Mahusiano nyota ya Punda na Mashuke (Aries and Virgo)

Rakims

 Punda na Mashuke

(Aries and Virgo)

Utangamano

Katika mahusiano haya ni baina ya Moto wa jaha na mchanga wa fungu,

Kitaalamu nyie ni baina ya moto na ardhi vitu ambavyo haviendani yaani wewe ni moto na yeye ni udongo,

Mahusiano yenu yapo hivi:

Kwanza kabisa ujasiri ulionao mara nyingi humpelekea kuwa na aibu yeye ambaye mara nyingi kitaalamu tunamuita binti maringo haijarishi jinsia yake, 

Nyote wawili ni wenye mawazo tofauti yaani kila mmoja na nguvu zake tofauti linapokuja katika suala la mawazo na utendaji vile vile, hasa linapokuja suala la chumbani bila shaka hili ndio kubwa hubeba na kuharibu mahusiano mengi, kila mmoja kati yenu utakuta ni mwenye mawazo tofauti na mwenzie katika kitanda jinsi ya utendaji na jinsi ya kufurahia tendo zima sote tunafahamu kwamba katika tendo la ndoa kwa upande wako ni kama vile uwanja wa vita tukirejea kwake yeye chumbani ni kama vile uwanja wa maonyesho, haiishii hapo tofauti yenu pia inatoka hadi nje ya kitanda kwenda kwenye maisha ya kila siku.

Mapenzi na mihemko yako wewe imejaa msukumo na moja kwa moja bila kupinda wala ubabaishaji.

Kwake yeye ngono zaidi ni suala gumu sana kugawa hata pia huchukua muda kuweza kumvulia nguo mwanaume au mwanamke. 

Kwenye maeneo mengine utakuta wewe ni mwenye shauku na mipango mipya na mawazo mapya. Na vile vile ni mwenye kulazimisha kuwa boss wa mahusiano hata kama utaficha mwanzoni.

 Tukija kwa bi maringo nimekwambia haijarishi jinsia yake utakuta ni mtu mwenye kukosoa na kusumbua, na hupenda mambo yaende jinsi yeye anavyotaka.

Huyu hawezi kuheshimu au kukubaliana na matakwa yako haijarishi atakuigizia vipi mwanzo.

Na yeye atakutoa kasoro kila siku zinavyoenda hadi utajihisi zuzu.

Na wewe utamuona ni mwenye mgomo baridi na asiyewezekana kufurahisha.

Niamini wawili nyie mwisho wa siku ni wenye kufanya vita sio mapenzi.

NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:

Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !