Mars in the 6th House
Mlango huu wa sita unawakilisha kazi, huduma, afya, maadui, washindani, shughuli za kila siku, na adabu.
Athari zake ukiwa hapa
-
Tunaona kuwa linapokuja swala la mijadala basi ni mtu ambaye ni mshindani, mfuatiliaji sana, mwenye uwezo mzuri wa kujieleza na kuwa na uwezo wa kufanya kazi zinazotaka stamina.
-
Ni mtu ambaye una uwezo mkubwa wa kuwashinda maadui, vikwazo na vipingamizi kwa ujumla.
-
Nguvu kubwa katika kutimiza kazi zako;ni mbora katika kazi za mzunguko na kufuatilia mambo
-
Unaweza kufanya vizuri katika kazi za kushughulika na watu kama vile, kazi za utabiti, kuwafanyisha mazoezi au kazi za shughuli za technique mbali mbali mradi tu ziwe ni za kuwavusha watu kutoka katika hali moja kwenda nyingine.
Unakuwa na matatizo na ni dhaifu katika matatizo yanayohusiana na mlipuko au ghafla kama vile matatizo ya koo au shingo na sehemu za shingo.
-
Ni mtu mwenye kupenda muundo na utaratibu sahihi wa mambo; hupata wasiwasi wakati mambo yanapokuwa na hali ya mchafuko/machafuko
Position hii hukuletea ushindi hasa wa madai, ujuzi mzuri wa kutatua matatizo, na nidhamu ya kila siku.