Ruka kwenye yaliyomo

Mahusiano kinyota Nyota ya Mizani na Kondoo (Libra and Aries )

Mwanamke akitabasamu — Mahusiano kinyota Nyota Mizani Kondoo
Picha: Pixabay

 Huyu Shufaa ni soul mate wako kinyota kwa maana nyota zenu zinaendana sana na ni mwanamke sahihi sana kwako kinyota, Ingawaje ni mtu mwenye pupu hasira za karibu, kupenda kujiweka kama kiongozi katika mahusiano au mwanaume na kadhalika..

Mahusiano yako na yeye kwa utangamano naona kuwa:

Mtizamo wako kwake;

Ni watu ambao kwa haraka kila mmoja alivutika na mwenzio kihisia, lakini hivyo hivyo ndivyo ambavyo mvutano pia hutokea upesi kwenu. Wewe ni Mwenye kutafuta furaha na amani katika mahusiano au ndoa, Wakati yeye ambaye hajatulizana na kupenda ushindani na kutafuta mambo mapya kila mara.

Wewe mara nyingi unamuona yeye kama mkorofi na asiye na busara; Yeye anafikiria kuwa wewe ni mtu ambaye hupendi kukubali ukweli/kuambiwa ukweli.

Yeye ni mtu ambaye anataka kuaminiwa na kuskilizwa yeye tu na awe huru katika kila analotaka kufanya na kutawala peke yake mapenzi. Na ugomvi mara nyingi huzuka katika hali ya wewe kusita sita katika kufanya maamuzi ambayo yeye anakuwa kayawekea msukumo.

Yeye hujiweka na kuamini kuwa ndio mwenye mapenzi makubwa sana kwako na wewe humpendi kwa dhati, Mahusiano yenu ni mazuri ingawaje ni kwa muda, na baadae huwa mtihani.


Mtizamo wake kwako;


Kuna mvuto mkubwa wa awali kati yenu wawili tukiangalia pande zote mbili a mambo haya mawili yanayopingana, kwani katika maeneo fulani kila mmoja huweza kutoa kile ambacho mwingine anakosa.

 Kwanza, jinsi alivyo na uchokozi wa katika mapenzi wakati mwingine huamsha uwezo wako wa kihisia.

Maisha yenu ya kimapenzi yanaweza kuwa yasiyo ya kawaida. Hata hivyo, yeye anajua kabisa kuwa wewe unataka amani, utulivu, na maelewano, na hali ya kuwa yeye ni mtu wa kupenda vitendo zaidi na matukio. 

Nyote ni watu wenye kupenda maisha ya kijamii, burudani, na raha, lakini wote wawili hamna utulivu kwa njia tofauti.

Baada ya muda, Wewe ni mtu ambaye utatafuta mtu mwingine asiye na madai au demands nyingi katika mapenzi na hili anajua wazi.

Na yeye atatafuta mtu mwingine wa kumliwaza anayempenda zaidi. Mapenzi yenu huwa moto sana lakini ndoa huwa ni duni (mbaya).
Rakims Spiritual
Imeandikwa na

Rakims Spiritual

Kufahamu zaidi pia niandikie kupitia Rakimsspiritual@gmail.com

Kuhusu Sisi →
Tunatumia cookies kuboresha tovuti yetu. Kwa kuendelea, unakubali matumizi yake. Soma zaidi
📱 Pakua App