Mahusiano kinyota Simba na Mashuke (leo and Virgo)

Rakims
0

Mtizamo wako kwake 

Wewe ni mwenye kuvutiwa zaidi na jinsi yeye alivyo kwa upande wa kiakili, lakini yeye utakuta hakuelewi wewe na kukuona ni mtu mwenye asili ya drama, 

Utashindwa kuelewa mahitaji yake kimwili kwa jinsi anavyokuwa kajiweka na kwenye tendo utakosa kuvutiwa nae kwa jinsi ufanyaji wake ulivyo utaona ni kichefu chefu.

Yeye anakuwa ni mtu mwenye kutaka vitendo na busara,  Wakati wewe utakuta ni mwenye ubadhilifu na kupenda kutumia.

Yeye utakuta  ni mwenye ubahiri hata wa nafsi yake mwenyewe. wewe utakuta ni mwenye kupenda kujiachia yeye utakuta ni mwenye kukubana bana kiasi kwamba muda wote hata kama hayupo utahisi kakubana tu.

Utaona ni mtu mkorofi, mwenye ujuaji mwingi na hata ukiongea nae utaona ni mtu mwenye kutaka kukutangulia na kujiweka msafi sana...

Hali ya kuwa wewe uhuru ni jambo la kwanza kabisa ambalo wewe unapenda. Wewe utataka hadhi yako iangazwe lakini kwa huyu atakufanya ujihisi kama mtoto kwa mama yake jambo ambalo kwako utaona ni upuuzi..

Kila kitu atataka kukupangia na kukupelekesha na yeye hata taka wewe umwambie kitu. Halafu ni mtu ambaye kitu kidogo tu anakuwekea Gubu huta jihisi amani wala furaha ya kutosha 

Ni bora tu uangalia ustaarabu pengine kwa hapa unatafuta majuto....

Hata ukiwa nae utaanza kuporomoka kiuchumi.

Mtizamo wake kwako

 Mahusiano haya ni ya watu wawili wasioendana sana hasa ukizingatia tabia ya majivuno na kujiona ya yeye ni machukio kwako na utajikuta hupendezewi na kutaka kwake kutukuzwa kwa kila jambo.

Wewe ni mwenye kujithamini na kujiwekea uzio na ubinafsi wenye manufaa yako binafsi utakuta ni fedheha kubwa kwake yeye mwenye kupenda kuwa juu na kutukuzwa pia ukimuignore kidogo tu hata akiwa anaongea basi gubu lake huta kuja kuamini.

Wewe ni mtu ambaye huna uwezo wa kulea mtu ambaye ni mwenye utukufu wa ndani ya roho yake.

Yes, yeye ni mtu mwenye ukubwa ndani ya roho yake yaani ana asili ya malikia kama ni mwanamke na kama ni mwanaume basi ana asili ya kifalme roho yake ni tajiri na sio tajiri wa kawaida ni tajiri fahari, kabla ya kuondokewa na uhai anatarajiwa kuwa tajiri. 

Hivyo kwa wewe ambaye wakati huna hujulikani na wakati unachohujulikani itakuwa ngumu kuishi na falme hii maarufu.

Pia wewe huwezi kumfikia hadhi yake jinsi alivyojiweka hata kama mkikaa nae utaona anakuzidi mengi na vile vile wewe sio mtu wa kutoa sifa kwake yaani kumsifu sifu na yeye hakuna kitu kinamtia nyege kama kusifiwa ukimsifu sifu basi utaona unamlainisha kila kukicha lakini mtu akikwambua jua zamani lilikuwa linachomoza mashariki na kuzama magharibi siku hizi linazama mashariki kubali ila tabia ya mtu huwa haibadiriki.

Ndivyo hivyo hivyo kwako utaushi maisha ya maigizo hadi lini ipo siku gari itawakia namba 5 hapo hapo kila mtu ataangalia uelekeo wake.

 Wote wawili ni wenye kujitegemea sana, sio wenye kupenda kutegemea watu

lakini yeye anaonyesha hii kwa njia ya hasira, yaani kujitegemea kwake au maendeleo yake utaona anatumia pesa nyingi hata kwa vitu visivyo na faida yeye haoni hasara kuwa fahari yupo radhi anunue kitu cha thamani kubwa au afanye jambo kubwa pasipo kujali atalala njaa.

wewe ni mchumi na mwenye kujibana sana. 

Hivyo yeye hapendi watu wa hivyo na vile vile utakuwa unampotezea muda kama yeye anashindwa kukwambia mimi nakwambia yaliyopo kwake linapokuja katika suala la matumizi hakuna anachokuelewa sawa na kupigia mbuzi gitar labda akuskilize tu kisha akitoka hapo vimeyayuka ana roho ya kitajiri na ukimvumilia mtakuwa matajiri baadae.

Mahusiano yenu ni mafupi sana kuliko uhai wa mayfly.

Wasiliana nasi

Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia email lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.

Unaweza kutupata kwa kupitia Email, nambari za simu,kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,

Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.

Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na rakimsspiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.

Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa members pekee; 

Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia


Email: Rakimsspiritual@gmail.com

WhatsApp: +255 783 930 601

Rakims

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !