NAKSHATRA YA MWEZI
Nakshatra ya Mwezi ni nini?Nakshatra ya mwezi ni sawa na kuangalia manazil ya mwezi wakati mtu anazaliwa,
MANAZILI ni nini?
Manazili ni kila siku inayochomoza kuanzia mwezi mchanga yaani muandamo wa mwezi unapoanza na manazili haya huanza; Katika manazili haya kiarabu yapo 28 lakini katika unajimu hususani huu tunaotumia kuangalia basi yapo 27 lakini kwa kuwa tunaingia deep zaidi basi huwa tunaangalia 28.
Tunapokuja kuangalia katika manazili yako mwenye chart hii basi tunakuta ni Manazili ya 5 ambayo kiarabu huitwa Al Haqa ingawa yanakuja kutofautiana katika maelezo tu.
Nakshatra ya Mwezi kwako hujulikana kupitia tarehe sahihi zako za kuzaliwa nayo huonyesha kuwa ni siku moja pekee ambayo mwezi hukaa kwenye nakshatra moja na kila nakshatra moja ina tabia yake.
Kuna umuhimu gani wa kutizama Nakshatra za mwezi katika unajimu?
1: Kujua Asili ya akili na Hisia za muhusika huonyeshwa hapo:
Hii huonyesha jinsi unavyofikiria, unavyohisi na unavyotenda (how you react)
2: Tabia zako: – Machale yako na jinsi unavyoweza kushtukia kitu na unavyokiendea huonekana hapa ikiwa ni pamoja na unayopenda na usiyopenda.
Kuendana kwenye mahusiano – Kuendana au kufanana kinyota za Jua (Sun sign) hakumaanishi usahihi zaidi kama ikivyo kwa Nakshatra Ikiwa tabia za nje (kimwili) zipo kwenye Sun Sign basi tabia za Moyoni kwa mtu zipo katika Mwezi wake.
Hivyo hata mtu akikujia kutaka mahusiano na wewe kama ni Mchungaji mfano au shekhi basi utamuona kama ni mchungaji au sheikh kupitia Sun sign (Zile mnaita nyota yako) lakini ukitaka kujua ukweli wake mfano Mchungaji lakini malaya basi tunaingia kwenye Nakshatra ya Mwezi.
Njia ya Maisha na Majaliwa yako – Tunaweza kuona kupitia hapa na mafanikio yako ya kiroho.
Mpangilio wa sayari zako – Ikijulikana Nakshatra yako ni ipi basi mpangilio wako wote unaonekana.
Ardra
Ukiwa umezaliwa katika nakshatara ya Mwezi ikiwa kwenye Ardra basi moja kwa moja tunaona kuwa;Moon Nakshatra Mula
Mfano pia tukija kwenye Nakshatra yake ikiwa kwenye Mula basi moja kwa moja ni mtu ambaye yupo katika kwenye position kubwa na yenye nguvu sana katika mabadiriko au kubadirisha hali ya hewa sehemu ya biashara au kazi,
Kwanza kabisa fahamu nini maana ya Nakshatra. Nakshatra ni Position ya Mwezi ambayo ni sawa na vile ambayo unaona position ya nyota za Jua mfano makundi nyota 12 basi katika unajimu kuna kitu au kipengele kinaitwa Nakshatra ambacho chenyewe huwa tunaangalia manazili ya Mwezi wakati Muhusika anazaliwa.
Hivyo mwenye Nakshatra ya Mula huyu ni mtu ambaye akianza biashara au kazi basi moja kwa moja tunaona kuwa ndio sawa na yeye kuwa kaanza kufanikiwa.
Nakshatra yako ikiwa kwenye Mula basi fahamu moja kwa moja ya kuwa utakuwa na sifa ama hali zifuatazo; Kwanza kabisa Jua misingi ya Nakshatra yako ikiwa kwenye Mula;
-
Mula Maana yake ni Mzizi
-
Nyota ya Mula ni: Mshale
-
Degrees zake: 0°00' – 13°20' Nyota ya Mshale
-
Sayari yake: Ketu (ambayo ipo kusini mwa mzunguko wa mwezi)
-
Alama yake: Mizizi iliyojifunga/Iliyofungwa
-
Nguvu yake; – Uharibifu na Mapinduzi
🌕 Katika upande wa hisia zake:
-
Hisia zake za ndani kabisa: Watu hawa ni wenye kuhisi vitu kwa undani sana na hata unapokuwa na jambo lako hulichukulia kama ni la kwake, Ukilia anaweza kulia pamoja na wewe.
Nao ni moja kati ya watu wenye imani sana ya kuamini kuwa kila unachofanya kumfanyia mwingine basi utalipwa hivyo hivyo -
Mabadiriko katika roho zao: Ni watu ambao wao wapo teyari teyari kwa majanga, nao wapo radhi kuachana na yoyote vyovyote na hawaoni shida kuanza jambo upya, ikiwa ni pamoja na kujiponya maumivu yao wao wenyewe. Wanapoumizwa huwa hawabadiriki tabia zao, Isipokuwa
Sifa yao nyingine ni watu ambao sio rahisi kuumizwa kulingana na uvumilivu na subira walionayo
Ukitaka uwakosee kiimani; waletee hoja za mafumbo, Kutaka kuwatawala au kuwataka wakae kama kimakundi. Hapo ni udhaifu wao kiroho na wapo radhi kugeuza dini.
Jambo kubwa kuhusu wao ni watu wenye kutaka ukweli tu. Na wanapenda kujua ukweli wa kitu kwa kuingi ndani yake zaidi.
🌿 Sifa zao
- Ni watu wenye welevu na falsafa nzuri ya kazi na maisha
-
Kipaji cha asili cha kuponya walichonacho – wanauwezo mkubwa wa kuongea au kusikiliza roho zingine au kuita na kuzungumza na mizimu.
Ni watafiti bora wakiamua kutafuta jambo
- Yakiwakuta majanga ni sawa na imewaijia charge ya maarifa zaidi
- Ukitaka kuwaangamiza basi huibuka kwenye maangamizi yako na unaweza usiamini ni mfano wa Ndege anayekufa kisha mwili wake unazaliwa upya kutoka kwenye moto.
⚠️ Majanga katika maisha:
-
Majanga yao katika maisha ni kupoteza au kukosa uelekeo mwanzo wa maisha: (Hususani kupoteza mama au Ardhi yao)
-
Ni watu ambao ni wakali linapokuja suala la hisia
-
Hung'ang'ania jambo na anaweza asiachie kirahisi au kukubaliana na hali
-
Wakati mwingine ni mtu wa Kujitenga au kuwa na moyo baridi katika mahusiano.
🧬 Mapito yao kwenye maisha:
Mula Nakshatra ni wenye kuhusishwa na kuvunja mapito ya maisha yao, Hususani katika maagano ya kurithi mambo ya kwao, wao huyakataa na kutaka kujiepusha na laana za ukoo na kuishi kivingine na ndugu zao,
Mwezi unapokuwa kwenye position hii basi moja kwa moja Mwenye position hii ni mtu mwenye kuamua kung'oa udanganyifu wa maswala ya kiroho, laana za mababu, au imani zenye mipaka yaani mambo ya masharti, na kuamua kuanza upya.
👁️🗨️ Watu wa position hii:
-
Ni watu wenye mizimu binafsi ambayo ni mikali (Yake binafsi sio ya mababu)
-
Ni watu Wanavutiwa na mambo ya kiroho, saikolojia, uchawi, au hata unajimu.
-
Kuumizwa mapema katika maisha kama kutelekezwa huwapa experience kubwa ya maisha
-
Ni watu wasioogopa giza nao ni wenye kung'ara kupitia Giza hilo.
🪐 Jambo la ziada:
NAKSHATRA YA MWEZI KATIKA Mrigashira
Nakshatra ya mwezi ni sawa na kuangalia manazil ya mwezi wakati mtu anazaliwa, MANAZILI ni nini?
Manazili ni kila siku inayochomoza kuanzia mwezi mchanga yaani muandamo wa mwezi unapoanza na manazili haya huanza; Katika manazili haya kiarabu yapo 28 lakini katika unajimu hususani huu tunaotumia kuangalia basi yapo 27 lakini kwa kuwa tunaingia deep zaidi basi huwa tunaangalia 28.
Tunapokuja kuangalia katika manazili yako mwenye chart hii basi tunakuta ni Manazili ya 5 ambayo kiarabu huitwa Al Haqa ingawa yanakuja kutofautiana katika maelezo tu.
Nakshatra ya Mwezi kwako hujulikana kupitia tarehe sahihi zako za kuzaliwa nayo huonyesha kuwa ni siku moja pekee ambayo mwezi hukaa kwenye nakshatra moja na kila nakshatra moja ina tabia yake.
Kuna umuhimu gani wa kutizama Nakshatra za mwezi katika unajimu?
Asili ya akili na Hisia za muhusika huonyeshwa hapo:
Hii huonyesha jinsi unavyofikiria, unavyohisi na unavyotenda (how you react)
Kuendana kwenye mahusiano – Kuendana au kufanana kinyota za Jua (Sun sign) hakumaanishi usahihi zaidi kama ikivyo kwa Nakshatra Ikiwa tabia za nje (kimwili) zipo kwenye Sun Sign basi tabia za Moyoni kwa mtu zipo katika Mwezi wake. Hivyo hata mtu akikujia kutaka mahusiano na wewe kama ni Mchungaji mfano au shekhi basi utamuona kama ni mchungaji au sheikh kupitia Sun sign (Zile mnaita nyota yako) lakini ukitaka kujua ukweli wake mfano Mchungaji lakini malaya basi tunaingia kwenye Nakshatra ya Mwezi.
Njia ya Maisha na Majaliwa yako – Tunaweza kuona kupitia hapa na mafanikio yako ya kiroho.
Mpangilio wa sayari zako – Ikijulikana Nakshatra yako ni ipi basi mpangilio wako wote unaonekana.
Hivyo kwako
-
Nyota ya Mwezi (Rashi): Ng'ombe
-
Nakshatra ya Mwezi: Mrigashira
-
Miguu yake: 3
-
Sayari ya Nakshatra: Mirikhi
Hivyo hii inamaanisha moja kwa moja kwa upande wako; Mwezi kwako ulikuwa umeingia kundi la Mrigashira nayo ipo katika miguu mitatu ambayo inakupelekea zaidi kwenye Hisia zinazotokana na akili ikiwa ni pamoja na majaliwa yako; Hivyo elewa zaidi ya kwamba;
Katika Nakshatra yako ya mwezi inaonyesha ipo kwenye Mrigashira
NAKSHATRA YA MWEZI IKIWA KWENYE MRIGASHIRA
Ambayo mara nyingi ipo chini ya Sayari ya mercury hivyo ikiwa katika position hii kwako inatuonyesha kuwa ni mtu maalum uliye kiakili sana, ya mwenye akili ya haraka, ya kudadisi, na mara nyingi ni mtu usiye na utulivu wa kiakili.
Hii hukupelekea kuwa ni mtu ambaye akili yako inakuwa ni nyepesi sana katika kutambua na kuelewa vitu, Kukupa uwezo mzuri wa kuongea na watu, kufundisha ikiwa ni pamoja na kuwasiliana, kujifunza, kusafiri pamoja na kuwa muandishi mzuri.
Tukianza na asili ya akili yako;
Katika position hii akili yako inatuonyesha kuwa ni mtu ambaye mchambuzi, mwenye msisimko ukipata mawazo mapya na husisimka kwa mambo yanayotumia akili zaidi hata starehe yako ni kwa vitu vyenye kutumia akili.
Ni mtu mtafiti wa elimu mpya, kuuliza maswali nyeti (Kwa kina zaidi) si mtu wa kupenda kuongea ongea na watu wenye kutumia akili kidogo katika maongezi. Hisia zako ni zenye kuamshwa na mambo ya kiakili pekee.
Kwenye maongezi:
Ni mzungumzaji mzuri.
Unaweza kuvutiwa zaidi na uandishi, Kuongea mbele za watu, kwenye media au kutengeneza makala (Content creation).
Unatabia ya kufiria kwa haraka, kuongea haraka na mwenye kwendana na hali za watu.
3. Mahusiano na Hisia
Tunapokuja kwenye mahusiano na hisia unapokuwa na position hii ya Nakshatra basi tunaona kuwa ni mtu ambaye ni mwenye hisia lakini hapo kwa hapo ni mwenye kujitenga na hisia wengine wakikuangalia katika hisia hukuchukulia kama vile mtu ambaye haeleweki anataka nini hasa.
Ingawaje wewe ni mtu ambaye unapenda kuwa na mwenza mwenye akili sana, muongeaji na mwenye akili iliyochangamka.
Mara nyingi ni mtu ambaye hukuta unajiumiza kihisia kutokana na kufikiria sana
Ni mtu ambaye umebobea katika Media ukiamua kuanza, uandishi, ikiwa ni pamoja na urushaji matangazo.
Shida ulizonazo kwenye Nakshatra hii ni:
1: Tunakuona kama mtu ambaye asiyepumzika.
2: Mwenye kuchunguza sana jambo kabla ya kulikubali kiakili na kihisia
3: Rahisi kupandwa na hasira ukilazimishwa kuelewa jambo ambalo haliingii akilini.
Upande wa kiroho:
Nakshatra yako ikiwa katika Mrigashira mara nyingi huonyesha mtafiti; Hivyo mwenye nakshatra hii tunatarajia ni mtu ambaye hamalizi jambo hadi pale atakapoona Ukweli wake, uzuri wake na maana yake hasa ni nini.
Mwezi wako katika position hii unatuonyesha kwamba ni mtu ambaye roho yake ni yenye kutokuridhika na mara nyingi hutaka zaidi kutafuta na kutafuta na hata hivyo ni mtu hujui wakati mwingine unatafuta nini hasa (Inatokea Automatic)
Mwezi wako katika position hii unatuonyesha kuwa moja kwa moja ni mtu ambaye unaweza kuutambua wito wako zaidi wa muda husika ikiwa utakaa sehemu ya asili kama vile ukijitenga mashambani au porini, ukiwa sehemu ya kimya zaidi au ukikaa riadha kivyako.
Soma kila mwezi unapokuwa mpevu:
“Surah al Araf ayah 54” Ikiwa ni Mwezi mpevu au Jumatatu na unashida yoyote ile ambayo huwezi kuitimiza basi soma mara 108 huku ukitia ubani hii ni ya kwako pekee mwenye Nakshatra ya Mwezi katika Mrigashira.Ikiwa unataka muongozo wa jambo lolote basi hakikisha unafanya meditation kwa utulivu wa akili sehemu ambayo hakuna sauti yoyote.
hakikisha kuwa hunywi sukari wala kinywaji chochote chenye caffeine usiku kwa maana hivi ni asili ya mtoto kwenye mwili na kwa wenye mwezi katika position hii ni adui kwao. Basi kwa mwenye Mwezi wa nakshatra ya Moto kwao ni kheri zaidi kunywa vinywaji hivi linapoingia giza lakini wale wenye baridi na maji ni mbaya.
Hakikisha haipiti wiki bila kutembelea sehemu ya maji au vyanzo vya maji. Ili kuweza kujaza nguvu yako ya kiroho.
Ikiwa kipindi kimefika cha Nakshatra yako ya mwezi katika mwaka basi hakikisha unavaa Kito cha Moonstone au Pearl katika siku mwezi mpya umeandama na usivae vipindi vyovyote tofauti na kipindi chako kwa mwaka.
Muendano na Muongozo wako:
Hisia kwako ni kitu cha siri sana hususani kimejificha nyuma ya akili yako hivyo; hakikisha unaelewa ni nini hasa kuendana na sherehe za kiakili; hakikisha watu wako pekee unaoongozana nao ni watu wasiopenda vitu vya kijinga, hakikisha haipiti siku bila kuingiza neno lolote la busara katika akili yako.
Usiongee hovyo au sana au kwa sauti hadi pale unapokuwa na uhakika kuwa ni muda sahihi wa kuongea. Ikiwa utafuata vema nakshatra hii kwako basi ni yenye maajabu mengi na hutatumia nguvu nyingi katika kufanikiwa mambo yako.
SHATABHISHA
Tunapokuja kwenye Nakshatra yako ya Mwezi hii inaonekana Ipo kwenye Shatabhisha Hii kwako inakumodify katika namna ifuatayo;
🪐 Mtazamo wake kwa ujumla ni kwamba
Maana yake: Shatabhisha = "Mamia ya nyota tabibu"
Alama yake: Duara iliyotupu au nyota 100
Historia za kale za kihebrania za kuamini miungu: Walikuwa wakiamini ni Mungu wa Tiba kupitia Maji
Sayari tawala: Huwa tunaita Rahu (Iliyopo uelekeo wa kuliani kaskazini mwa mwezi)
Namba yake ya Nakshatra: 24 hadi 27
Nyota inayokuwa inamulika: Ndoo ambayo ni A ♒︎ (6°40’ – 20°00’)
Basi hii ni Nakshatra ambayo inaingia sana kwa undani kwenye maswala ya Maajabu ajabu(Majini na Vitu visivyojulikana), Tiba, Siri na Sayansi ya kiroho.
🌙 Tabia za wenye nakshatra hii
Watu wenye Shatabhisha manazili haya ya mwezi ni:
Wenye kufikiria sana, wasiri wenye aibu iliyojificha, wamekaa kiroho zaidi.
Wanavutiwa na elimu za siri, Unajimu, Nguvu za kiroho kupitia sex (Tantra), Meditation, Saikolojia na tiba kwa ujumla.
Ni mtu ambaye unaweza kuwa mwenye kupenda upwekee, na kufurahia upweke na kutafakari vitu vyako vya ndani.
Akili yako ni ya maendeleo na fikra yako imekalia kwenye maendeleo zaidi, Hupendwi kuongozwa au kutawaliwa.
Mara nyingi ni mtu wa Maajabu — watu inawawia vigumu kuweza kukujua vizuri.
Machale makali sana na Uwezo wa nguvu za miujiza.
Muda mwingine udhaifu wako ni mtu wa kubadirika badirika kitabia (mood swings), hisia kugeuka ghafla ghafla. Kwa sababu ya Rahu (Kupatwa kwa Mwezi) kukutawala upande wako huu wa Mwezi.
🌌 Nguvu yako
Una asili ya uponyaji (Kuponya mwili, akili au Roho)
Mtafiti Bora — mwenye uwezo wa kuchimba sana kupata ukweli wa jambo.
Uwezo wa kujitenga au kuachilia jambo bila kujivuruga kihisia (Kujitenga hata kwenye mahusiano kwa amani).
Unaweza kutenda mageuzi makubwa, Na kuleta mawazo ambayo hata hayakufikirika.
Una uvumilivu wa hali ya juu kuwa mpweke - pia una starehe zaidi ukiwa peke yako.
⚠️ Changamoto za Position hii (Changamoto zako)
Kujitenga — Muda mwingine huwa unajihisi upweke hata ukiwa kwenye kikundi cha watu
Unaweza kupotea kwa kuwa na mawazo kupita kiasi, depression, au kutoroka jambo.
Msukumo mkubwa wa Rahu → mwelekeo wa uraibu(addictive) au mawazo ya ajabu.
Kuwa na hisia baridi au kujitenga katika mahusiano.-
💖 Mapenzi na Mahusiano
Kwenye mapenzi ni mtu unapenda kuficha hisia zako → Mwenza wako anaweza kuhisi kutengwa na wewe.
Unapenda mtu ambaye anaweza kukuelewa undani wako na asiye kulazimisha kufunguka upesi/ au kusema mambo.
Mara nyingine huvutiwa na wapenzi wasio wa kawaida au wasio na hali ya kitamaduni (Wenye tabia za kigeni na wewe)
💼 Kazi zako
Unajimu, Tiba, Madawa, Saikolojia, Hizi ni kazi ambazo zinakufaa sana.
Teknolojia, Anga, Utafiti na Sayansi ya kichawi (Uganga/kujua habari za uchawi usio na madhala) hizi ni kazi unapenda sana.
Unavutiwa na kazi yoyote inayotaka ukae peke yako na Uweke Fokasi katika kazi hiyo.
🍀 Bahati zako
Ruling Planet: Rahu (Kaskazini mwa Mwezi/ Katikati ya kupatwa kwa mwezi)
Namba za bahati: 4, 7, 8
Rangi za Bahati: Blue, Kijani kibichi na Nyeusi.
Lucky Stone: Gomed (Hessonite Garnet) – na hii ni kama tu chart yako nzima ya unajimu itakubaliana nalo.
Kwa kifupi zaidi; Mtu ambaye ana Nakshatra ya Mwezi katika Satabhisha (Manazili ya 24 katika mwezi) Basi tunaona kuwa ni mtu ambaye ni wa ajabu kiasi, mwenye uwezo wa kuponya lakini pia ni msiri sana katika mambo yake. Ndani yako umebeba hekima kubwa sana na unaweza tu kuwafungukia wale uliowaamini sana pekee.
Hii ndio Nakshatra yako ya Mwezi na Haya ndio maelezo yako.
UTTARASHADHA
Nakshatra hii huwakilishwa kwa alama ya pembe za ndovu, Nayo ni moja kati ya nakshatra 27 za mwezi ambayo hapa tunaona kuwa;Chini ya Nyota ya Mshale katika degree 26 hadi 10 Capricorn. Na asili yake ni takatifu au thabiti na ipo katika makundi (Fixed).
Nguvu yako;
Hisia kali za uwajibikaji.
Mamlaka ya asili na charisma yako.
Ni mtu ambaye mwenye uvumilivu na uwezo wa kushinda vikwazo.
Mambo ya kiroho na hekima ya kutenda kwa ujumla.
Mitihani yako:
Ni mtu ambaye unaweza kuwa ni mgumu kupita kiasi au ya kusisitiza unapokuwa unataka jambo lako.
Unaweza kuja kuhangaika na maswala ya kujielezea kihisia kwa wenza ambayo itakufanya kuonekana ni mwenye hisia za mbali au huna ukweli katika hisia zako.
Msukumo wa kutaka kufanya mambo kwa ukamilifu utakusumbua sana, Mara nyingi jinsi utakavyokuwa unataka kitu kionekane bora zaidi ndio njia pekee ambayo itakuwa inasababisha wewe kuishia kudhalaulika.
Ramani ya Maisha (Njia ya Maisha)
Mara nyingi mafanikio yako kimaisha yanaangaliwa sana kupatikana kupitia jamii na kuonekana kama kiongozi, mwalimu au mtawala wa sehemu husika.
Nakshatra hii huwaletea waliozaliwa katika position hii na hata ikifika kila mwezi katika position hii basi wao huwa na nafasi kubwa ya ushindi, Chochote unachokuwa unashindania siku hii mwezi ukiwa kwenye position hii basi unaweza kushinda.
Watu wenye nakshatra ya mwezi ikiwa Uttarashadha ni wenye mihemko thabiti, nidhamu, na misingi ya kanuni.
Hawapendi drama na wanapendezwa zaidi na uwazi, uaminifu, na utaratibu katika mahusiano na mazingira.
Muda mwingine ni wenye kujificha kuonyesha hisia zao na hawapendi kujielezea sana kwa watu. na hili mara nyingi hukufanya uonekane ni mwenye ubinafsi wa mambo yako au kujitenga na wengine (Msiri)
Nguvu iliyoko ndani yako ni kubwa sana ambaye inapelekea muda mwingine hata kwenye mazingira magumu unakuwa upo na hali ya kawaida,
Mahusiano yako na familia yako:
Mwenye nakshatra hii tunakuona kuwa ni kama mtu ambaye mwenye kutafuta kwa nguvu zote uaminifu na kuaminiana katika mahusiano. Hivyo basi kwenye ndoa ni mtu ambaye huingii kwenye ndoa isipokuwa na mwenza ambaye unaamini ni mtu ambaye ni sahihi katika majukumu yake na hii hupelekea wewe kuchelewa kuingia kwenye ndoa.
Katika familia tunaona kuwa;
Kazi na Ajira yako katika maisha
Kazi nzuri kwako ni;
utawala, serikali, sheria, mafundisho, uongozi, utafiti, kijeshi, na kiroho.
Ni mtu ambaye unafanya kazi bora zaidi pale ambapo unapofanya kazi unayohisi ni ya wito zaidi au ya kujitoa zaidi kwa ajili ya jambo kubwa.
Hiyo ni kutokana na kuwa; Nakshatra hii ina ahidi Ushindi wa Milele, Mafanikio huja baadae na huwa ni ya moja kwa moja na yenye faida kubwa sana.
Na ndio imani ambayo kwako unatakiwa kuifuata tofauti na wenye Nakshatra zingine wanaweza kuchanganya Imani.
Utimilifu wa kweli huja unapolinganisha malengo ya kibinafsi na manufaa ya pamoja.
Sababu yako kuu ya maisha ya wewe kuwa duniani inahusisha zaidi wewe kuwa mwanga elekezi au mtu mwenye mamlaka ambaye anashikilia haki na ukweli kwa ajili ya wanaomfuata nyuma.
Nakshatra ya Mwezi UTTARA PHALGUNI
Tunapokuja kwenye manazili ya mwezi au Nakshatra kwako wewe ni nakshatra ya Uttara Phalguni (Uttaraphalguni) ambayo ni manazili ya 12th katika manazili ya mwezi ambayo kiarabu pia tunaweza kusema Al Sarfa hii kwako inaonekana kuwa katika Utarra Phalguni wakati unazaliwa au tunaweza kusema Mwezi ulikuwa daraja la 12 wakati unazaliwa.
Kwako wewe tunapoangalia kipengele hiki basi moja kwa moja tunaona kuwa hii Alama yake inaashiria upande wa nyuma wa miguu ya meza au kitanda.
Yani kwa maana nyingine ni Manazil yenye kwenda pamoja yaani pacha kwa ikiwa inahusiana pia na Mikataba, Umoja na Ushirika.
Sayari yake tawala huwa tunaona ni Jua. Fahamu ya kuwa katika elimu ya unajimu jua huwa tunalipanga kama sayari, Ufuatao ni uchambuzi wa Nakshatra yako.
Tabia zako mwenye Nakshatra hii
Nzuri:
Hisia Zako:
Hisia za mwenye manazili hii tunaona kuwa ni mtu ambaye mambo yake mengi huja kwa ukamilifu pale tu anapokuwa thabiti yaani asipoyumbishwa, akiwa na mwenza na akiwa katika mahusiano ya kijamii.Kazi za Mwenye Nakshatra hii:
Nakshatra hii inapendeza sana kwa muhusika wake kufanya kazi za pamoja yaani kushirikiana na Mwengine hata kama ni Kampuni.
