Punda na Ng'ombe
Mahusiano haya ni mshike mshike baina ya mbingu na ardhi au magharibi na mashariki na haijulikani hadi leo ni nini kina waunganisha,
Kipo kinacho waunganisha tofauti na mapenzi ya dhati mara nyingi hata mimba hutokea bila kujipanga,
Mtizamo:
Nyote wawili ni wenye hisia lakini wewe ni mwenye kuwa annoyed na makusudi yake ya ufanyaji mapenzi.
Yeye ni mtu wa kupenda kukaa nyumbani jina lake la utani kiroho ni manyama uzembe yani mvivu na wengi wao huwa ni wenye usafi wa nje tu.
Wakati wewe ni tofauti na yeye, wewe ni mwenye mihemko na msukumo wa kutoka na kupenda mambo mapya na ya sasa hivi sasa hivi bila kuchelewa na pia kupenda uhuru bila kubanwa banwa.
Yeye ni mwenye wivu mkali na pia ana husda ya chini chini na hutaka mambo yaende jinsi anavyotaka yeye na mambo yake ni mwenye kupenda mwenyewe jinsi ya kufanya mambo anavyotaka na hujiweka kwenye kivuli cha dini na hujifanya wanaroho safi lakini hamna kitu hawa ni sawa na kuishi na mafia bila kujua. Na anapokuwa na wewe mwenye msimamo hukuona kama vile ni mbishi na kiburi husikii ya wengine hali ya kuwa yeye ndio mwenye kiburi na gubu,
Japo kuwa yeye ana bahati sana ya kutengeneza pesa. Lakini wewe ni mzuri katika kuponda pesa, Ukipata pesa matumizi yako ni ya hali ya juu sana, zinayayuka kama moto na pale zinapoisha roho yako ndio hutulia.
Safari ndefu ya mapenzi inaweza kuwa ngumu kwenu kwenda, ingawa mkiishi sana itafikia sehemu utapenda style yake ya matumizi na kujinyima ili kufanikisha maswala ya nyumbani.
NOTE:
Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:
Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:
Email: rakimsspiritual@gmail.com
: mnajimu@unajimu.com
WhatsApp +255 783 930 601
Rakims