Katika mlolongo wa nyota 12 basi kuna nyota tatu ambazo hizi ni nyota zenye bahati zaidi kuliko zingine na zenye mafanikio zaidi katika bahati nasibu;
YA KWANZA:
Ya kwanza ni nyota ambayo ukitizama kwenye mfumo mzima wa nyota 12 basi utakuta inatawaliwa na sayari ya bahati.
Ambayo ni sayari tegemezi kwa wengi kuangalia bahati zao zipo wapi na safari zao za maisha ziko vipi na hata aspects za matarajio ya mtu yaani aspects za future yake huangaliwa hapo.
Msikufuru aspect inayozungumziwa hapa ni viewing ya mafanikio ya mtu. Hivyo nyota ya kwanza kabisa katika nyota 3 zenye bahati tutaipa nyota ya Kausa yaani Saggitarius ama kwa kiswahili ni
Mshale
ambapo mshale ni nyota ya 9 katika mlolongo wa nyota 12 nayo ni nyota yenye bahati zaidi kuliko nyota zote.
Kila nyota ina sifa zake lakini kwa bahati ni nyota hii inayo milikiwa na Sayari ya mapato na iliyoko chini ya usimamizi wa malaika Israfiil ama Rafael kwa wakristo.
Nae ni malaika mwenye kupuliza baragumu siku ya Qiyama yaani Judgement Day au Siku ya hukumu.
Ukikuta una nyota hii na huna bahati. Basi rekebisha bahati yako
Kwa maana bahati yako hukwamishwa na mahusiano (Mwanamke/mwanaume) achana nae. Maana utajikuta kwa uchumi kila unalofanya hufanikiwi
na hata ukiwa kwenye mahusiano ni mkosi mtupu heri yako wewe ni ndoa maana ukiwa kwenye mahusiano pesa hazikai mkononi na unakuwa ni mwenye kusingiziwa maneno. na ukiwa mzinzi basi mizimu itakusumbua sana hivyo utatakiwa uchague kati ya Mwenyezi Mungu au Mizimu.
Na ukichagua mwenyezi Mungu umeshukuru Ukichagua mizimu umekufuru za kuambiwa changanya na zako.
YA PILI:
Yapili ni nyota ambayo ukitizama kwenye mfumo mzima wa makundi nyota 12 ni nyota inayo tawaliwa na sayari ambayo hutizamwa na wanajimu wote kama sayari ya Mapenzi na mahusiano zaidi
Na hii ni nyota yenye kutawala mlango wa saba yaani mlango wa Mahaba na mahusiano ya mtu hivyo, katika bahati zaidi tutaipa nyota ya Saba ambayo ni nyota ya Miizaan ama Libya ambayo kiswahili ni Mizani
Hii ni nyota ambayo inatawaliwa na Sayari ya Zuhura amba Venus ambayo inakuwa chini ya usimamizi wa malaika An'yail ama Hananel, jina lingine ni Anael ama Aniel
Ambaye ni malaika anaetawala na kusimamia doria mbinguni inaamika kwa imani za wengine kuwa ni malaika anaesimamia hisia za watu katika mahusiano ya ndoa na mapenzi.
Hivyo kwa bahati tunaipa nafasi ya pili nyota ya Mizani.
Ikiwa una nyota hii na huna bahati basi Punguza Ukatili, Hamaki na Umalaya na ujitahidi kudumu katika mahusiano maana ukiendekeza hayo bahati yako huja uzeeni unapokata tamaa. Jitahidi kushika ibada
YA TATU:
Ya tatu ni nyota ambayo ukitizama kwenye mfumo wa makundi nyota 12 ni nyota inayotawala NYOTA ama kwa maneno ya kinajimu huitwa sayari pia.
Yaani the Sun (Jua) ambayo ni msimamizi wa nishati bora ya asilia ya uhai.
Ambapo kinajimu ni sayari inayohusishwa na Utajiri tofauti yake na Sayari za nyota mbili zilizopita.
- Jupiter ni sayari ya Mapato
- Venus ni sayari ya pesa
- Sun ni Sayari ya Utajiri