Mahusiano kinyota Ng'ombe na Samaki (Taurus and Pisces)

Rakims

 Ng'ombe na Samaki 

(Taurus and Pisces)


Utangamano

Katika mahusiano haya kuna ugumu wa Samaki katika kuelewa kabisa Mtazamo wa uhalisia wa maisha. 

Lakini hili litategemea na uchaguzi wa maisha ya Ng'ombe atakayotaka kwenda nayo kwa samaki, Maana yoyote mwenye nyota ya samaki maisha yake huwa kama ni ndoto ambayo anaimani ipo siku itatimia hata kama hana nyenzo.

Nyota ya samaki ni moja kati ya watu wenye imani sana kwa kila kitu,
Hivyo jinsi ng'ombe atakavyo kuwa anamuendea mwenza wake ndivyo hivyo kunaweza kunusuru mahusiano haya;-. 

Taurus (Ng'ombe) mwenye bidii huweka mfano mzuri wa jinsi mtu unavyotakiwa kuyaendea maisha na mwenye nyota hii ya Pisces ambaye tabia yake kubwa ni uvivu.
 
Pia, asili ya vitendo vya mwenye nyota ya ng'ombe huenda kwa taratibu yaani hujitahidi kwenda na mtu jinsi alivyo humfanya samaki kuweza kufunguka na kuingiwa na msukumo wa kutambua maisha ni nini, Hasa ukizingatia Samaki ni mwenye asili ya mihemko ya kulipuka na kupoa ghafla.

Katika upendo wawili hawa kila mmoja ana tabia yake, Taurus ni mwenye kujitolea kwa yule anaempenda na Pisces ni mwenye kumuabudu mwenza wake yaani kutii kupitiliza yeye kila kitu kwake ni sawa. 

Ingawa Pisces anakuwa na nguvu zaidi inapokuja kwenye maono ya kiroho au mitizamo akisema kitu mara nyingi hutokea hasa linapokuja swala la kumbashiria kitu.

Ukija kwenye suala la kufanya mapenzi wawili hawa wanaendana sana na wanaweza kuridhishana Taurus ni mwenye shauku katika kufanya, Pisces ni wa kimwili zaidi, 
na kuna ubaya gani hapo? hivyo nyota mbili zinazoendana hasa ukizingatia kwamba. Ng'ombe ni udongo na samaki ni maji.


NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:


Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !