Ng'ombe na simba
Yeye hupenda sifa za mara kwa mara na Kutamaniwa na watu pamoja na kusifiwa.
na yeye milele mpinzani wake huwa ni mwenye nyota ya Ng'ombe ambaye ni wewe, Ningekuwa namfahamu huyu mwenzio ningemwambia atafute pa kwenda kwa maana wewe na yeye ni kama mbingu na ardhi vyovyote vile atakuja kukukera au utamkera mchukiane maisha hata salam zitagoma,
Matokeo yake kwenye mahusiano yenu. Kila siku yeye atataka kuabudiwa na wewe utataka kuthaminiwa hii couple haijawahi kwenda sawa hata kwa marafiki tu wa jinsia moja. Wewe utajikuta ni mwenye kupenda kuonekana hata kwa kidogo tu unachofanya yaani kuthamini sana hata kama jambo ni dogo na yeye atapenda kutukuzwa sana hata kama ni dogo.
Wapi uliwahi ona mfalme akamsujudia mtumwa au banki ikaomba mkopo kwa maskini (hutaona isipokuwa miujiza ya Mungu itokee) mkiachana wewe ni mwepesi sana kupata mpenzi wa kawaida na yeye ni mzito sana kurejea kwenye mapenzi.
Katika mahusiano yenu utakuja kumkosea kitu kidogo atakuchukia hadi maiti yako atainanga ukitangulia mbele za haki.
Hakuna kati yenu atakae pata anachotaka kwa mwenzie kwa wakati bila kutumia ubabe na nguvu ya ziada mkielewana leo kesho lazima amsha amsha ianze.
Zaidi ya kuongezea yeye ni mwenye ghazabu na wewe ni mpole.
Ghadhab, yake yeye ni kujaa kifuani fundo la miaka mingi na upole wako wewe ni Gubu.
Kuna ugomvi mkubwa kati ya tamaa zako kwa kutaka mambo yaende kwa mpangilio na yeye mwenye kuhitaji zaidi kupita hali ya maisha yani kama mna budget ya mwezi yeye yupo radhi aitumie wiki.
Kingono/tendo utapenda jinsi mnavyoendana ni balaa, lakini yeye anaangalia maisha kama duara 3 ambazo zinatakiwa kuzunguka pamoja na wewe hii itakuwia ugumu kutizama.
Muache aende kwa kina Aquarius ndio wanawezana nae na wewe tafuta Scorpio akuchangamshe vile unavyotarajia.
NOTE:
Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:
Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:
Email: rakimsspiritual@gmail.com
: mnajimu@unajimu.com
WhatsApp +255 783 930 601
Rakims