Uwanja wa kawaida kwako: Sheria, Ushauri, Sanaa, Ualimu, Serikali au kazi za ubunifu wa pamoja.
Hisia kali za haki na usawa zinaweza kukupelekea kwenye kujitoa zaidi katika sababu za kijamii na ubinadamu.
Nguvu za Uhusiano:
Nguvu za uhusuano katika nakshatra hii
Ni mbora zaidi kwenye mahusiano ya muda mrefu na mara nyingi huvuta sana wenza ambao ni wawajibikaji na wenye kukusaidia.Ni mwenye kustawi sana pale ambapo mwenzi wako anashiriki maadili yako ya uaminifu, wajibu, na kuendana nawe.
Unaweza kuteseka kama mahusiano yanakuwa yanakosa usawa na kujitolea.
Upande wa kiroho
Kiroho, unaweza kukua sana ikiwa utafanya shughuli za kiroho wewe mwenyewe, na kuwahudumia wale unaowapenda katika maswala ya kiroho.
Moon Nakshatra Aswini
Kwa kifupi tunaweza kusema manazili hii imekaa kwenye nyota ya Punda (Kondoo) hivyo ni kusema kwamba ni mtu ambaye una manazili ya kwanza kabisa katika manazili 28.
Tukianza na sifa za Manazili hii.
Mwezi unapokuwa umeingia kwenye Manazili hii ya Ashwini (ambayo kiarabu huitwa Sharatain), basi mara nyingi humuonyesha mtu aliyezaliwa chini ya manazili hii kuwa ni mtu wa nguvu, mwenye kupania mambo, Ikiwa ni pamoja na Mjazo wa Maisha.
Ni mtu ambaye tunatarajia watu wakikuona wataona ni mtu ambaye umejitosheleza kimaisha na uliye hai usiyetetereka.
Kama ilivyo Manazili hii ya mwezi kuwa ya kwanza basi ndivyo ambavyo tunaona kuwa ni mtu ambaye mwenye kuwazidi wengi katika mambo mengi.
Manazili hii hutawaliwa na Ketu ambayo ni uelekeo wa kusini mwa Node ya mwezi. Na huashiriwa kwa kichwa cha farasi.
🌙 Tabia zake
-
Huwa na Muonekano wa kichwa cha farasi yaani farasi wawili, Ambaye katika imani za wenye kuamini miungu basi walikuwa wanaamini kuwa huyu alikuwa ni mtabibu wa miungu (Majini) Hivyo unapokuwa na manazili hii tunaona kuwa inakuwakilisha kama mtu ambaye ni mwenye kuponya, kuleta uhai sehemu unayokuwepo na wepesi wa mambo.
-
Sayari yake tawala ni: Ketu ambayo hii inatuonyesha kukupa maono ya kiroho na kujitenga, wakati tabia za kondoo zinakuzidishia ujasiri na msukumo wa kutimiza mambo yako.
-
Maada yake ni: Moto
-
Asili yake ni : Tukufu
🌟 Tabia inazokujaza na kukuletea
-
Nguvu na Uwezo wa Manazili hii: Watu waliozaliwa kwenye Nakshatra hii ya Mwezi ya Ashwini ni watu ambao wapo upesi, wenye hali ya kuwa na hiari, na yenye mwelekeo wa vitendo zaidi. Ni wenye kupenda kuanza jambo jipya na kulipeleka Upesi.
-
Machale ya kuponya: Ni watu ambao wamejaliwa kuponya, kutibu, kihisia au kiroho.
-
Roho ya Ujana: Wenye manazili hii ya Ashwini tunaona kuwa ni wenye muonekano wa umri mdogo kuliko uhalisia. Na wenye kubeba shauku au mihemko ya kitoto.
-
Wenye fikra za maendeleo: Wenye Nakshatra hii ya mwezi tunaona kuwa ni watu ambao hawapendi kutawaliwa au kuongozwa (Kupelekeshwa) na mara nyingi wao hupenda zaidi uhuru katika mambo yao.
-
Katika misaada na kujitolea: Ni wenye msukumo sana wa kusaidia watu wengine, hasa hasa wanapokuwa kwenye majanga.
💕Mahusiano
-
Wana shauku na waaminifu lakini wanaweza kutenda bila kusita kwa upendo.
-
Mara nyingi ni wenye kuhitaji washirika ambao wanaweza kuendana na kasi yao na kuheshimu uhuru wao.
💼Kazi na Kipaji
-
Ni watu bora katika nyanja zinazohitaji kufanya maamuzi ya haraka na juhudi—dawa, uponyaji, michezo, teknolojia, ujasiriamali, na uvumbuzi.
-
Mara nyingi wengi wenye manazili hii ni wenye kufanikiwa zaidi katika kuanzisha jambo au kulifuatilia kwa ukaribu jambo lao
🕉️Matarajio ya kiroho
-
Utawala wa Ketu katika manazili hii huleta shauku katika ukuaji wa kiroho, kujitenga, na mazoea ya uponyaji.
-
Meditation na shughuli za kutuliza akili husaidia kusawazisha asili yao ya moto.
Purva Bhadrapada Nakshatra (Manazili ya 25 ya Mwezi)
Tunapokuja katika nakshatra yako (Manazili yako ya mwezi) tunaona kuwa kwako ipo kwenye manazili ya 25 ambayo hii inatuonyesha kukuletea mchanganyiko wa mambo ya maajabu kiroho/kichawi na uelewa wako mzima kuhusu hayo.
Hali ya manazili haya kwa ujumlaSayari yake tawala tunaona ni Jupiter: (Sayari ya Bahati)
Alama yake ni: Miguu ya Mbele ya upanga au kitanda cha mazishi
Nyota zake ni Ndoo degree (20°00’) kwenda Samaki (3°20’)
Hali yake ni: Utu au ubinadamu
Jinsia: Kiume
Maada yake ni: Moto
Tabia za wenye Nakshatra hii:
Ni wenye mawazo mapana, Falsafa na Ubinadamu.
Nia yako — uwezo wa hisia za kina na kujitolea au shauku kubwa.
Wana vutiwa sana na elimu za kiroho, Kichawi, Unajimu na Maswala ya Metafizikia (kuamini visivyoonekana)
Ni watu wenye Kuwa na dira yenye nguvu ya maadili, lakini inaweza kukabiliana na migogoro ya ndani ya roho zao.
Wanaongea kwa Busara; mara nyingi huwavutia wafuasi au watu kuwapenda kuwasikiliza.
Hisia zao na Muonekano wa nje
Wenye manazili haya tunaona kuwa ni watu ambao wana uwezo mkuwa wa kutengeneza hisia ambazo zinaweza kuwaongoza kutambua undani wa mambo kama vile - Ukweli wa watu husika kwa kuwasikiliza na kuwaangalia tu.
Wana nguvu ya miujiza ambayo imejificha katika kuhisi jambo na likawa kweli hata kama lipo magharibi mwa dunia na yeye yupo mashariki
Ni watu wenye kutafuta ukweli tofauti na maisha ya kidunia, na mara nyingi hubadirika kwa mifumo yao ya maisha pale wanapokuwa wameamka kiroho.
Wana hali ya kuingia ndani zaidi kuhisia na kujua ukweli wa roho ya mtu kwa kuungamanika nae kwa ukaribu. Muda mwingine ni watu ambao hawaeleweki katika mawazo yao au wanapokuwa serious na jambo fulani.
Kazi zinazowafaa sana ni kazi zinazohusisha maswala ya kiroho, kutibu, ualimu, unajimu, saikolojia, utafiti, uandishi au utendaji.
Kazi yoyote inayowataka kuwa ni wenye mtizamo mkubwa wa kiroho na kiimani basi wao wanaweza kuitenda vema na hata hivyo ni wenye huruma na familia zao na ndugu zao.
Ubaya wao
Ni watu ving'ang'anizi wenye kujitenga na kujidhuru wao wenyewe wanapokuwa hawaeleweki kihisia. Wakati fulani, inaweza kuwa na tamaa au kujisikia kutengwa.
Ili kwenda sawa na manazili haya inabidi kusawazisha malengo ya kiroho na maisha ya vitendo. Ukichanganya unakuwa una haribikiwa hususani kila mwezi unapoingia katika manazili haya.
ASLESHA
Tukija katika Moon Nakshatra Yako:
Kwanza kabisa fahamu kuwa ipo katika 28:17 Degree Aslesha Cancer 8th House
Ya kwamba hii nakshatra yako ipo katika Aslesha (Manazili yako ya Mwezi yako katika manazili ya 9 katika manazili 27 ya mwezi) Tukirejea kwako katika position hii basi inaonyesha ya kwamba;Kwanza kabisa fahamu ya kuwa position hii Mwezi upo katika Nyota yake husika ambayo ni Cancer (Kaa) na upo katika manazili ya 9 katika miguu 4 na mlango wa nne katika Degree ya 28:17.
Mwezi wako upo katika:
-
Kaa (Nyota yake unapotawala → una nguvu sana)
-
Aslesha Nakshatra (nguvu ya nyoka, kubobea kwa saikolojia, machale/ufahamu)
-
Pada 4 ( Miguu minne katika samaki → inaonyesha kiroho, maajabu, mtu mwenye huruma)
-
8th House (Mlango/Nyumba ya 8 mabadiriko, uchawi, ulimwengu wa giza, kina zaidi cha sirini)
-
D degree zake: 28°17' → Manazili iliyochelewa (Inakaribia katika mpaka wa Alama/Nyota ya Simba → Inatoa mvuto wa karama na nguvu za kihisia).
Hivyo hii huonekana kama ni moja katika ya Position ya Mwezi ambayo ni yenye nguvu zaidi katika uangalizi wa chart ya mtu.
🔱 1. Nguvu ya Degree zake (28°17')
Katika Degree 28°17' Kaa, Mwezi wako unakuwa:
-
Karibu na mpaka wa alama ya simba
-
Ingawaje bado umejaa katika manazili ya 9 Aslesha
-
Hupata hila za msukumo wa simba ambazo ni kama vile:
-
Nguvu ya kuwa sehemu (Unapotokea)
-
Muonekano wa Kiongozi
-
Mmiliki wa hisia
-
Sifa za ndani
-
Tamaa ya kuheshimiwa
-
Pia:
-
Wewe ni moja kati ya watu wenye nguvu sana ya miujiza ya machale/hisia ya kitu kikawa.
🐍 2. Maana ya Aslesha Yako
Aslesha = fahamu ya kuwa katika Lugha ya kihindi ni nyoka aliyejikunja, hii inakuwa ni alama ya kuwasilisha kuwa ;
-
Una nguvu ya ulaghai
-
Unaweza kuchota mtu akili.
-
Nguvu kali ya Hisia
-
nguvu ya mabadiliko
-
Hekima iliyojificha
-
Uwezo wa kuponya au kuharibu kabisa (Inategemea na umekomaa vipi kihisia)
Hivyo basi unakuwa ni mtu ambaye:
-
Una uwezo wa kusoma akili ya mtu na hisia zake
-
Nguvu kali ya Machale
-
Aura kali isiyoeleweka kirahisi.
-
Kumbukumbu kali ya kihisia
-
Kipaji asilia cha kufichua siri.
🌊 3. Miguu minne katika Samaki (Maswala ya kiroho na Uwezo wa miujiza)
Miguu hii minne inatuongezea katika kukuona kuwa ni mtu ambaye:
-
Mwenye huruma
-
Mtenda uchawi uchawi/Vitu vya ajabu
-
Kuota ndoto zikatokea au mawazo
-
Mtu ambaye upo kihisia
-
Akili kali ya kiroho
-
Mkarimu kiimani
Ikiwa utaelemea katika upande huu zaidi basi moja kwa moja inakupelekea kuwa:
-
Mponyaji
-
Mwenye Huruma na wenzio
-
Kuwa na roho karibu ya kujitoa.
-
Mtu ambaye unakuwa mshairi mwenye hisia kali.
Katika Miguu yote ya Aslesha basi mguu wa 4 ambao ni huu wako ndio huwa tunaita ni mtu ambaye yupo kiimani na kiroho zaidi kuliko Aslesha wengine wote (Waliozaliwa katika manazili hii).
🜂 4. Mlango wa nane (Mlango wa Kifo na Ufufuo ukiwa na position huu/ Mlango wa Giza)
Mwezi katika mlango huu wa nane tunaona kuwa:
-
Unakupelekea kuwa ni mtu mwenye maisha ya kihisia sana.
-
Kupata mabadiriko ya kimaisha kupitia majanga.
-
Kuvutiwa sana na mambo ya siri.
-
Nguvu za miujiza za machale
-
Kuvutiwa na elimu ya kiroho au uchawi, Nguvu za kingono na unajimu.
-
Uwezo mkuwa wa kushinda mitihani ya kihisia.
-
Kujifunza kwa majuto baada ya kuumizwa kihisia
Akili yako mara nyingi inavutwa katika:
-
Mambo ya siri
-
Saikolojia
-
Kufa na kuzaliwa pengine
-
Machale/kuelewa jambo bila kufikiria
-
Maono usiyojua yanatoka wapi
-
Maarifa ya siri/Giza
Basi wengi wenye position hii utakuta ni Wanajimu, Wenye maono, waganga, wenye nguvu za miujiza, wanasaikolojia, na wenye kufanya mambo ya kichawi (Wachawi).
🔮 5. Wewe kwa ujumla
Jinsi ulivyo
-
Msiri sana, Mwenye machale, Mwanandani.
-
Una nguvu sana kihisia
-
Mchunguzi sana na mkali wa saikolojia
Mkimya lakini ni mwenye mvuto wa watu
Umebarikiwa nguvu ya Kiroho
-
Ni mwenye kuelewa nishati ya eneo uliopo (Mf; kuna jini, mchawi, muongo n.k)
-
Ni kioo (ambaye watu wakikuangalia wanahisi unawajua kabla hawajajieleza.
-
Hueleweki na ni fala kihisia
-
Una uwezo wa kusoma akili za watu na kubashiri matokeo yao.
Ndani yako
-
Una hisia kali (Ukipenda umependa)
-
Mapenzi yako ni yakufia
-
Una kumbuka kila kitu cha kihisia si mwepesi kupotezea.
-
Ni mwenye kuhisi hatari upesi
-
Huwezi kuvumilia mahusiano ya juu juu
-
Ni mwenye kubeba mizingo ya kihisia ambayo ukimpa mtu hawezi kuimudu
-
Roho yako ni kama mzee mwenye hekima.
Giza lako
-
Si, Muaminifu kihisia (Kutokana na kukosa usalama kihisia)
-
Unaogopa sana usaliti
-
Unajikinga kuumizwa kwa kuachana na mahusiano.
-
Mgumu kuamini mtu
-
Ni mwepesi kuathiriwa na kudanganywa kihisia
-
Muda mwingine ni mtu una hukumu mapenzi kupita kiasi (Usipoangalia utakufa peke yako)
💕 6. Mahusiano yako
Ni mtu unatamani:
-
Hisia za ndani sana kwenye mahusiano ambazo ni ngumu kupata.
-
Uaminifu sana
-
Ukweli na uwazi kwenye mapenzi.
-
Unapenda mtu ambaye ana elimu za kiroho na muelewa kiroho.
Katika mapenzi:
-
Ni muaminifu kupitiliza
-
Ni mwenye kulinda sana mapenzi na kujitoa sana kwenye mapenzi
-
Una uwezo wa kujua mwenza anataka nini kabla hajasema
-
Mapenzi yawe ni kama haki sawa na ya kiimani sana na yaliyojaa huba.
-
Unapenda kuiga hisia za mwenza wako
-
Unapokosa uhakika wa mapenzi ni mtu unapenda kupelekeza mpenzi wako.
Shida zako.
-
Huamini mtu yoyote kirahisi.
-
Unaogopa muda wote kuumizwa.
-
Kumletea wenge mwenza na mwisho wa siku hukukimbia au kukuacha.
-
Unataka uachwe kwa muda/Muachane ili akili yako ikae sawa
Mwenza wako atakuwa:
-
Mtu mwenye hisia kali.
-
Mwenye mambo ya kiimani na mtulivu kiroho.
-
Hata eleweka au kuelewana na watu kirahisi.
Ni mtu ambaye wote wawili mtakuwa ni watu mnafanana historia za maisha ya nyuma.
💼 7. Kazi yako
Kazi unazovutwa nazo zaidi;
Saikolojia, Tiba, Utafiti, Maajabu ajabu ambazo kwa ufafanuzi ni kama ifuatavyo.
-
Mwanasaikolojia
-
Tabibu wa hisia za watu (Therapy)
-
Mshauri
-
Mnajimu
Msoma ramli
Meditation au kazi za kutibu
-
Nguvu za kiroho au kutibu kiroho.
-
Tiba za Ngono (Tantra)
-
Upasuaji, Madawa, Nesi.
-
Mpelelezi
-
Mtafiti wa kisayansi
Akili yako inafanya kazi zaidi katika kutafuta maswala yaliyojificha kama vitu vilivyofichwa au havionekani hata mali za maficho.
💰 8. Mlango wa nane katika Pesa na Utajiri msukumo wake.
Nguvu yako:
-
Utajiri wako unakuja kupitia:
-
Kurithi
-
Mpenzi (Mwenza)
-
Mali ya pamoja
-
Kupata kwa ghafla
-
Pesa za siri au pato la siri (Mf; Chuma ulete au ndagu)
-
Mitihani ya kipato:
-
Ni mtu mwenye kupata ghafla na kupoteza ghafla
-
Msongo wa mawazo ukiwa na mali za kushirikishwa
-
Unatakiwa ujidhibiti sana na maswala ya mapato.
⚕️ 9. Afya yako
Akili yako ndio inayotesa zaidi mwili wako. Matatizo ambayo unaweza kuwa nayo;
-
Wasiwasi wa mfadhaiko
-
kukosa kulala kwa utulivu
-
kuzidiwa kihisia
-
matatizo ya kusaga chakula
Mabadiliko ya homoni
kundalini yako kuamka na kuzima mara kwa mara bila kutaka
-
Kunyonya hisia za maumivu za wengine, Ukikaa na mtu anaugulia kitu unaanza na wewe
Unatakiwa uwe unajitakasa mara kwa mara kiroho kwa maana wewe ni sumaku ya matatizo ya wengine.
🧬 10. Majaliwa yako
Position hii ya mwezi unatakiwa sana ujue kuwa kwa wale wanaoamini waliwahi kuishi maisha ya kabla na sasa wamezaliwa sehemu nyingine basi wengi wao hii imani huwa nayo wenye position hii (Lincarnation) ambapo Roho yako inakuwa na ujuzi wa kuzaliwa nao ambao kwako ni:
-
Hisia zako mwanzo uliwahi kuzitumia vibaya
-
Uliwahi kujihusisha na uchawi au mambo ya kiroho
Bado roho yako inaugulia kutengwa au kukosa.
-
Ulikuwa mponyaji, nguvu za kiimani, mganga, mtenda miujiza au mchawi.
Hivyo kwa experience hizo kwa sasa roho yako:
-
Inapingana na mengi yaliyokuangamiza ili kukuponya kihisia
-
Kuamka kiroho katika njia sahihi
-
Kujifunza kuamini
-
Kuvuta tena nguvu yako ya ndani
-
Kubalance matakwa yako kuyapata katika hali isiyokuja kukuletea utulivu
Tunapoendelea na nakshatra yako hapa kwako ni kwamba; Nakshatra yako inakuwa ni Krittika ipo katika nyota ya Taurus (Ng'ombe) ambayo pia tunaona kuwa imeingia katika degree ya 5:25 katika mlango wa nane yaani;
Moon in Krittika Degree 05:25 Taurus in 8th house pada 3 ld/sl su/me
Hivyo position hii inatuonyesha kuwa;
Jambo la kwanza ni Moon in Taurus (Hii ni position ambayo mwezi unakwa umeinuliwa)
Hivyo hapa tunaona kuwa ni mtu mwenye hisia kali sana;
Kumbuka Ascendant ni Watu wanavyokuchukulia au muonekano wako au vile ulivyojiweka.
Sun Sign ni Uhalisia wako.
Basi tunapoangalia moon sign huwa ni ndani yako (Moyoni mwako).
Tukija katika Moon Nakshatra huku tunaangalia ramani ya roho yako (Ramani yako kiroho)
Hivyo katika position hii tunakuona kuwa ni mtu ambaye mwenye hisia kali:
Muonekano ambao wa kujiamini, kumbukumbu kubwa, mwenye kutulizana na jambo (msimamo) pia mwenye hisia kali katika mipaka na kujilinda, ikiwa ni pamoja na kupenda chakula kizuri, hisia za kugusa kitu na msawazo wa mambo.
Lakini mara nyingi hali hii hubadilishwa kwako kulingana na Nakshatra ya Krittika inapokuwa kwako katika mlango wa 8th house hivyo badala ya amani zinazoletwa na msukumo wa nyota ya ng'ombe katika position hii.
Unakuta ni mtu ambaye ni mwenye kupenda amani na usalama lakini maisha yanakuwa yanakulazimisha kubadirika.
Nakshatra hii inatawaliwa na moto na asili ya moto ni Jua na mara nyingi hukutia majeraha kihisia na kukuchoma kihisia lakini pia hukutakasa.
Hii inatuonyesha kuwa ni mtu ambaye unapokuwa hisia zako zimeumizwa akili yako hufanya kazi maradufu na inakuwa na uwezo mkubwa wa kuona uongo wowote ule ikiwa ni pamoja na kutokukubali unafiki.
Basi pindi unapokuwa umeumizwa roho yako hutawala na kukusababishia kujitenga na kuwa mkimya na hivyo katika kipindi hicho unakuta ni mtu ambaye unachoma kila hisia za udanganyifu hasa hasa katika familia na ndugu ikiwa ni pamoja na maswala ya mahusiano.
Mwezi katika mlango wa 8 unatuonyesha kuwa;
Mlango wa nane ni mlango wa kifo, ufufuo (Kuzaliwa upya) kiwewe, kuumizwa, saikolojia,maisha yaliyopita na uchawi.
Mwezi katika position hii unakuwa unamaanisha kuwa; Ni mtu ambaye utakuwa unaendelea kwenye maisha yako huku ukiwa na donda rohoni la toka utotoni, hisia kali za machale,
Ni mtu mwenye uwezo wa kuhisi maumivu ya watu wengine na unavunjika moyo ghafla kwa maswala ya kihisia
Lakini pia;
Ni mtu ambaye unaweza kuponya, kushauri, kutafiti, kufanya mabadiriko, kuondosha kiwewe.
Katika Purpose yako ya maisha umejaliwa kutembea katika njia ngumu na kupitia hiyo unapata hekima na kutoka kwa hekima.
Pada 3 katika position hii tunaona kuwa; Inakufanya kuwa ni mwenye focus kubwa ya mahusiano, Kuvutwa katika mapenzi na mtu ambaye ni majaliwa yako kinyota, Mara nyingi katika maisha yako utapitia vipindi ambayo havikai sawa katika mizani, Usaliti, Hisia za kudaiwa katika mapenzi.
Lord/Sub Lord (Sayari yako tawala na sayari iliyochomoza): Ambazo ni Sun / Mercury (Jua na Atwarid)
Hapa zinatuonyesha kuwa ni mtu ambaye unaongozwa/kupelekeshwa na;
Jua (gubu, kiburi, mabavu, mizani ya baba, msukumo wa takwa la kiroho)
Atwaridi (Akili, Mawasiliano na uchambuzi)
Sayari hizi mbili zinajenga kwako;
Kujielewa zaidi, kuzidiwa na mawazo, kujisemea na nafsi yako kama vile unaongea na mtu (Mawazo au fikra zako ni kama unabishana na mtu)
Msukumu wa kutaka kujua kwa nini watu wanakutenda wewe (Kukuumiza)
Karma ya Baba yako, walimu au wanaume wenye nguvu.
Hii ikiwa na maana kwamba roho yako ni sawa na baba au mwalimu uliyerithi kutoka kwa wanaume wenye nguvu.
Hivyo kwa sasa katika maisha yako unatakiwa kujitahidi kuongea ukweli hata kama utakuuma mwenyewe.
Vile vile nakshatra yako inaonyesha kuwa ni mtu ambaye ni mwenye kuogopa kuachwa na kutengwa hivyo hili hukupelekea kufukuza watu kihisia kwa kuhisi ni muda wowote wanaweza kukutenga au kukukalia kimya kwenye maisha.
Ni mtu mwenye kupenda kupima uaminifu wa watu;
Hupendi kufanya mambo ya juu juu, ni mwenye kutaka kufanya kila kitu au ni bora uache kama itakuwa ni nusu nusu.
Position hii pia inaingia katika maisha yako ya zamani;
Hapa wengine wenye kuamini katika lincarnation yaani maisha mengine baada ya kufa tunaangalia roho yako ina akili gani ya kuzaliwa (Hivyo tunaweza kuona hapa pia maisha ya nyuma wewe ulikuwa nani au roho yako inajua nini kabla)
Katika position hii unaonekana ni mtu ambaye unaujuzi mkubwa juu ya usaliti na roho yako ina ujuzi mkubwa juu ya uponyaji, kutoa fatwa au kuhubiri, ushauri nasaha maarifa ya kiroho.
Hizi ni fani ambazo zimejificha katika roho yako.
Hivyo kwa experience hizi ulizonazo kiroho:
Tunaona kuwa katika maisha ya sasa ni mtu ambaye una wito wa kujifunza hisia za uaminifu kwa watu bila kupoteza nguvu yako.
Purpose yako ya kiroho;
Ni mtu ambaye roho yako inatafuta ponyo la kiwewe ili usiendelee kuweweseka katika maisha uliyonayo,kuvunja kila kile ambacho kinataka kukuvuruga katika maisha yako sasa kiroho.
kutumia maumivu ya kihisia kama charge ya kuamka kiroho. Ni mtu ambaye hujaandikiwa maisha rahisi isipokuwa ni mtu ambaye umeandikiwa maisha yenye maana zaidi. Hivyo Purpose yako kiroho ni kutafuta maana kamili ya wewe kuwepo eneo husika na sio kustarehe eneo husika.