SIMBA NA NG'OMBE
Mahusiano haya Simba haki yake ya kutaka uhuru na kutawala mahusiano inakuwa inaendeshwa na kujaribu sana kupingana dhidi ya dhamira ya Ng'ombe kutaka kupeleka mambo jinsi anavyotaka yeye.
Wawili hawa wote ni wenye nyota thabiti yaani zisizopinda hivyo hakuna ambaye atataka kupindishwa na mwenzie jinsi anavyotaka mambo au kurekebishwa vita huanzia kwenye tabia ya simba ya kutaka usafi na Ng'ombe usafi wake ni wa nje tu.
Utakuta mara nyingi Simba anakuwa ni mwenye kughadhabishwa na Ng'ombe na Ng'ombe zaidi anakuwa na kiburi chake cha asili.
Utamshangaza kwa tabia yako ya matumizi ya kujiachia na hali ya kuwa yeye ana asili ya Ubahiri na uchoyo hata kwa wazazi pia. Yeye ni mwenye tahadhari kubwa na makusudi sana;
Wakati wewe ni mwenye kupenda kujitanua na kujiachia kupita kiasi.
Asili ya Simba hupenda kutukuzwa kama mfalme sasa kwa yeye Jeuri utakuta kila mara anakupinga kiuhalisia huyu kwako ni mpinzani na wala sio mpenzi haijalishi mna mapenzi kiasi gani au umemfanyie nini baadae atakuona hufai tu. Na pia wewe ni mfalme binafsi hivyo kunyenyekea yoyote kwako sio rahisi zaidi unapenda kusikilizwa na kuheshimika.
Mnapoelewana zaidi ni wakati wa kufanya ngono tu.
Ubinafsi mwingi sana kati yenu na ndio kitakacho wagombanisha maana hakuna kati yenu anaekubali kuambiwa ukweli kama ni mbinafsi lakini wote nyie wabinafsi.
NOTE:
Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:
Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:
Email: rakimsspiritual@gmail.com
: mnajimu@unajimu.com
WhatsApp +255 783 930 601
Rakims