Mahusiano nyota ya Mbuzi na Samaki ( Capricorn and Pisces)

Rakims

Mbuzi na Samaki 

Mahusiano haya ni baina ya mchanga wa pwani na maji ya kisima kuna visima pia vinakuwa na mchanga wa bahari au mweupe chini hivyo couple hii inawezekana.

Mtizamo:

Wewe ni mwnye uwezo wa kutoa na kumpa katika kila sector ambayo yeye anatamani katika mahusiano kuanzia kumtimizia na kumkamilishia yale yote anayotamani katika mapenzi au kutoka kwako na wala hilo kwako sio tatizo hata katika kumfikisha kwenye tendo kwako ni rahisi sana na yeye kufurahia zaidi na husikia raha pale tu unapoonyesha dalili za kumtaka kimwili hata kama kakasirika utaona anaanza kulegeza uzi,

Nae pia ni mwenye kukutamani na hakuna kitu wewe unapenda kama kutamaniwa na yule uliyenae kwenye mahusiano yaani akionyesha tu hata kukutizama kwa jicho la huba wewe hoi.

Kama ilivyo kwa nyota yako kuwa na kutambulika ni nyota ya watu wa serikalini au viongozi basi ndivyo ulivyokiongozi mzuri kwake ambaye yeye hata ikitokea kampoteza hujihisi kuchanganyikiwa na huona maisha yake yameharibika kama kapoteza mzazi, ndio maana wengine utakuta wanakuwa wagumu kuingia kwenye mahusiano kwa kuhofia siku ya kuachana. Lakini yeye anakuwa na nia ya dhati ya kukufuata kwa yale unayomuongoza. 

Ingawaje mtasumbuka sana kwenye malezi ya watoto na matatizo ya uzazi lakini ikitokea hili limeenda sawa basi katika watu ambao watakao tamba kwamba oeni mpate kutulia na kufarijika wewe utakuwa ni mmoja wao.

Ladha yake ya ajabu katika mapenzi inaweza kukuathiri kisaikolojia pale mnapogombana ukaona mambo hayaendi ni vile utamu wake utakugusa sana rohoni kuliko kimwili. Mapenzi yake ukarimu na hisia zako kali za uaminifu vinachanganyika na kufanya kila mmoja ajisikie yuko salama na analindwa katika mapenzi na mwenza wake.

Hakika nyinyi ni watu wawili tofauti ambao mtakuwa mmekutana na mwenza sahihi kwa maana kila mmoja atakuwa ni mwenye kuvutika na kujiona kapata kwa mwenzie mtu sahihi.

 NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:


Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !