Mahusiano nyota ya Mbuzi na Ndoo (Capricorn and Aquarius)

Rakims

 Mbuzi na Ndoo

Katika mahusiano haya mnaonekana ni wawili msioendana hasa ukizingatia kwamba wewe ni mchanga wa bahari na yeye ni Upepo wa kimbunga;

Unaonaje dhoruba ikitokea kando ya bahari?

Hayo ndio mahusiano yenu yalivyo mkiunganisha roho, 

Wewe utajikuta unamuona yeye ni mtu usiyeweza kumtabiri, na yeye atajikuta ni mtu ambaye anashindwa kwenda na wewe kirahisi hadi atumie nguvu nyingi, 

Mbinu zako za kawaida tu za kumuendea hata katika kuomba mchezo utakuta kwake ni kero kubwa sana na atakuona kama vile muda wote wewe ni mwenye kumtibua tu mwanzoni utaona kama anakuvumilia lakini baadae sura kamili ya dhoruba itaonekana.

Yeye hujiamini katika kujieleza kimtizamo wake bila maneno.

Na wewe hujiamini katika kujiheshimu bila mipaka, mawasiliano yenu kila mmoja atajikuta haeleweki kwa mwenzie na pia ataona kama anaaibika na kudhalilika kwa mwenzie.

Yeye utakuta ni mtu wa kupenda mitoko na wewe utakuta ni mtu wa kupenda mtu mwenye kumaintain maisha ya nyumbani huyu ni mtu mtafutaji wewe utafurahishwa kwa utafutaji wake mwanzo kwa kufuata mkumbo lakini baadae itakuwa too much hata kama atakuletea maigizo sasa hivi lakini baadae visafari vya kwa ndugu jamaa na marafiki huwa havikatiki.

Yeye alivyompenda uhuru safari ya mapenzi yenu itakuwa ngumu sana na uvumilivu wake kwako ni mdogo huyu anataka mtu mwenye nyota ya moto wa mkaa ambaye yeye akimletea habari za kutoka anakuwa kama kamtia ny*ge. Hakika kipenzi chako hiki ni chenye kupenda kutoka sasa ukimfungia ndani kwa maisha yako ya siasa kali kimbunga kitazunguka kisha vumbi lako litapeperuka na kubaki umechafuka tu.

Nyie mnapendeza zaidi kuwa ni wenye urafiki tu na hata mapenzi yenu mara nyingi huishia kirafiki tu.

NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:


Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !