Mahusiano nyota ya Nge na Ng'ombe (Scorpio and Taurus)

Rakims

 NGE NA NGOMBE


Scorpio and Taurus
(Utangamano)

Kwa mtizamo unaonenyesha wewe ni maji ya moto na yeye ni mchanga wa fungu. huyu ndio mwenza wako mnaoendana kwa safari nzima ya maisha na anaweza kukukamilisha na kukufaa zaidi na ni perfect match wako kwa sababu;-
Yeye anaonekana ni mtu mwenye stamina na hamu na ana uwezo mzuri wa kukidhi mahitaji yako hasa mkiwa chumbani na mkiwa pamoja ni watu wenye kujiweza kuwasha na kuzima moto wenu wenyewe ni watu mnaweza kugombana dakika 1 kisha ya pili mkaelewana.

Lakini kipi ambacho kinaweza kuwa tatizo kwenu kwa masaa yaliyo baki mnaonekana;-
Kwanza kabisa nyote wawili ni wenye wivu wa kupindukia na viburi(wakaidi) tofauti yenu ni kwamba yeye ni mtu anaependa kummiliki mpenzi wake na kama mtu wa thamani sana, kama ilivyo kwa kitu cha thamani na wewe unakuwa ni mtu wa hisia sana.
Ingawa mnashiriki mshikamano mzuri kuhusu maswala ya pesa, wewe ni mfadhili na hudharau uvivu,
wakati yeye anapenda kutumia kwa kujiridhisha kama yeye na ni jambo lingine nyote wawili japokuwa ni watu mnaendana sana lakini ni sawa na fahari wawili kila mtu anataka awe zaidi na ikitokea mmoja hajakubali kuwa chini ya mwenzie basi ni sawa na nahodha wawili wanaogombania kuendesha meli vita vikizidi chombo kinazama.

Elewa kwa mtizamo huu ukishindwa kuishi na watu wenye mchanga wa fungo ambao wanaweza kukumudu wewe basi utaishia kuwa mpweke na kila mtoto kuwa na mama yake kama mlivyo na sifa hii wengi wenye maji ya moto

NOTE:
Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:

Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !