Mahusiano nyota ya Punda na Mapacha (Aries and Gemini)

Rakims

Punda na Mapacha

 (Aries and Gemini)


Utangamano

Mahusiano ya wawili nyie kwanza kabisa ni watu ambao sio wenye kuchoshana au kumfanya mwingine ajihisi bored kwa sababu wote wawili ni wenye kupenda kuongea;
Maongezi ni jambo kuu kwenu japo kwa maongezi yeye mapacha hushika nafasi ya ushindi.
 Wawili nyie ni wenye kuendana kwa usahihi zaidi. Kwa maana mahusiano haya ni sawa na moto na upepo, 
Upepo ni yeye ambaye akipuliza moto unawaka na moto ni wewe mwenye nyota ya Punda kwa maana ukiwaka yeye hujihisi ni mwenye kuwa na msaada mkubwa kwako kimaisha na kimahaba.
Hii ni moja kati ya couple ambazo kama muhusika  ni mwanaume basi utaona kabisa kuwa anajiona ni mwenye bahati anapokuwa na mwanamke huyu.
Yeye  (Gemini) utaona ni mtu asiyependa kutulia na mwenye tamaa ya kujaribu mambo mapya na hata wewe utakuta pia kwa upande wako ni hivyo hvyo.
Kati ya wawili hawa wala hakuna vizuizi kwa pande zote mbili. ni wenye kuendana na wenye mapenzi mazuri ya kuvutia, labda katikati yao kuwe na watu wenye kufuatilia mahusiano yao. Mara nyingi mahusiano yenu utakuta ni yenye kufuatiliwa sana na ndugu zenu.

Yeye ni mwenye akili ya haraka kuweza kutambua kwamba wewe mwenye nyota ya Punda moja kwa moja unataka kumtawala.
Na pia yeye atatafuta mihemko ya hisia nje ya mahusiano yenu lakini ni mwenye busara juu ya hilo.

Fikra zenu hucheza pamoja. Utakuta wewe ni mwenye nguvu na akili kwenye mahusiano haya na yeye ni hodari na mwerevu katika mahusiano haya.

Wewe (Aries) hupenda kuwa kiongozi wa tendo la ndoa mnapofanya, na yeye (Gemini) utaona ni mwenye kukufurahia kwa kutoa sauti za miguno kwenye tendo ili kukupa hamasa ya kuzidisha mapenzi.
Kwa mtizamo wa nyie wawili ni wenye kuendana na hamna mashaka.

NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:

Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !