Mahusiano nyota ya Mbuzi na Mashuke (Capricorn and Virgo)

Rakims

Mbuzi na Mashuke

Capricorn and Virgo

Yeye (mashuke) ni msafi na akili yake imepangilika vema hasa akiwa na wewe (mbuzi) ambaye ni mwenye kujiheshimu na mwenye uwezo mkubwa wa wa kujituma. Nyote wawili ni wenye kuvimba yaani kujitanua ndani mwenu, na pia wenye kufurahia kuwa na marafiki wachache kuliko wengi, na mnapendezewa kila mmoja na tabia ya mwenzie, 

kiukweli haya ni mahusiano mazuri ambayo hata ukizingatia katika asili zenu yeye (mashuke) ni mwenye asili ya udongo mwekundu na wewe ni (Mbuzi) mwenye asili ya mchanga wa bahari licha ya kuwa na rangi tofauti lakini nyote ni wenye asili ya ardhi hiyo kupelekea nyie kuendana vema kwenye mahusiano.

Ukitizama nyote wawili ni wenye uwezo mzuri wa kuchambua mambo kiakili hata mmoja anaweza kutaka msaada wa ushauri unaotaka matumizi mazuri ya akili na hataweza kujuta. Hakuna sababu ya wawili nyie kutokuendana isipokuwa tu kitandani. ambapo yeye anataka uwe ni mtu mwenye nguvu zaidi kuliko kiasi ambacho wewe unaweza kumpa/kutoa. Ingawa pia ni mwenye kupenda mtu atoe mapenzi kwa uwezo wake yaani anaridhika ukijitahidi japo sirini atakuwa anatamani ukazane shida yako ya maradhi ya magoti na kuchoka maungo itakutaka uje upate madini na kito cha nyota yako ili kuzuia hili kusambaa kiroho hata kwa wenza wengine,

Vyovyote vile hii ni couple ambayo baadae utulivu na maelewano yapo tu haijarishi changamoto mtakazo kuwa mnapitia mwanzoni.

 NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:

Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !