Mahusiano nyota ya Samaki na Ng'ombe (Pisces and Taurus)

Rakims

SAMAKI NA NG'OMBE


Pisces and Taurus

(Utangamano)

Mahusiano haya yeye anaonekana ni mwenye nguvu, mamlaka na mwenye uwezzo wa kutoa usalama kwako ambaye mara nyingi unakuwa na asili ya kuyumba yumba, Pia yeye ni mtu anaeweza kukuongezea mawazo ya ubunifu kwa kuwa wewe una asili ya ubunifu,

Wewe pia utamletea tabia ya kumjali, na pia kwake yeye utakuwa ni mwenye kujiachia, mkiwa pamoja basi mtahakikisha kuyaweka sawa mapenzi yenu na kuwekana sawa ikiwa ni pamoja na kurekebishana, nyote ni wenye mapenzi ya dhati katika mahusiano haya na wenye hisia kali, ingawa wewe ni mwenye hisia kali zaidi na na tabia yeke yeye ya kutaka kujiweka kuwa mtawala basi hukufanya kujihisi kama kakulinda na kukulindia mapenzi yako.

wakati utawala wake hukufanya wewe kujihisi umelindiwa mapenzi basi ndivyo inavyokuwa kwa maana anakuwa ni kweli kalinda mahusiano yenu na vile vile itafikia sehemu utahisi na kuona kakutosheleza na hutahitajia mwingine tofauti na yeye.

Ikiwa yeye atajirekebisha na kitabia chake cha kutaka usaliti kichini chini basi ni mtu ambaye mnaendanana nae pia katika mahusiano haya.

NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:


Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !