Ifahamu Cosmic energy ni nini? | Nguvu ya roho

Rakims
0

 Vipindi katika vipindi vilivyopita niliwaahidi kwamba mkifika subscriber elfu 1 nitafundisha kuhusu Cosmic energy hivyo katika video hii nitakufundisheni mambo yafuatayo: 

  • ni nini cosmic energy? 
  • ina kazi gani? 
  • ina faida gani? 
  • ina msaada gani kwa mtu mwenye kuipokea? 
  • kwa nini huitwa zawadi katika zawadi za meditation ambazo mtu akipokea hupanda rank yake kutoka sehemu moja kwenda nyingine?

Kwa kuanza:

Cosmic energy ni nini?

Kwanza kabisa fahamu ya kwamba ubongo wako kazi yake sio pekee ya kutengeneza na kufikiria peke yake lakini pia kazi yake ni kupokea yaani hufanya kazi kama receiver vile vile.

 Inategemea na unazungusha mawimbi wapi nao utapokea maelezo vema. Mathalani tunapokuja kwenye maelezo ya Cosmic Energy. 

Kwanza kabisa fahamu ya kwamba cosmic energy, ni nguvu ambayo ipo kila sehemu ambapo yupo mwanadamu yaani kwa kiswahili rahisi ni nguvu ya roho ambayo ipo kila sehemu waliokufuru huita Mungu. 

Lakini walioshukuru huita malaika wa Mungu ama betri za roho, 

Roho yako ni sawa na simu iliyoishiwa charge muda mwingine hujicharge automatic lakini muda mwingine inategemea wewe mwenyewe unataka iwe na charge kwa asilimia ngapi.

Cosmic energy ni nguvu ambayo ipo kila sehemu aliyopo mwanadamu ambayo inamfanya atambue na ajue ya kwamba kila kitu kimeungana. 

Na vyote huenda kwa hesabu na pia kwa mizani sawa na yeye anaweza kuwa ama kufika ama kusikia chochote pale pale alipo ikiwa atakuwa na maarifa.

Kila kitu kimeunganika na kimeungana yaani wewe, dunia, galaxy na kila kitu.

Jinsi tunavyoishi maisha yetu ya kila siku ni  kutokana na haja na uthubutu tulionao na kile tulichopangiwa kwa mizani yake mwenyewe Roho ya kwanza ama chanzo cha roho,

Mara nyingi na watu wengi hupokea nguvu hizi kwa kupitia fikra yaani pale fikra chanya inapokuijia ya kufanya mabadiriko ya maisha yako ama watu wengine au mazungira yako kuwa vizuri basi huwa ni kama redio yenye kupokea transmition kutoka kwenye roho iliyo takasika ama zilizo takatika.

watu wengi hawatambui hili pale ambapo nguvu hii inapowashukia na mara nyingi watu wenye imani husema nimeongozwa na roho takatifu katika kufanya hili  lakini pia wapigaji nao hudanganya watu kwa kusema hivyo na kinachobaki kwao ni kujideceive wenyewe tu.

Kuna ishara tofauti tofauti kwamba muda huo wewe unapokea cosmic energy katika maisha yako ambapo ya kwanza ni 

1: Msukumo wa ghafla 

Ndio unapokukuta msukumo wa ghafla na ambao ni chanya wa kukusukuma ufanye kitu ama kuanza jambo na unajikuta unatamani ama kulipenda katika roho yako yaani kabla hujafanya unaanza kusikia raha rohoni. 

Ambapo hii unakuta moja kwa moja inakuongoza kurudi katika makusudio ama sababu ya wewe kuwa hapa duniani.

2: Ndoto

Hii ni kutokana na baadhi ya watu waliotangulia kabla yetu na mafunzo ya dini na mitume kufundisha kwamba Watu wengi hujicharge automatic yaani ile iliyokadiriwa pale tu wanapoingia kulala usiku 

maana kiimani usingizi ni nusu ya kifo yaani ukiingia kulala roho hutoka na kwenda anapopataka Mwenyezi Mungu haya mafunzo yapo kidini pia.

Ndio maana pale unapolala unaweza kupokea ujumbe kutoka katika mwili na roho yako. vile vile kuwa na ndoto ambazo kwa hakika hukuwahi kujua kabla mfano taarifa ama maarifa ya kitu mwanzo wa maarifa ya wengi ni kupitia mawazo na ndoto.

3: Subconscious mind

Hii hutokea hata wakati wa kuangalia video au movie kisha inakupa majibu ambayo ulikuwa unajiuliza yaani kama vile wale characters wanakuwa wanakupa taarifa ya jambo ambalo unajiuliza muda mrefu kisha unakuwa umepata majibu pale.

Ama  kuskia mziki ukiwa umebeba ujumbe ambao ulikuwa unataka kuusikia yaani ukisikiliza huo wimbo unasikia imani inapanda ama mlio ama ayah ama vifungu vya biblia.

Tena inakuwa inarelate na swali ambalo ulikuwa unajiuliza sana hupati majibu mfano mimi nitatajirika vipi kisha majibu yanafunguka pale pale na hii ni kutokana na roho zinakuwa zinaongea na wewe kupitia subconcious mind kukwambia purpose yako ni ipi ya kufanya,

4: Kuvutia kuelekea wazo  moja

Unaweza kujikuta kila unachofanya labda unaangalia movie na marafiki unakua na wazo limekuganda linakuvuta ulifanyie kazi, ukikaa unakuwa una waza hilo hilo jambo moja tu kutaka kulifanya

basi hii ni cosmic energy inajaribu kukupa taarifa kwamba unachelewa muda wa kuanza.

5: Hesabu takatifu

Kuna usemi usemao katika hesabu za fizikia kwamba hesabu ni lugha ya ulimwengu yaani ukitaka kuongea na ulimwengu mzima basi piga hesabu ambapo kuna maomba ya dunia na ulimwengu na mwili wa mwanadamu ambayo yana ujumbe mkubwa sana kwake akiamua kusikiliza, 

Ikiwa kuna umbile linakuijia mara kwa mara ama kuna picha unapenda kuitizama mara kwa mara ama eneo basi fahamu ya kuwa kuna ujumbe kwenye hilo hivyo wekeza hapo utapata purpose yako, kama utaona namba, umbo chochote kinachokuijia mawazoni pasipo wewe kukitaka basi kifanyie kazi.

6: Kuongezeka kwa hisia

Mara nyingi cosmic energy pia humtembelea mtu pale anapokuwa na hisia kali na ghafla hisia hizo zinakata na anaanza kuhisi jambo lingine la ghafla lenye kumliwaza na kumpa picha kamili kwenye akili. Huo huwa ni ujumbe kutoka kwenye cosmic energy

7: Kujihisi unapenda bila sababu 

Muda mwingine mtu humuingia upendo usiokuwa na sababu na kuanza kujihisi kupenda mazingira na watu wanaomzunguka, 

Kama ghafla tu kujiona umependa mtoto ama muonekano wa mtu mzima na kujihisi kutaka kumsaidia kujihisi unapenda kila mtu na kila kitu bila sababu nayo hutokea kwa muda mfupi. 

Hii ni alama kuwa kwa muda huo unakuwa unapokea cosmic energy na kama unaijua basi utakuta mtu hazubai na anaanza kujitahidi kukaa na kupokea zaidi na zaidi ukiinuka hapo wewe ni mtu mwingine

Shida hii huwa inatokea ghafla na mtu unakuwa hujajiandaa unakuja kushtuka ghafla siku imepita nyingine na unabaki unashangaa nini kilipelekea jana yake ulikuwa na roho nzuri kupitiliza na furaha isiyo na kifani bila sababu. 

Wasiliana nasi

Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia email lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.

Unaweza kutupata kwa kupitia Email, vile vile kwa namba za simu, kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,

Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.

Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na RakimsSpiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.

Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa Members pekee;

Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia:-


Rakimsspiritual@gmail.com

au

mnajimu@unajimu.com


WhatsApp number


+255 783 930 601


Rakims
Tags

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !