Mahusiano kinyota Ng'ombe na Nge (Taurus and Scorpio)

Rakims

Ng'ombe na Nge

(Taurus and Scorpio)


Nyota hizi mbili ni kinyume kwa asili yake;

Hizi mbili ni kinyume katika mtizamo wa kinyota yaani hasi na chanya hivyo moja kwa moja kwa nyota zozote zile ambazo ni hasi na chanya yaani kwa mtizamo mmoja zenye kuwa na maada ambazo zipo katika mizani sare 

mf; inayogawanyika kwa mbili na nyingine yenye kugawanyika kwa mbili na zikaendana au kugawanyika kwa moja na nyingine ikagawanyika kwa moja kisha moja ikawa maji na nyingine udongo ama moto na upepo. 

Basi mara nyingi mkanganyiko huo huwa unaweza kuendana tu vema. Sasa tukirejea kwa hawa wawili ni wenye uwezo zaidi wa kuendana wao kuliko kuendana na nyota zingine.

Wote wawili ni wenye kudhamiria katika mahusiano yao na wanatamani, na kati yao wakikutana hakuna anaetamani kutoka nje ya mahusiano, ama kumtelekeza mwenzie, 

Hata hivyo, kuna majaliwa yenye nguvu kwa wawili hawa hasa linapokuja suala la mapenzi ya nguvu na kufanyia kazi upendo wa kila mmoja kwa mwingine;

Tukianza na ng'ombe ni mwenye shauku katika mapenzi na mwenzie ambaye ni Scorpio (Nge) hivyo Ng'ombe anakuwa na uwezo zaidi kuliko nge mwenyewe kwa maana kama ingekuwa ni kupimisha nani anampenda mwenzie zaidi basi moja kwa moja tungesema kwa couple hii wewe mwenye nyota ya Ng'ombe basi ndio unampenda mwenzio zaidi hapa. Ikiwa utaonyesha ama utaficha.

Tukirejea chumbani kwenye tendo mnakuta ni wenye kuendana na kuridhiana lakini Nge ni mwenye tabia ya kupindukia mfano kuadapt jambo katika tendo kisha kuwa nalo kama addicted, na vile vile tabia yake ya wivu kuonyesha wakiwa pamoja basi humfanya Ng'ombe kuchemka kwa hasira. 

Ingawa ni wenye kuendana sana lakini inapokuja kwenye wivu wawili hawa hufika hadi kwenye ndoa lakini lazima tu hutokea mtafaruku na kuachana ambao unasababishwa na mwenzie kutokuwa na msimamo.

Hivyo msimamo hapa ni kufikia hatima ya makubaliano yenu kama mmeamua kuwa wapenzi milele basi ni milele na kama mmeamua kuwa wenye ndoa basi ni moja kwa moja.

 NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:

Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !