Majini au Bethor

Rangi zao ni Bluu iliyochanganyika na Kijani na Aqua. Rangi zinazowapa uwezo wa Mapenzi, Mahaba na Furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Udongo, Njano na Njano-machungwa.

Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Nyekundu. Wenye nyota ya Samaki wanatakiwa wapake nyumba zao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi ambayo haijakoza ya Bluu au Kijani au Urujuani (violet).

Kito (Jiwe) ni Almasi Nyeupe. Madini yao ni Bati. Manukato yao ni Yungiyungi (Lotus).

MAMBO MUHIMU:-
Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye uwezo wa kushikilia muundo na hali.

Maadili yao ni Uwezo mkubwa wa Kuhisi, Kujitoa Mhanga, Kuishi na Kutenda kwa ajili ya Manufaa ya Wengine, Uungwana, Utu, Ubinadamu, na Ubingwa wa Maono.

Matakwa yao ni Mwanga wa Kiroho, Uhuru na Haki ya kujiamulia la kufanya.

Tabia za kujiepusha nazo ni Tabia ya Ukwepaji wa Matatizo na mambo, Kununa, Kususa, Kunung’unika pasipokuwa na sababu ya Msingi, na Kuwa na Marafiki Wabaya.

USHIRIKIANE NA NANI?
Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Kaa na Nge.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Mapacha, Mashuke na Mshale.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mshale.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Mapacha.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Punda.

Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Kaa.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Mashuke.

Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Kaa.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Nge na Ndoo.

Siku yake nzuri katika wiki ni siku ya Alhamisi.

KIPAJI CHA SAMAKI:
Samaki wana wana kipaji cha kufikiria jambo na kuliunda na likawa vile walivyotaka wao visionary.

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Watu wenye nyota ya Samaki ni wenye huruma, wapole na wenye moyo mzuri, hawawezi kukubali kumuona binaadamu mwingine akipata taabu au uchungu. Kwa hakika ni watu ambao wana hisia kali kwa wengine, hawajipendelei na wako tayari wakati wowote kujitoa mhanga ili watu wanufaike, mapenzi yao au huruma kwa binaadamu wengine hayana masharti yeyote.

Nafsi zao zimegawanyika katika nafsi ndogo ndogo kama vile muathiriwa mwenye kujitoa mhanga, mwokozi, na mkombozi.
Hayo yote yaliyotajwa wanaweza kuyatekeleza inapohitajiwa na akishatumbukia katika moja ya mambo hayo huwezi kumtoa.

Kwa ujumla nafsi za Samaki siyo za kidunia, ni watu wabunifu na wenye ndoto za kufikiri mambo ya baadaye na katika maisha yao, wanaona raha sana kuwa na mawazo ambayo yatawaepusha na ugumu wa maisha.

Ikiwa wamekwama katika jambo lolote basi wataitafuta faraja au watajituliza kwa ulimwengu wao wa mawazo. Samaki ni wenye kukamilika na Mahaba mengi na wanapenda sana kujitumbukiza na kuzama kwenye dimbwi la mapenzi.

Kuwa katika mapenzi ni kitu wanachokipenda na kukifurahia sana. Ni waangalifu wazuri kwa wapenzi wao wana huruma nyingi.
Wana hisia kali za kimapenzi na ni wepesi kuathirika.

Mara nyingi huwa waoga wa vitu vya kimapenzi kwa sababu ya kuogopa kuvurugika kwa mipango yao ya baadaye.
Samaki huyachukulia mapenzi kama ua la waridi na wanawaona wapenzi wao kama binaadamu wasio wa kawaida.

Tatizo lao kubwa la kimapenzi ni kwamba wanawaamini sana wapenzi wao na wanakuwa na mawazo au firika za kimapenzi ambazo hazipo katika dunia hii.

Kwa ujumla wenye nyota hii wanapokuwa katika mapenzi wanakuwa wamejawa na shauku na mifano ya kuvutia na wanapenda wapenzi wao waishi kiroho. Mategemeo yao yanakuwa makubwa na yasipotimia huwa wanavunjika moyo.

KAZI NA BIASHARA ZA SAMAKI:
Kugundua muelekeo wa kimaisha kwa Samaki wakati mwingine huwa ni matatizo.
Tabia yao ya kushughulikia sana binaadamu wengine huwafanya wasiwe na muelekeo.

Wanatakiwa wafanye kazi ambazo zinazohusiana na kusaidia watu. Kipaji cha kutafsiri mambo, huwasaidia vile vile kufanya kazi za sanaa kama vile kupiga picha na kazi za muziki au maigizo.

Kazi zingine zinazowafaa ni za kuhudumia wagonjwa, kucheza shoo, uaskari wa majini (Navy) kazi za dini au kazi za kutoa ushauri nasaha (Counselling).

MAVAZI NA MITINDO:
Samaki wanatakiwa wavae nguo za michezo kama vile fulana au za kiasili na zilizoongezwa madoido na vimbwanga vingi.Nguo zao ziwe za rangi ya Zambarau au Kahawia iliyochangamka na rangi ya bluu.Kitambaa kiwe cha sufi (tweed) Wanawake wapendelee sana kuvaa sketi, ikiambatana na mikanda na viatu vyao viwe vya buti.

MAGONJWA YA SAMAKI:
Nyota hii inatawala nyayo na vidole vya miguu. Matatizo yao ya kiafya yanakuja pale wanaposhindwa kutekeleza ndoto zao au mipangilio yao kimaisha au wanapokorofishana na wapenzi wao.
Wanapoathirika na hayo yaliyotajwa hukimbilia kwenye ulevi na utumiaji vidonge uliokithiri.

Tatizo lingine ni maradhi ya nyayo za miguu, uvimbe unaotokana na baridi kali hasa katika vidole vya miguu.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA SAMAKI:
Samaki wanashauriwa wapende kula matunda au vyakula vifuatavyo.
Matunda ya Kunazi, Nyama mwitu kama Swala, Nyati na kadhalika.Vile vile wapendelee kula Maboga.

Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota yao.

Nchi hizo ni Tonga na Tanzania na miji ni Alexandria (Misri) na Seville (Ufaransa).

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Samaki ni Platnum ikiwa ngumu kupata tumia Bati (Tin). Vito vyao vya kuvaa katika pete ni Aquamarine
Mafusho ya Samaki ni Udi Kafur. unachoma siku ya Alkhamisi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

FUNGUO:
Funguo ya samaki ni "Naamini" wao pale wanapokua na imani juu ya jambo basi hufanikiwa nalo mwisho wa siku,

Wasiliana nasi

Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia email lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.

Unaweza kutupata kwa kupitia Email, vile vile kwa namba za simu, kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,

Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.

Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na RakimsSpiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.

Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa Members pekee;

Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia:-


Rakimsspiritual@gmail.com


au


mnajimu@unajimu.com


WhatsApp number


+255 783 930 601


Rakims

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !