Mahusiano kinyota Ng'ombe na Ng'ombe (Taurus and Taurus)

Rakims

Ng'ombe na Ng'ombe 

(Taurus and Taurus)


Utangamano 


Hii ni moja kati ya mahusiano yenye kuvutia sana, kwa maana wawili hawa ni wenye kupenda maajabu sawa na salama katika mahusiano.
Walakini wote wanashare na kusaidiana mapato,matumizi,kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na mvuto wa kila mmoja kwa mwenzie. 

Tamaa na hali za wawili hawa kwenye mahusiano huwa sawa na mara nyingi mwanamke hapa huwa na hisia zaidi kuliko mwanaume ambacho ni kitu kizuri pia na wao utaona ni wenye kuendana kwa maswala ya mapenzi kila kitu tofauti na nani anampenda mwenzie zaidi.

Hii ni kwa maana wawili hawa wote ni wenye nyota moja yenye asili ya udongo na wote wawili linapokuja suala la kukutana kimwili basi utaona ni wenye kepeana direct bila kunyimana wala kubaniana au kufanya ajizi.
Wao kwenye maswala ya chumbani utakuta hakuna tatizo wala kasoro ukitaka utapewa tu, hata wakikasirisha basi wanapokuwa chumbani mwenzie akianza kuomba basi humpa na kesi huishia hapo.

Kila couple ina udhaifu wake na hii kwenye suala la kuchoshana kwao ni tishio hawa huwa tunashauri kila mmoja ajitahidi kuwa na marafiki wa nje ambao hawataweza kuibua hila za mwingine.

Ama katika nyota za watu wenye hila zaidi ni hii ya ng'ombe hivyo mapenzi yao huchanua kwa nafasi kubwa kila mmoja kwa kulinda hila ya mwenzie isitokee.

Hila hapa kwa maana nyingine inaweza kuwa ni vitimbi.
Hivyo mlinde mwenza wako asianze vitimbi maana nyota yenu hii inavitimbi sana kwa wenza na hata kwa nyinyi wenyewe kwa wenyewe.

NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:

Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !