UNAJIMU
Unajimu au astrolojia ni elimu juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha ya binadamu duniani. wengi hutizama unajimu kwa mazoea ya siku hizi kama utani wa kale uliopitwa na wakati lakini kuna mengi ya siri yaliyomo ndani ya elimu hii achilia mbali ufanisi wake katika falaki na uchawi wa nyotaWasomi wa unajimu wanaeleza ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio mbalimbali na mifano yake inakuwa ni kama ifuatavyo:-
amani,
vita.
maelewano.
maafa.
Mahusiano haya hayajaweza kuthibitishwa na sayansi ya fizikia au sayansi nyingine ambazo ni za kuonekana kwa haraka.
Alama za nyota 12 ni msingi wa falsafa hii ya unajimu.
Elimu hii ya Unajimu imekuwa ikitumika kwa miaka mingi lakini siku zote imekuwa ikipata upinzani mkubwa toka kwa wana sayansi hasa ukizingatia kila siku inavyozidi kupoteza uelekeo wake zaidi kulingana na uvumbuzi mbali mbali unaokuwa unafanywa na baadhi ya wagunduzi mbalimbali wa maswala ya anga kama sayari na nyota za ziada.
Unajimu una misingi tokea enzi za zamani wakati sayansi ilipokuwa ya chini na imani za kiroho na kiungu zikiwa za kiwango cha juu katika jamii nyingi.
Baadhi ya tafiti zilizofanywa kuchunguza usahihi wa unajimu unaonyesha kuna usahihi wa asilimia kama 25 ambayo ni sawa na robo ya nguvu ya usahihi mzima.
Hii kwa watu wenye imani za kiroho inawatosha sana kuamini hili suala kwa maana wengi hutambua na kufahamu kuwa elimu ni bahari hivyo unavyojua wewe basi kuna wenzio wanaojua zaidi si uzito kuamini katika hili ingawa bado kuna upinzani mkubwa toka katika ulimwengu wa sayansi ya kisasa

Tukirejea katika Tabia za watu na alama za Nyota kwa kulinganisha na unajimu;-
Alama za nyota zinabashiri tabia na haiba ya binadamu katika dunia.
Mpangilio au nafasi ya sayari katika mzunguko wake angani unaaminika kuleta athari kwa binadamu na matukio katika dunia.
Kuna nyota 12 za kinajimu ambazo mnajimu yoyote huzitambua na kupitia hizo hupatikana muongozo mbali mbali wa mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu.
Kila moja ina mvuto wa nguvu wa kipekee toka katika mpangilio wa nyota fulani.
Nyota hizi ni kama ifuatavyo:
Waliozaliwa Des 22 – Jan 19 wana nyota ya Mbuzi(Capricorn)
Waliozaliwa Jan 20 – Feb 18 wana nyota ya Ndoo (Aquarius)
Waliozaliwa Feb 19 – Machi 20 wana nyota ya Samaki (Pisces)
Waliozaliwa Machi 21 – Aprili 19 wana nyota ya Kondoo (Aries)
Waliozaliwa Aprili 20 – Mei 21 wana nyota ya Ng’ombe (Taurus)
Waliozaliwa Mei 22 – Juni 20 wana nyota ya Mapacha:(Gemini )
Waliozaliwa Juni 21 – Julai 22 wana nyota ya Kaa(Cancer)
Waliozaliwa Julai 23 – Agosti 22 wana nyota ya Simba(Leo)
Waliozaliwa Agosti 23 – Sept 22 wana nyota ya Mashuke(Virgo)
Waliozaliwa Sept 23 – Okt 22 wana nyota ya Mizani (Libra)
Waliozaliwa Okt 24- Nov 21 wana nyota ya Ng’e (Scorpio)
Waliozaliwa Nov 22- Des 21 wana nyota ya Mshale (Sagittarius)
Makundi ya Alama za Nyota
Makundi ya alama za nyota hizi ambayo ni 12 yamegawanyika katika sehemu kuu 4 ambazo ni maada;-
- Moto Yenye matamanio ya mafanikio au makuu,dadisi
- Maji Yenye kubadilika na yenye uwezo wa ufahamu wa ndani
- Upepo Imara na yenye kukuza au kuendeleza
- Udongo Yenye elimu au uwezo wa kutambua na yenye kuhamasisha
Hizi ni Maada nne zinazoongoza astrologia/unajimu. Na kila moja ya kundi hilo linabeba tabia fulani za kipekee.
Tukirejea katika Alama hizi 12 za nyota zimegawanyika kama ifuatavyo:
Moto: Kondoo, Simba,Mshale
Maji: Ng’e, Samaki, Kaa
Upepo: Mapacha, Mizani, Ndoo
Udongo: Ng’ombe,Mashuke,Mbuzi
Kila alama ya nyota 12 zimegawanyika pia katika makundi mengine matatu ambayo ni Yenye Umuhimu au Msingi
- “Cardinal” ikiwa na maana zenye Kubadilika: Kondoo, Kaa, Mizani, Mbuzi
- “Mutable” ikiwa na maana zenye kutokubadirika: Ng’ombe, Simba, Ng’e na Ndoo
- “Fixed” ikiwa na maana zenye nyuso mbili: Mapacha, Mizani, Mshale na Samaki
Alama ambayo iko katika moto na iko katika kundi la msingi huwa na tabia za upinzani na ubishani wa hali ya juu kama Kondoo.
Alama ambayo ipo katika kundi la Udongo na Kubadilika huwa na tabia za utulivu wa hali ya juu kama Ng’ombe.
Haiba na Tabia za Alama za Nyota
1 Nyota ya Kondoo
MIMI
“Mimi Kwanza”
Mimi nasema,
mimi nimeamua
Hii mara nyingi huwa ni kauli na msimamo wa watu wenye nyota hii na wao huhukumiwa kama watu ambao ni wabinafsi
- Ni mwenye maamuzi yasiyopinda na mtendaji mzuri wa kazi.
- Anategemea makuu juu yake mwenyewe na kutoka kwa wengine
- Mwenye kujitegemea na mwenye hali ya juu
- Anauthubutu wa kujaribu mambo makubwa
- Mwenzilishi wa mambo na mbunifu
- Kiongozi
- Muongeaji
- Ni mwenye hisia kali na asiye na uvumilivu mkubwa.
- Mwaminifu kwa marafiki na familia
- Anajali mpenzi wake na mwenye hisia kali za mapenzi
Bonyeza hapa kupata maelezo kamili ya nyota yako NYOTA YA ARIES (PUNDA)
2 Nyota ya Ng’ombe
“Nafanya ninachokipenda” Nimepata.Ni mwenye nguvu na mstahimilivu kimwili na kiakili
Makini na muangalifu
- Ana kiburi na asiyekubali kushindwa kirahisi
- Mstahimilivu
- Mwenye kutegemewa
- Ni mgumu kubadilika
- Anapenda vitu vizuri na vya thamani
- Anapenda urembo na vitu vya kupendeza
- Mwenye hisia zilizofichika
- Huenda akaonekana mbinafsi lakini ni wenye kutoa wakiwa na mali au fedha.
Bonyeza hapa kupata maelezo kamili ya nyota yako NYOTA YA NG'OMBE (TAURUS)
Ninafikiri, Nadhani “Ninapanga” Ndugu zanguNi mwenye kipaji kikubwa,mwenye kubadilika na anayechoka haraka na kukata tamaa
3 Nyota ya Mapacha
Ninafikiri, Nadhani “Ninapanga” Ndugu zanguNi mwenye kipaji kikubwa,mwenye kubadilika na anayechoka haraka na kukata tamaa
- Anafikiri kwa haraka na mcheshi
- Ni mwasilianaji mzuri
- Ni mtu anayependa watu na mwenye kupenda mabadiliko.
- Mwenye kuamua kwa akili na mbunifu
- Hana utulivu
- Ana mipango na malengo makubwa
- Mwenye kubadilika kirahisi
Bonyeza hapa kupata maelezo kamili ya nyota yako NYOTA YA MAPACHA (GEMINI)
Ninahisi, Nasita, Nakwama
“Nina wasiwasi kuhusu Jambo”Naogopa
Bonyeza hapa kupata maelezo kamili ya nyota yako NYOTA YA KAA (CANCER)
Nitafanya, Nitaanza
“Najifanya” Nitasingizia
4 Nyota ya Kaa
Ninahisi, Nasita, Nakwama
“Nina wasiwasi kuhusu Jambo”Naogopa
- Anapenda kukaa nyumbani na kuwa na makazi mazuri yenye kumpautulivu ,usalama na amani
- Anapenda marafiki na familia. ANanpenda kufuatilia historia ya ukoo
- Hisia zake ni za wazi na ni rahisi kujulikana
- Ana huruma
- Ni mwangalifu
- Mkimya na
Bonyeza hapa kupata maelezo kamili ya nyota yako NYOTA YA KAA (CANCER)
5 Nyota ya Simba
Nitafanya, Nitaanza
“Najifanya” Nitasingizia
Kama alivyo simba ni jasiri na mwenye uthubutu. Anapenda kuonekana na watu
Sanaa ni mojawapo ya maeneo ambayo anayamudu na ambayo yanamfanya afanikiwe
Wana maamuzi mazuri na ni waigizaji mahiri.
Sanaa ni mojawapo ya maeneo ambayo anayamudu na ambayo yanamfanya afanikiwe
Wana maamuzi mazuri na ni waigizaji mahiri.
- Ni wenye moyo wa kutoa na wenye upendo mkubwa
- Ni viongozi wazuri na wenye nguvu
- Mwenye matumaini mazuri
- Mwenye kuheshimika
- Mshindani
- Mpangiliaji mzuri wa mambo ya kufanya
- Mwenye mvuto
Bonyeza hapa kupata maelezo kamili ya nyota yako NYOTA YA SIMBA (LEO)
Ninasoma, Nasikitika, nakula, naumwa, Naonewa
“Nina khofu” nitakunywa, nasingiziwa, napoteza, nakunywa dawa, kelele nyingi.
6 Nyota ya Mashuke
Ninasoma, Nasikitika, nakula, naumwa, Naonewa
“Nina khofu” nitakunywa, nasingiziwa, napoteza, nakunywa dawa, kelele nyingi.
Ana mategemeo makubwa juu yake mwenyewe na kutoka kwa watu wengine
Ni mwenye ujuzi na mwenye mafanikio makubwa kazini
Ni mchunguzi na mdadisi wa mambo na mwenye kufanya kitu kimoja kwa wakati mmoja.
Wapangili wazuri wa muda na watekelezaji
Ni mdadisi na mbishi katika kuhakikisha mambo yanafanyika kwa ukamilifu.
Ni wafanya kazi wenye umakini na ni waangalifu katika kazi zao.
Wanajali afya
Bonyeza hapa kupata maelezo kamili ya nyota yako NYOTA YA MASHUKE (VIRGO)
Ninashirikiana, Nakusanya, Naimba, Napenda, Nakumbatia
7 Nyota ya Mizani
Ninashirikiana, Nakusanya, Naimba, Napenda, Nakumbatia
“Nafanya mambo nisiyoyapenda” Nachumbia naunganisha.
Ni alama ya hewa. Mwenye nyota ya mizani anatumia muda mwingi katika kuleta usawa na haki na kusuruhisha migogoro.
Mizani anatumia akili zaidi kuliko nguvu za mwili.
Husimamia haki na usawa
Anapenda sanaa na urembo
Wabunifu wa sanaa
Ni mpenzi wa muziki
Ni muwazi katika kuonyesha upendo
Ana ustadi wa kukabiliana na mambo ya kijamii
Anatoa matazamo wake pale tu anapochokozwa au anapoguswa kihisia
Mpenda amani
Wenye mvuto wa kupendwa
Bonyeza hapa kupata maelezo kamili ya nyota yako NYOTA YA MIZANI (LIBRA)
8 Nyota ya Ng’e
Nataka kufanya, Natamani, Nadhibiti. “Ninashuku” Ninahusudu.Anapenda mambo makubwa na maisha ya mazuri
Mjasiriamali namwenye uwezo wa kukabiliana na vizingiti vikubwa
Anapenda malumbano makali
Wanatumia nguvu
Jasiri
Wastahimilivu
Washindani
Wanauwezo ,
Wachunguzi wa mambo
Wasiri
Ni mpenzi mzuri na mwenye tabia za umiliki
Wanajitegemea
Ni wenye maamuzi
Bonyeza hapa kupata maelezo kamili ya nyota yako NYOTA YA NGE (SCORPION)
9 Nyota ya Mshale
Ninaelewa, Nafahamu yote, hakuna NisilojuaMwanafalsafa na mkusanyaji wa habari
Mwenye uwezo mkubwa kiakili ma anapenda changamoto
Ni mwenye nguvu ambazo humfanya mara zote aende mbele.
Ni mwenye kupenda uhuru
Ni mpenzi mwenye mvuto na anapenda kumridhisha mpenzi wake
Rafiki
Mwenye ari
Hawana utulivu
Waaminifu na wakweli
Wanapenda safari
Bonyeza hapa kupata maelezo kamili ya nyota yako NYOTA YA MSHALE (SAGGITARIUS)
Ninatumia, Nimezoea, naongoza “Sijiamini” Nimebanwa
10 Nyota ya Mbuzi
Ninatumia, Nimezoea, naongoza “Sijiamini” Nimebanwa
Mwenye malengo , mipango na matarajio makubwa
Ni mtatuaji wa matatizo kwa vitendo na mapangiliaji mzuri wa mambo-Mtendaji
Ni mwenye mipango na mfuatiliaji wa mipango yake
Si mshirikishaji mzuri mpaka aombwe au asukumwe.
Ni mpenzi mzuri na rafiki wa maisha
Mgumu kubadilika
Mbishi na asiyekubari kushindwa kirahisi
Mfanyabiashara
Mwajibikaji
Bonyeza hapa kupata maelezo kamili ya nyota yako NYOTA YA MBUZI (CAPRICORN)
11 Nyota ya Ndoo
Ninajua, Nathibitisha “Usinitegemee” NitakwepaNi mbinafsi na asiyependa kufuata utaratibu au sheria.
Wakipekee
Anaejitegemea na hupenda kuwa peke yake
Mwenye huruma
Muona mbali
Mwenye ufahamu wa hali ya juu nma mbunifu
Anafanya marafiki wa aina mbalimbali
Ana utu na mwenye kudai haki
Anapendwa na watu na anategeneza urafiki kwa haraka
Anapenda sanaa na maisha ya anasa.
Bonyeza hapa kupata maelezo kamili ya nyota yako NYOTA YA NDOO (AQUARIUS)
Ninaamini, Ninaota “Ninakwepa”
12 Nyota ya Samaki
Ninaamini, Ninaota “Ninakwepa”
Ni mkweli na mwenye hisia nzito
Hana ubinafsi
Ni mpenzi mwaminifu na rafiki
Mpenda amani
Ana huruma
Anajitoa
Wana ndoto
Wabunifu
Wana aibu
Bonyeza hapa kupata maelezo kamili ya nyota yako NYOTA YA SAMAKI (PISCES)
Wasiliana nasi
Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia email lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.Unaweza kutupata kwa kupitia Email, nambari za simu,kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,
Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.
Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na rakimsspiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.
Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa members pekee;
Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia
Rakims