Mahusiano nyota ya Mshale na Samaki (Sagittarius and Pisces)

Rakims

MSHALE NA SAMAKI

Sagittarius & Pisces

Baina ya nyie wawili wewe ni Moto wa nyasi na yeye ni Maji ya kisima kwa maana hii yeye atavutiwa zaidi kwako kulingana na nguvu yako ya utafutaji wa maisha, na vile vile wewe utavutiwa nae zaidi kwa mtizamo wake wa kiimani na mambo ya kiroho.

Ukweli ni kwamba katika mahusiano wewe unahitaji mwenza ambaye ni kama mshkaji na yeye anahitaji mwenza ambaye ni kama mwenye ndoto za mapenzi yaani mapenzi muda wote mfano mwanaume wa ndoto zake nyote wawili hamuendani kwa maana kati yenu hakuna anaeweza kumsaidia mwenzie katika mahitaji yake 

Asili yako ya roho ya uthubutu na kujitoa utakuta inakwamishwa sana na yeye ambaye ni tegemezi zaidi kwako na uoga wake pia

Yeye ambaye huwa na hisia kali sana muda wote hata kuona unamapenzi nae zaidi ya kumtaka akutimizie haja zako kingono tu, vile vile atakuona ni mtu ambaye hujatulia mambo mengi na vile ulivyo ni mtu wa kupenda uhuru basi moja kwa moja utajiwekea akilini kuwa huyu ni wa kuwa nae tu kwa muda kisha utatafuta mwingine lakini mahusiano yenu taratibu huanza kuzama mfano umemwaga maji kwenye mchanga kila mtu ataangalia uelekeo wake. ndio ndoa hizi mara nyingi watu wanakuwa pamoja ajili ya kuangalia matumizi na watoto tu lakini ni ndoana.

NOTE:
Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:


Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !