Ascendant

Rakims
0

ASCENDANT YAKO IKIWA KWA  MASHUKE VIRGO:

 Kuwa na ascendant ya Virgo inakuonyesha kuwa ni mtu mwenye asili au tabia ya uchambuzi 

Ingawa mihemko yako ya uchambuzi inategemea na mitizamo mingine katika mzunguko wako mzima wa unajimu wako (chart yako nzima).

kwa ujumla ni mtu ambaye unategemewa kuwa na uwezo mkubwa hata wa kuchambua dunia nzima kupitia akili yako hii haimaanishi kwamba ni mtu kila jambo unatumia akili na huna hisia.

Hakika kinyume chake ni kweli,

ni mtu unaetegemewa kuwa ni mwenye kujali sana watu wengine. 

Hata hivyo, ni mchakato wa kufikiri kimantiki unaotoa wewe ni wenye kuridhisha ndani kabisa. 

Unashukiwa kuwa ni mtu mwenye kutoa mawazo ya akili na mwenye uwezo mkubwa wa kujua ukweli wa jambo.

Utambulisho wa amri na kutambulisha chochote ni uwezo ambao unao pia, yaani ni kipaji chako cha ziada na pia una muonekano mzuri wa kuwa muandishi bora wa habari.

 Ni mtu mwenye mawazo yasiyobadirika na ukitoa wazo lako unataka libaki kuwa ni hilo hilo na lisiweze kupingika.

Na kwa wewe adui au jambo usilopenda ni kupingwa au kutokusikilizwa ukisema kitu.

Kwako wewe dhambi kuu ni kutojua ujinga wa mtu. 

Kosa lako wakati mwingine ni kutoweza kwako kuweka mambo sawa, 

na kupoteza mtazamo wa picha kubwa yaani kujua jambo kwa undani zaidi. 

Unakuza umuhimu wa maelezo madogo na kisha kuwa na kinyongo ikiwa wengine wanaposhindwa kuona umuhimu wako.

Kazi ni muhimu kwako, na kwa kawaida hutimiza jambo kubwa sana katika uhai wako. 

Mara nyingi uko kwenye vita ndani yako mwenyewe yaani ni mtu mwenye kufanya debate na akili yako muda mwingine, kutaka mambo yaje kwa urahisi na kuhitaji kufikia kwa juhudi zako mwenyewe.

ni mtu mwenye udhibiti - katika mambo yote mawiili

Yaani binafsi na matukio—ndiyo yanayo kufanya ujisikie salama. 

Na matokeo yake unaonekana ni mwenye kupata mafanikio ya jambo lako mwenyewe bila kusikiliza ushauri au maneno ya watu wengine. 

Una uchangamfu na ni mtu mgumu kutawaliwa popote kimapenzi ama kiakili.

Wewe sio rahisi kila wakati kujiweka karibu na mtu. 

Na unaonekana ni mtu mwenye aibu na kujitenga (wakati mwingine kujificha vyema na mambo ya kijamii) lazima mtu akuchimbe sana ikiwa anataka kuwa karibu na wewe. 

Unaonekana ni mtu mgumu kuonyesha hisia zako. Ingawa uso wako huonyesha mengi yanayokuwa yanaendelea nyuma ya pazia kwako. 

Kama wakati upo mtoto, wakati mwingine ulikuwa unakabiliwa na kuwa na  afya mbaya kwa kukosa furaha. 

Na jinsi ulivyokuwa unaenda unakuwa basi ndivyo unavyozidi kuwa na afya njema na furaha, afya inaboresha kadiri unavyozeeka. 

Na pia kwako, mwenzi wa ndoa huleta mali au utajiri. 

na mara nyingi katika nchi ya kigeni ni mtu mwenye kuweza kupata mali na utajiri huko. 

Mafanikio kwako mara nyingi huhusishwa na shughuli za kuhama kutoka ndani na kusafiri hadi maeneo ya mbali na nyumbani huko ndio wewe huanza kufungukiwa na mafanikio.

Unategemewa kuwa na tabia ya kuwa mpole, uso wa mviringo, macho yanayozunguka chumba na kuingia ndani kila kitu yaani una macho ya uchunguzi, na mwili unaotoa taswira ya udhaifu

lakini wenye nguvu sana.

Sayari ya Mercury, ambayo inatawala nyota ya mashuke, ni maarufu sana

katika horoscope yako. 

Ushawishi wa Mercury hutoa akili yenye mantiki, nguvu kali za uchunguzi, kiakili

mtazamo wa nje, mtazamo wa maono na ustadi wa sayansi na uandishi.

Pia huchochea ugomvi, hali ya neva kujikuta ni mwenye kejeli, kutafuta makosa, na wasiwasi.

Huo ndio mtizamo wa ascendant yako

NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:

Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims
Tags

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !