Nge na Kaa
Utangamano
(Scorpio and Cancer)
Nyota yako kwanza kabisa inahusiana na kifo na kila aina ya jambo baya kwa maana ina tawala mlango wa nane (House of dealth and regeneration). na vile vile wenye nyota yako sifa hizi mbaya huja kutokana na hisia kali ulizonazo na pia ukandamizaji wako katika tendo la ndoa,
Mahusiano haya ya nyota hizi mbili za asili ya maji yaani maji ya moto na maji ya bahari ni yenye kuvutia na kupendeza machoni kwa watu kwa jinsi mnavyokuwa hata mbele za watu. Kwa hapa hujakosea kama hujafunga ndoa basi nenda hata kafunge kesho.
Ingawa sasa nyota yako ya Nge ni nyota ya mtu ambaye ni sawa na mbalamwezi iliyodondoka ambayo mbalamwezi ni sayari ya nyota ya kaa kinajimu kwake wewe ni sawa na baba au mama kutegemea na jinsia yako. Sasa kama wewe hisia zako zikichanganyika na ukali basi mahusiano yenu yatakuwa ni sawa na mapenzi ya ugomvi wenye hisia za mahaba makali ndani yake yaani mnaweza kutukanana kisha mkacheka Isipokuwa baadae hii itakuja kumchosha yeye na vile uombaji wako wa tendo mara zingine umetawala mabavu na shari.
Kwa hivyo hapa mtakuwa mnaendana kwa asilimia 90%
Nge & Kaa uaminifu wenu
Wewe (Nge) unapopenda moja kati ya jambo kubwa kwenye mahusiano yako huwa ni Uaminifu, Ikifikia sehemu umejihisi kusalitiwa basi mara nyingi huonyesha wivu wako wote na uchungu sana bila kuficha na kila mtu aliyekaribu yako atajua kuwa umesalitiwa.
Na nyote vile ni wenye asili ya maji mara nyingi ni watu ambao usaliti kwenu kila mmoja ni kitu anachopenda kufanya japo ni wenye mapenzi ya dhati kila mmoja kwa mwenzie hivyo kwa ugumu kidogo mwanzo kwenye uaminifu mapenzi yatayumba lakini baada uaminifu huja kwa upana sana kwa maana kila mmoja kati yenu anajua ni jinsi gani mapenzi yanauma.
Hivyo linapokuja suala la uaminifu mnaendana kwa asilimia 95%
Nge na Kaa mawasiliano yenu na mazungumzo:
Wawili nyie ni wenye kuelewana hata kama pasipohitajika mazungumzo yaani sura tu huonyesha kujielezea kwa kila mmoja wenu. Hii pia huweza kuinfluence maisha yenu ya tendo la ndoa na kulifanya kuwa bora kuliko watu wengine. Lakini vile vile hii inaweza kuwa ni yeye kuleta mtafaruku kama mapenzi ya mwingine yataelemea katika kitu fulani tuchukulie mfano hajakupenda wewe na kapenda kile ulichonacho. Mazungumzo yenu ni mazuri sana kwa kuwa tu mara nyingi huhusisha hisia zenu. Na hata muda mwingine kwa wale wanaoanza urafiki utaona ni wepesi kila mmoja kumalizia sentensi ya mwenzie. Wote ni wenye kupenda kuzungumza mara kwa mara ingawa hili mwanzoni sio rahisi kuonekana na mara nyingi kwako wewe ni mwenye kupenda kujiweka hupendi maneno na una katabia ka kuexaggerate mambo.
Ikitokea yeye akaanza kukuona tofauti mwanzo basi moja kwa moja atashindwa hapo hapo mwanzoni kuendelea na wewe na atatafuta kila njia ili kila mtu ashike nafasi yake. Lakini hii ni ngumu kwa maana mkiwa pamoja kila mmoja wenu anatamani na kutaka kuhakikisha anamuweka mwenzie sawa vile anavyopenda aende nae yeye.
Hivyo tunapokuja kwenye maelewano yenu mnaendana kwa asilimia 99%
Nge na kaa Hisia zenu:
Hii ni nyeti sana na tawala ya kimbinu sana kwenye mahusiano kama haya.
Kwa hali hii kwenye suala la hisia mnaendana kwa asilimia 70%
Nge na Kaa Thamani:
Linapokuja katika suala la kuthaminiana hapa huwa kuna mtiti kwa maana yeye ni mbinafsi katika suala la thamani na ni mwenye kutaka familia yenye kumtegemea yeye tu. kwenye familia huyu ni mbinafsi na bahili, Lakini kwenye familia wewe ni mtu wa kujiachia na inapokuja kwenye kuthaminiana wewe huthamini mwanzo wa thamani yenyewe kisha baadae kushusha kisha kupanda yani wewe kwake suala la thamani ni jambo la kupanda na kushuka. Ni ngumu na ugumu kwenu huja kwenye suala la kuthaminiana hata mjitahidi vipi ugomvi wenu mkubwa utakuwa ni kuchanganya maana ya neno thamani na kujali.
Hivyo kwenye thamani nawapeni asilimia 25%
Nge na kaa Kushirikishana
Kwenye suala la kushirikishana mambo litawalindia sana issue ya nyie kuthaminiana kwa maana ndio kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba thamani na kujali mahusiano yenu hajajui maana yake ndio maana linapokuja suala la kushirikishana utaona mmoja kati yenu anasema kuna muda ananithamini na kuna muda hanithamini hapana hayo ni matumizi mabovu ya maneno haya mawili na elimu ya kutofautisha hili hata muwe ni waelewa vipi kwenye hili la kuthaminiana hamuwezi kuendana wala kuelewana.
Hivyo kwa ushirikiano hapana shaka mnaendana kwa asilimia 95%
Summarize:
Mahusiano kati ya wawili nyie yanaweza kupiga kila siku hatua kutoka hatua moja kwenda nyingine. Kiukweli ni watu wenye kuendana sana na mahusiano yenu hushamiri kama umeoa au kuolewa na mtu haeleweki na umempata huyu basi muache yule kaa na huyu lakini kama upo nae kwenye mahusiano tu basi oa leo kabla ya kesho, na kama ni mtu una mfukuzia usikate tamaa.
NOTE:
Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:
Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:
Email: rakimsspiritual@gmail.com
: mnajimu@unajimu.com
WhatsApp +255 783 930 601
Rakims
