Mahusiano nyota ya Nge na Mapacha (Scorpio and Gemini )

Rakims

 Nge na Mapacha / Compatibility

Wewe ni mwenye kuvutika nae kutokana na tabia yake ya uchangamfu na yeye zaidi kwako ni mwenye kuvutiwa na tabia na utata ulio nao. Kwa muda fulani utaona kuwa yeye anavutiwa zaidi na tendo la ndoa mnapokuwa pamoja yaani anavutiwa zaidi na vile unavyo au utakavyokuwa ukimfanyia. 
Lakini yeye ni kama kinyonga kwa maana ni mtu wa kubadirika badirika na hili lipo wazi kwake na hii inakuwa kwako ni ngumu ambaye wewe ni mtu mwenye asili ya msimamo na kutimiza jambo kwa ufasaha ukiamua kulifanya na wewe ni mpenzi kipofu yaani unasifa ya kuwa ukipenda umependa yaani una mapenzi ya kihindi,
Sasa kwa yeye ambaye kidogo ana udhaifu wa kutokutulia na mwenye tamaa ya maendeleo au vitu vyenye kuendelea ukilegeza kidogo tu basi huweza kukuondoka , wakati wewe ukiwa kwenye kuhangaika kumpata mpenzi ambaye utaweza kumtawala na kummiliki,
Kiuhalisia wewe una asili ya upweke na hupenda kujitenga na watu na mashughuli au mchanganyiko lakini yeye ni mwenye kupenda mipango ya nje na kupenda shughuli yaani kiguu na njia.
Mtakuwa na maisha mazuri kiasi ya furaha.
Lakini mapema sana utaanza kuona yeye anaanza kutafuta njia za kuachana ili akachakatie mbele.
maana kwako ataona ni sawa na jela.

 NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:


Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !