Mahusiano nyota ya Simba na Simba (Leo and Leo)

Rakims
Simba na Simba

(Leo and Leo)


Utangamano;

Mahusiano yenu hapa huwa ni sawa na Mfalme na Malkia wanapokutana, 
Vichwa hugeuka kwa maana wawili nyie wote ni Simba na mahusiano haya ni sawa na simba dume na simba jike. Wawili nyie hapa ni wenye kuwa na uaminifu mkubwa sana, 
Mahusiano haya pande zote mbili huwa ni zenye shauku kubwa sana katika mizani wa kila mmoja kwa mwenzie. Wote wawili nyie ni wenye mapenzi makubwa na mko romantic sana.
Kila mmoja kwa mwenzie, wenye rangi za kupendeza na furaha kubwa katika maisha yenu ya sasa na ya baadae na wenye uwezo mkubwa sana wa kufikishana kileleni. 

Swali kubwa la kujiuliza hapa ni; Nani kati yenu atakae kuwa mtawala?
Ni ngumu sana kwa Simba mmoja kumuachia nafasi mwengine kutawala na kujiona muhimu na kujistahi kuliko mwingine.
Lakini hilo ndio kubwa linalohitajika zaidi kwenye mahusiano haya. 
Kila mmoja wenu hata taka tu kukaa kwenye kitu ya ufalme huu isipokuwa kila mmoja atataka aonyeshe mabavu yake pia.
Kwa ushindani wa kuridhishana kitandani nani atakae mridhisha mwenzie, Nani atakae muhudumia vizuri mwenzie, nani atakae mpa zawadi mwenzie, nani atakae pendeza zaidi ya mwenzie, nani atakaejali zaidi wazazi wa mwenzie, nani atakae mbembeleza zaidi mwenzie. 
Yaani ni ushindani wa mahaba makubwa na heshima kubwa hakuna mfano na umejaa hisia kali na kila mtu atakae waona atataka kuwaiga.
Wawili nyie ni sawa na mkaa unaopika chakula ukaongezewa mkaa mwingine, wawili nyie ni sawa na jua moja likaongezewa lingine yaani nyie ni watu mnaendana kuliko kawaida unless mmoja wenu awe kadanganya details;

Binafsi nayapenda mahusiano baina ya Simba na Simba maana wakiungana wanakuwa ni kivutio cha utalii na pia ni nyota pekee katika unajimu zinazoendana sana kuliko zingine kwa maana wote mnatawaliwa na sayari ya jua na hakuna anaeendana na mwingine isipokuwa jua mwenzie ni jua, simba mwenzie ni simba na vile vile mfalme mwenzie ni malkia.

Basi kama bado hamjafunga ndoa mnasubiri nini?

Nyie ni Grand lovers and interesting rivals (wapenzi wakuu na wapinzani wa kuvutia).

NOTE:Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:

Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !