Mashuke na Mashuke
(Virgo and Virgo)

Jinsi alivyo:
Kwa upande wake linapokuja suala la mahusiano au mapenzi;
Mapenzi kwa upande wake yeye huweka udhibiti mkali, yaani ni muangalifu sana inapokuja kwenye suala la mapenzi. Na ni mbaguzi katika suala la mapenzi, lakini kwa chini ni mwenye hisia za kimapenzi na mwenye tamaa ya kuwa na mapenzi japo ni mwoga. Kwa nje anaweza kuonekana ni mtu aliyetulizana. muda mwingine ni kama anajiweka kuwa asiyepatikana kwa muda sahihi anaohitajika.
kwa muhimu yeye ni mwenye asili ya utulivu na ni mwenye nyota ya kupingana sana na nyota zingine yaani yeye wengi humuona kama ni mwenye kupinga pinga mambo.
Kimsingi, mwanamke huyu huwa haamini na anaogopa kidogo inapokuja kwenye maswala ya hisia.
Kwake ni sawa na jambo ambalo halijulikani yaani unapomwambia habari za mapenzi kwa kuwa yeye ni mchambuzi basi utaona anakuwa kama hana maelezo sahihi kuhusiana na mapenzi na hisia.
Mara nyingi mapenzi kwake ni sawa na bahari iliyochafuka ambayo inaweza kuwekwa bila ramani au dira au usukani kwa nahodha mwenye chombo.
Na kwa hili basi mwanaume yoyote anayekuwa nae utaona kabisa kwamba anashindwa kuelewa kama huyu mwanamke ni wa baridi.
Uwezo wake mkubwa wa mapenzi huweza kumwagika kwa yule anaempenda na hili ni kama tu akiweza kufunguliwa hisia zake kwa maana ni hisia kali zilizojificha sasa akipata mtu akajua funguo yake na akamfungua vema basi utamuona anakumwagia mapenzi ya kila aina. Na taratibu nitakazo kuelezea hapa basi zitakuwa ni msaada mkubwa sana wa kuweza kufungua hisia zake zilizojifunga kwa muda mrefu sana.
Mwanamke huyu anatambulika kama mwanamke ambaye asiyeeleweka sana inapokuja kwenye suala la mapenzi. na vile vile kwa watu wengine huonekana kama muoga wa mapenzi, mwenye kukwepa mapenzi na mwenye kujihifadhi.
Lakini hili huwa sio kweli kwa maana kile anachofanya ni kuamini kwamba hisia za kimapenzi ni lazima ziongozwe kwa heshima kubwa yaani ili mtu aone anampenda lazima awe ana muheshimu sana.
Yeye ni nyota ya udongo ambayo ni sawa na nyota zingine za udongo yaani (ng'ombe,mashuke,mbuzi)
Yeye ni mwenye fumbo kubwa inapokuja kwenye suala la hisia na kujihifadhi yani cha kwanza kwake mapenzi ni nidhamu na kujiheshimu. Ukiwa na hilo ni sifa ya kwanza yeye anataka kwa mtu haijarishi kama amemzidi umri au laa unaweza tu kumwambia unajua mimi nakuheshimu sana basi hapo hapo moyo wake unaanza kukufungukia na hasa ukisema hivyo kwa upole.
Mwanamke huyu hupenda wanaume sana yaani ni rahisi kwa mwingine moja kwa moja kuwa malaya, lakini kwa huyu japokuwa anasifa ya kupenda sana wanaume ni mtu makini sana linapokuja suala la kujihusisha nao huwa hakubali kukurupuka na mtu. Hata kama kavutiwa sana na wewe basi utamuona hakuonyeshi kuwa wewe ni udhaifu wake ni mgumu sana kuelezea hisia zake kwanza kumwambia mtu anampenda yeye kwake ni jambo la aibu.
Macho yake na mwili wake mitindo yake ya kukaa na mavazi yake vinaweza kuwa kama vinakuita kwamba nisogelee lakini ukimsogelea basi tabia na heshima yake vinaweka kama ngao ya wewe kuanza habari zako za kuzimu.
Kwa kuanza nae kama ungejua tabia na muonekano wake ni vitu viwili tofauti ungejizuia hata kumtongoza ghafla.
Nae anatambua kwamba mwanaume sahihi kwake ni yule anaeweza kupitia mitihani hivyo anaweza kukupa mitihani mingi ili kuona kama unamstahili. Nae ni muoga wa kutumbukia katika mapenzi na mwanaume asiyekuwa sahihi katika kipindi kirefu mfano kufunga nae ndoa.
Kabla ya yeye kuingia kwenye mahusiano au ndoa utamuona ni mwenye kuandaa kabisa mazingira ya kutokea pale mambo yatakapo mshinda. Nae utamuona katika mahusiano anasogea hatua kwa hatua ili kuweza kujidhihirishia kuwa anaeingia nae kwenye mahusiano ni mtu wa aina gani na anajitahidi kuchunguza kama ni mtu wa kuaminika.
Ni bora ajiumize kuliko kutoka na mwanaume ambaye hajamridhia rohoni yaani yeye hafanyi mradi kafanya. atakaa nyumbani na kusoma kitabu au hadithi nzuri.
Na wanajimu wenzangu au wengine utaona wanamchambua mwanamke huyu kama mwenye kuonelea ni bora kusoma hadithi au kuangalia tamthilia ya kusisimua kuliko kufanya mapenzi.
Ni vi vile tu hapendi kukaa na kusubiri Mtu sahihi (Mr right) aweze kumfikia na mume sahihi anapomfikia basi moja kwa moja huona mwanamke sahihi ndani ya mwanamke huyu ambaye alikuwa anamtafuta ambaye ni mchangamfu na mwenye kujituma katika kila sector.
Kwa maana hiyo yeye huona kujiengua kwenye mahusiano yasiyo na maana ndio humfikisha kupata mwanaume sahihi.
Ambapo tabia hizi kwa mwanaume ambaye sio sahihi kwake hawezi kuzivumilia na huona kama tabia hizi zinamshinda na hujiengua.
Ili kuweza kuwa na mwanamke huyu unatakiwa ukumbuke kuwa yeye bado ni mwenye kuamini kuwa mapenzi ya kweli yapo na ndicho kitu anachokitafuta na kukitaka.
Na pale anapopenda kweli basi utaona vidhibiti vyake havitamzuia kuonyesha tamaa zake kwa mtu huyo. Anaoenda mwanaume wake na anapenda kumtibua tibua kwa matani mwanaume wake kihisia na hupenda kujaribu jaribu mambo mapya kwenye mapenzi ambayo yanaweza kuinua furaha kubwa ya mapenzi.
Ingawa huyu si mwanamke unaeweza kumuwekea asilimia zote kwenye maisha. kwa maana unatakiwa kwanza uteseke ili kuweza kumteka, mnyenyekee, mbembeleze, mtimizie kwa wakati, kama utaweza hayo basi utakuwa na mwenza ambaye atakulipa kila fadhila ambazo ulishawahi kumfanyia kubwa na dogo kwa maana yeye kwake fadhila ni deni na lazima alipe ni mwenye kupenda kulipiza visasi pia.
Basi ni mwanamke ambaye kwake utapata mapenzi makubwa, heshima, kujaliwa na kulindiwa mapenzi yako ukiweza kumfanyia hayo.
Utengamano wenu
NOTE:
Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:
Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:
Email: rakimsspiritual@gmail.com
: mnajimu@unajimu.com
WhatsApp +255 783 930 601
Rakims