Mahusiano kinyota Ng'ombe na Mshale (Taurus and Sagittarius)

Rakims

NG'OMBE NA MSHALE

(Taurus and Sagittarius) 

Utangamano

Mahusiano haya yanaweza kwenda pale to Ng'ombe akiweza kujikaza na kumvumilia Mshale. Wawili hawa ni wenye kuvutiwa kila mmoja na mwenzie kimwili, kwa maana hisia na mihemko ya Ng'ombe huchangamshwa na ufanisi wa mshale katika kufanya mapenzi.
Lakini Ng'ombe itamuwia ugumu kuzoea tabia ya Mshale kuzungusha macho sehemu zingine tofauti na kwake yaani kusifia au kutizama wenza wengine ikiwa ni pamoja na kutamani ama kutoka nao kabisa.

Mshale ana tabia ya kujirahisi kimaongezi japo kwa ndani anaweza kuwa ni mwenye msimamo wa dhati na mwenza wake lakini anaposogelewa na mtu wa pembeni ambaye anakuwa kavutika nae basi hujirahisi kimaongezi na moja kwa moja Ng'ombe huanza kumshuku kuwa ana tabia za kimalaya.

vile vile katika mahusiano haya mshale ni mwepesi sana katika kutambua maisha ni yenye kutaka mtu kuwa huru katika tendo na kila kitu';l- hivyo hutaona akimbana sana Ng'ombe na ndipo gubu na dhana za ng'ombe huanzia hapo na kuonekana hajali.

Vile vile wawili hawa wote ni wenye kupenda kutawala mwenza wake kichwani. Na inapokuja kwa upande wa mshale kuona anataka kutawaliwa vita huanzia hapo kwa maana yeye si rahisi kutawaliwa na mwenza iwe ni mwanaume au mwanamke.

Hakuna wakati mgumu kwenye mahusiano haya isipokuwa ni vichekesho lakini mpango mzuri wa magomvi ya kila mara. 
Uchumba unaweza kufurahisha ila ndoa inaweza kuchukiza sana. 
(Hawa ndio baadae huanza kulalamika ndoa ndoana) na hujinadi kwa kusema tunalewa watoto.

NOTE:
Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:


Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !