Mahusiano nyota ya Mapacha na Ng'ombe (Gemini and Taurus)

Rakims

 Mapacha na Ng'ombe

Haya ni mahusiano yasio na matumaini, ingawa mwanzoni utajikuta hujibu vema mapigo yake, na yeye ndio hivyo hivyo mwanzoni huvutiwa na misimamo yako. 

Lakini kiuhalisia utakuta yeye ni mwenye kutaka maisha ya msimamo na imara na kuamuru, 

wakati wewe hupenda maisha ya rahisi na kuchukulia maisha ni jambo la kawaida na halina mkazo sana isipokuwa ni kufuata mkumbo tu ni mwepesi sana wewe kuboeka na yeye mwenye asili ya itikadi za kujua yeye mwenyewe hivyo utachoshwa na yeye mwenye kutaka kufuata vitu hatua kwa hatua kama shule au kambini. 

Yeye hupenda maisha ya nyumbani na huona kama nyumbani ndio sehemu yake ya starehe wakati wewe unaona kutoka na kuwa mguu na njia ndio maisha.

Mapenzi yake utaona anayokupatia ni kwa udogo sana na vile vile utaona kama ni mtu anakubania bania linapokuja suala la kujiachia kimapenzi, 

Na kwa kuwa yeye ni mtu binafsi atakuwa anakitabia cha chini chini cha kukusimangia mapenzi, na yeye mwenye wivu, na mwenye kutaka kumiliki na kumtawala mwenzie basi hawezi kushughulikia

Mashindano na wewe kwanza kiasili toka mwanzo anakuwa anakuona hujatulia kicheche. 

Mapenzi yenu yatakuwa ni baridi.

NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:


Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !