Mahusiano kinyota Ndoo na Mbuzi (Aquarius and Capricorn )

Rakims
0
Katika mahusiano haya mnaonekana ni wawili msioendana hasa ukizingatia kwamba yeye ni mchanga wa bahari na wewe ni Upepo wa kimbunga;

Unaonaje dhoruba ikitokea kando ya bahari?

Hayo ndio mahusiano yenu yalivyo mkiunganisha roho,

yeye atajikuta anakuona wewe ni mtu usiyeweza kumtabiri, na wewe utajikuta ni mtu ambaye unashindwa kwenda na yeye kirahisi hadi utumie nguvu nyingi

Mbinu zake za kawaida tu za kukuendea hata katika kuomba mchezo utakuta kwake ni kero kubwa sana na atakuona kama vile muda wote wewe ni mwenye kumtibua tu mwanzoni utaona kama anakuvumilia lakini baadae sura kamili ya dhoruba itaonekana.

wewe hujiamini katika kujieleza kimtizamo wako bila maneno.




Na yeye hujiamini katika kujiheshimu bila mipaka, mawasiliano yenu kila mmoja atajikuta haeleweki kwa mwenzie na pia ataona kama anaaibika na kudhalilika kwa mwenzie.

wewe utakuta ni mtu wa kupenda mitoko na yeye utakuta ni mtu wa kupenda mtu mwenye kumaintain maisha ya nyumbani wewe ni mtu mtafutaji yeye atafurahishwa kwa utafutaji wako mwanzo kwa kufuata mkumbo lakini baadae itakuwa too much hata kama utamletea maigizo sasa hivi lakini baadae visafari vya kwa ndugu jamaa na marafiki huwa havikatiki.

wewe vile ni mpenda uhuru, safari ya mapenzi yenu itakuwa ngumu sana na uvumilivu wako kwake ni mdogo wewe unataka mtu mwenye nyota ya moto wa mkaa ambaye wewe ukimletea habari za kutoka unakuwa kama umemtia hamasa.

Hakika wewe ni mwenye kupenda kutoka sasa akitaka kukufunga funga kwa maisha yake ya siasa kimbunga kitazunguka kisha vumbi lako litapeperuka na kubaki umemvuruga.

Nyie mnapendeza zaidi kuwa ni wenye urafiki tu na hata mapenzi yenu mara nyingi huishia kirafiki tu.

Wasiliana nasi

Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia email lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.

Unaweza kutupata kwa kupitia Email, vile vile kwa namba za simu, kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,

Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.

Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na RakimsSpiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.

Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa Members pekee;

Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia:-


Rakimsspiritual@gmail.com

au

mnajimu@unajimu.com


WhatsApp number


+255 783 930 601


Rakims

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !