Nge na Ndoo
(Scorpio and Aquarius)
Mahusiano haya ni baina ya maji ya moto na upepo wa kimbunga hii ni fahari wawili hawakai zizi moja na pia hawa ni wagomvi wawili walio kubaliana kila mmoja akae upande wake wa dunia,
Mahusiano yenu yapo hivi:
Wewe utakuta ni mwenye kuwa na matakwa mazito ya kihisia, lakini yeye hata kuruka nae mara moja sio jambo zito kwake kwa upande wako yaani kumvulia nguo kwako yeye kwake ni jambo la kawaida wala halina uzito wowote katika hisia zake, kwake yeye wewe kukutana nae kimwili ni kama tu kupanua upeo wake wa yeye kukujua zaidi wala sio jambo la ajabu na kumfanya ajihisi yupo kwenye serious relationship.
Wewe ni mtu ambaye hutaweza kuvumilia jinsi yeye atakavyo kuwa anachukulia mapenzi yako kirahisi rahisi.
na kila mara unaweza kuwa na hisia kwamba hayupo serious na wewe isipokuwa ni part time tu.
Yeye binafsi ni mtu ambaye ni mwenye kuvutiwa zaidi na vya nje hata hivyo vya nje akiingiza ndani bado atavutiwa na vya nje tu hata ukiwa kwenye ndoa nae huyu hashindwi siku moja kukwambia umalaya upo kwenye damu you deal with it or leave it.
Japo akimpata anaemmudu kinyota huwa mpole kama kondoo.
Kitu ambacho wewe kitakutia wivu wa ajabu na vile una asili ya wivu, basi utataka kujaribu kumtawala na utakuta kila mara anakuvuruga jinsi anavyopenda uhuru na alivyo na mood za kuswing basi safari yenu itakuwa ngumu.
Wewe utakuta ni mwenye kupenda kuwa nyumbani na yeye utakuta ni mwenye kupenda uhuru wa kuendelea hadi mwisho kila mtu atashika njia yake.
Mkilazimisha nyie ni mtu na jamaa yake wasioelewana wanaochangia nyumba kulipia kodi.
NOTE:
Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:
Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:
Email: rakimsspiritual@gmail.com
: mnajimu@unajimu.com
WhatsApp +255 783 930 601
Rakims