.png)
SAMAKI NA MBUZI:
Mahusiano Kinyota
Inaonyesha kwamba nyie wawili ni watu tofauti, ambapo kila mmoja anajitahidi kumfurahisha mwenzake. Yeye ana asili ya utawala, nafasi nzuri ya kukuridhisha, na utu wenye kukufurahisha.
Wewe unaonekana unapendelea kulindwa kwa vitendo badala ya maneno. Hivyo basi, yeye ana uwezo wa kukulipa hitaji lako kihisia na kukukamilishia upendo na faraja unayohitaji. Kwa upande wako, ujira wake ni pumzi ya mahaba, mawazo ya maisha, ushauri na support ambayo wewe huna tatizo kumpatia, bila ajizi kwake.
Mtindo unaotumia katika suala la anasa ni kitu kinachompendeza yeye. Mtizamo wako juu ya anasa unamfurahisha, na utaratibu wako wa kutumia asili ya upole na imani ni faraja kubwa kwake.
Wakati mwingine yeye hushindwa kueleza hisia zake kikamilifu, lakini tayari wewe umeshazielewa hata kabla hajamaliza kueleza. Hii ndiyo sababu nyingine inayoongeza mapenzi yake kwako. Aidha, ni rahisi kwako kuelewa shauku yake na uaminifu wake kwa sababu imani ni jambo muhimu sana kwako.
Huyu mtu wa siasa na uongozi unaonekana kummudu vyema, ingawa yeye ni msiri katika kuweka mambo wazi. Ngono katika mahusiano yenu ipo sawa, na tofauti za tabia au mitizamo yenu ndizo zinazokamilishana kwa ustadi.
Kwa ujumla, haya ni mahusiano ya kistaarabu sana. Hakuna jipya wala baya; nyie ni watu wa kawaida mnaoishi kwa kuelewana.
NOTE:
Ikiwa unahitaji kutazamiwa nyota yako na mwenza wako, au mtu unayetaka kuhusiana naye na kujua mtaendaje, usisite kuwasiliana nasi.
Gharama: Shilingi 5,000
Kwa Mawasiliano na Huduma:
Email: rakimsspiritual@gmail.com
Email: mnajimu@unajimu.com