Hamuendani mkuu japo ni watu mahusiano yenu yamejaa raha utani na maelewano ya hapo hapo kisha mkipeana nafasi imeisha hiyo wewe ni msaliti na yeye ni msaliti mzuri tu, Haijarishi mtaficha kwa muda gani.
Tunapokuja kwenye suala la kununua vitu yeye ni mtu anataka kujenga na kuweka sawa maisha yake ya baadae haijarishi ni maskini au tajiri.
Wote nyie ni wenye akili nzuri lakini katika mitizamo miwili tofauti wewe ni mwenye kujitanua na mwenye maisha ya fujo na yeye ni mwenye kupendelea urahisi wa mambo na mipangilio na kutokujitesa.
Wewe kuna muda unamdhania yeye ni mjinga haelewi vitu au hajajua mambo hivyo hamna maisha marefu ya kulala shuka moja kati yenu.
Huu ndio mtizamo wake kwako kinyota.