Mahusiano nyota ya Simba na Punda (Leo and Aries)

Rakims
0

Utangamano 

Katika mahusiano haya wewe ni mwenye moto wa mkaa na yeye ni mwenye moto wa jaha hivyo moja kwa moja nyote wawili ni wenye kuendana vema hasa ukizingatia tabia zenu ni kama washindani wawili wenye kushindania mahaba...


Wawili nyie ni sawa na Watu maarufu kinyota kwa maana ni wenye kuendana sana na hasa linapokuja kwenye suala la chumbani ni wenye mapenzi ya kushangaza.

Ni wenye kufanya kila kitu kinachohusu mapenzi kama ushindani yaani nani mshindo ni wenye kupenda matani ya mara kwa mara. Ingawa wewe ni mwenye Mood swing na yeye ni mwenye kupenda kuwa mood off.. lakini muda mwingi utakuta ni watu wenye mapenzi makubwa.

Kwa uaminifu wewe ni muaminifu katika mapenzi lakini kwa upande wake punda ni punda tu hivyo utatakiwa umfanye atulize kishwa.

Linapokuja swala la kujamiiana kwenu ni vita. Kila mtu anakuwa kajiandaa vya kutosha ingawa face expression muda mwingine inaweza ikawa haijitoshelezi.. 

Lakini moyoni ni wenye kujiambia hapa sikubali kushindwa, Ni watu ambao mnachangia kupendezewa na vitu sawa. 

Kwako hufikia umri ambao utajikuta ni mtu mwenye kupenda sana kwenda sinema na yeye ni mwenye kuvutiwa zaidi kufuatilia sinema..

Mara nyingi movies zako pendwa ni Sci-fi na Fantasy na yeye ni Actions and Intelligence hivyo ni wenye kuvutika kila mmoja wenu na mwenziwe anachopenda.

Hivyo hivyo hata kwa vitu ambavyo hampendi navyo hufanana kwenu. Tatizo lenu kubwa kwenye mahusiano haya ingawa mnaendana sana ni jambo moja.

Kila mmoja wenu anagubu la asili na kupenda kulalamika kwa kitu kidogo hasa kwa upande wako ambaye kila kitu wewe hupeleka moyoni.

Kila mmoja kati yenu ni mwenye kutaka kumtawala mwenzie..

Wewe ni kama mfalme kutawaliwa ni jambo ambalo halikuvutii hata katika historia ya maisha yako na yeye ni kama Amir Jeshi Mkuu.. Kutawaliwa kwake ni Mwiko..

Ili mahusiano yenu yaweze kwenda kila mmoja huvutiwa zaidi na mwenzake akiwa atampa uhuru wa maamuzi na kujitawala.

Shida nyingine katika nyumba yenu. Wewe ni Mtu utakuwa mwenye kupenda watu yeye atakuwa hataki watu hata kidogo.
Either atakwambia au hata kwambia mwisho wa siku kila anaekuja kwenu yeye atakuwa anamtoa kasoro ili tu ifikie sehemu aone vibaya awaache.

Rakims

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !