Mshale na Mshale
(Utangamano)
Saggitarius and Sagitarrius
Mahusiano haya ni baina ya moto wa nyasi kwa moto wa nyasi moja kwa moja unaweza kusema ni mfano watoto mapacha yaani wenye kufanana sana.
Lakini hata hivyo ukirejea mwanzo nilishaelezea kuwa hata nyota zenye kufanana huwa zina mushkeli yake.
Baadhi ya wanajimu huamini kwamba mwenye kuweza kumtosheleza Mwenye nyota sawa na nyota hii yako ni pacha wake lakini kwa uzoefu na elimu pamoja na experience nilionayo katika unajimu hapana hii pekee haitoshi bila kuwa na marekebisho.
Imagine mnaishi na mtu mnafanana kila kitu?
Mapenzi yenu yatakuwa lakini lazima tu kuna migongano,
Moja kwa moja twende kwenye uchambuzi wako:
Nyote wawili mnaonekana ni wenye kupenda maendeleo na wenye kuendana sana mwanzoni karibu kila kitu chenu, wenye kupenda kutoka toka na kuroam, japo kuwa ni jambo zuri kwenu machafuko, uhusiano wa matukio yasiyotabirika wala kufikirika huja kwa kushangaza sana.
mnaonekana hata kwenye macho ya watu ni wenye kuendana na kupendezana sana.
Lakini ni kawaida sana kwenu kila mmoja wenu kumletea majanga mwenzie, Kila mmoja kati yenu anakuwa sio mwenye kujitolea kwa mwenzie kwa udhati na mnakuwa nyote wawili ni wenye kupenda kuchakatia nje,
Pair yenu huwa inaokolewa sana na imani ya dini hasa ukizingatia nyota yenu inatawala sana elimu ya dini na vilevile akili ya kiimani zaidi lakini kwa Sagitarians ambao hawana dini katika nyoyo zao utakuta mwanaume anachakatia huku na mwanamke kule.
Mkikutana kila mmoja anaweza kumlia mwenzie yamini kwamba hana hayo mambo lakini pale zinapoanza kuingia mimba za ghafla na kuletewa watoto usio wajua ndio unakumbuka kumbe naishi na jini mwenye miguu miwili.
Wote kati yenu mnatabia ya kumsukuma mwenzie katika kufanya mambo maovu mnapokuwa mnakwazana anaweza kukuboost na kukwambia katembeze nje sibabaiki na wewe ukajaa kweli,
Ni nyota moja ya mahusiano ikiwa na msimamo na imani basi dunia nzima huona kama ya kwao lakini otherwise ni wachezaji wazuri tu wa nje furaha ikiisha ndani.
NOTE:
Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:
Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:
Email: rakimsspiritual@gmail.com
: mnajimu@unajimu.com
WhatsApp +255 783 930 601
Rakims